Mafuta bei juu kuanzia kesho, baadhi wafunga vituo kusubiri bei mpya

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta(EWURA) imetangaza ongezeko la gharama za mafuta nchini kuanzia kesho Julai 05, 2016 kutokana na kupanda kwa bei ya nishati hiyo duniani.

Petroli itauzwa shilingi 1888 badala ya shilingi 1865 ya sasa huku Diseli ikiuzwa shilingi 1720 badala ya shilingi 1633 na Mafuta ya taa nayo yakiuzwa shilingi 1687 badala ya shilingi 1607 ya sasa.

Saa chache baada ya wafanyabiashara kugundua kupanda huko kwa bei baadhi ya vituo vimefungwa kusubiri bei mpya ambapo onyo limetolewa juu yao.

Mafuta.jpg
 
hii bei yako ni kwa mkoa gani............?........
 
Ni kweli, kuna mkoa wafanyabiashara wa mafuta wamefunga vituo kwa madai hakuna mafuta lakini EWURA imedai mafuta yapo
 
Bei imepanda lini huko duniani kiasi cha kuaffect bei ya nyumbani??
Ewura ni jipu
 
Bado hatujakoma tunasubiri nauli zipande, sababu tumewapaenda wenyewe wacha wele(sijui kinanani) waisome namba.
 
Sio kupanda kwa bei duniani iyo ni nyongeza ya vat 18% per bado na vingine tutasikia tu soon
 
Back
Top Bottom