Mafuriko ya dunia nzima kwa mujibu wa biblia

simplemind

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2009
Posts
16,691
Reaction score
9,578
Biblia inasema:Maji yalizidi juu ya mlima mrefu(Mt Everest?) kwa dhiraa 15(mita 7) (Mwanzo 7:20)
Ilikufunika hadi kilele cha Everest dunia ingehitaji maji ya ziada kiasi cha takribani kilomita za ujazo bilioni 4.5 mara tatu ya maji yote yaliyopo kwenye bahari sasa.

Changamoto iliyopo hakuna chanzo kinachojulikana cha maji haya yote, wala sehemu ambapo maji hayo yangeenda baada ya mafuriko kumalizika.

Naomba mwongozo wa wana elimu.
 
Mwandishi ni muongo..
Ukichambua kwa kina kwenye hivi vitabu uongo ni mwingi sana...
 
Biblia inasema:Maji yalizidi juu ya mlima mrefu(Mt Everest?) kwa dhiraa 15(mita 7) (Mwanzo 7:20)
Ilikufunika hadi kilele cha Everest dunia ingehitaji maji ya ziada kiasi cha takribani kilomita za ujazo bilioni 4.5 mara tatu ya maji yote yaliyopo kwenye bahari sasa.

Changamoto iliyopo hakuna chanzo kinachojulikana cha maji haya yote, wala sehemu ambapo maji hayo yangeenda baada ya mafuriko kumalizika.

Naomba mwongozo wa wana elimu.
Umesoma tu kidogo ukaja kuandika ukisoma zaidi biblia inaeleza ni wapi maji yalitoka na wapi yalienda chanzo hakikuwa mvua pekeyake
 
Tupe maelezo zaidi kwa faida ya Umma.
 
Mwandishi ni muongo au tafsiri yetu ya tukio siyo sahihi?
Si ndio hizo hadithi unaambiwa watu walitembea miaka 40 kwenda nchi ya ahadi, watu wenyewe walikuwa wakitokea Egypt kuelekea Israel... Egypt na Israel ni kama Tanzania na Kenya..

Kuna vingi ukijiuliza hupati majibu...
 
Biblia imesema ukosefu wa imani na mamalalamiko kibao ndio sabu ya Mungu kuwaadhibu wana israel adhabu ya "kuzurula jangwani miaka 40"
 
Hizo ni fiction za uongo na kweli ngoja nikupe kisa...

Kanisa Katoliki la Roma lilimpa adhabu Galileo Galilei, na sababu kuu ilikuwa ni mafundisho yake kuhusu mfumo wa jua.. heliocentric theory...

Galileo alithibitisha ushahidi wa kisayansi kwamba sayari, pamoja na dunia, huzunguka jua. Hii ilikuwa kinyume na imani ya wakati huo...

Kanisa Katoliki lilikuwa na ushawishi mkubwa katika masuala ya kisayansi, kifalsafa, na kijamii. Mafundisho ya Biblia yalionekana kuunga mkono wazo kwamba dunia ndiyo inazungukwa na jua... soma mhibiri 1:5 na Zaburi 104:5 ...

1633 Galileo alishutumiwa kwa kushikilia na kufundisha imani potofu kwamba jua halisogei na dunia ndiyo inayozunguka. Alilazimishwa kujiondoa kwenye imani hiyo hadharani, na inasemekana alijitetea kwa sauti ya chini akisema 'na bado inazunguka'....

Galileo alihukumiwa kifungo cha maisha cha nyumbani ,house arrest, na vitabu vyake vilipigwa marufuku. Aliishi chini ya uangalizi hadi kifo chake mwaka 1642.

Miaka mingi baadaye, Kanisa Katoliki lilianza kukiri makosa. Mnamo mwaka 1992, Papa Yohane Paulo II alikiri rasmi kwamba Galileo alihukumiwa kimakosa na kwamba Kanisa lilihitaji kujifunza kutokana na tukio hilo.

Yaani miaka yote hio kanisa kwa aibu limekija kukiri kumkosea Galileo mwaka 1992...

Always naamini katika sayansi ....
 
Back
Top Bottom