Mafuriko: Mama Tibaijuka adai hakukuwa na dhamira ya kisiasa kulinusuru bonde Msimbazi wakati yuko Ardhi

Mama Tibaijuka kwa kuwa wewe ni msikivu na "mcha" Mungu, nakushauri ukae kimya ili usiwatoneshe vidonda vya tumbo na ubongo Watanzania. Endelea kula hela yako yako ya "mboga" 1.5 Billioni. Hiki ulichoandika mimi kama MTANZANIA nimekipokea kama kejeli na matusi kwa Watanzania. Jitafakari Mama Tibaijuka.
 
Tatizo la hivi sio Dar tu ni nchi nzima
Sehemu ambazo maji ya mvua yalikuwa yanapita yamefungwa kwa kugawa viwanja na bila kuweka hata madaraja ya uhakika na matokeo yake ni uharibifu mkubwa wa barabara

Na hii inaigharimu tena serikali kutengeneza tena kwa gharama za kila mwaka
Sio ujinga wa mwafrika tu bali ni wizi waliouzoea (dili)

Hela zitaliwa kila mwaka na ni kila mahali
 
Sasa mama kwako kila kitu kilifeli au? political will kutoka kwa nani tena wakati wewe ulikuwa kwenye baraza la mawaziri? vipi na ile project ya kigamboni satellite mliyotuaminisha nayo tena hakukuwa na political will au?
Hahahaa kigamboni sattelite city the blue diamond mpaka leo video yao nnayo nzuri kweli.
 
Nimefurahishwa na uzi huu unaobeba mawazo ya Profesa Anna Tibaijuka kwa sababu tatu.

Kwanza, ndio jana nimetoka Dodoma na kushangaa maamuzi yaliyofanywa na uongozi wa mkoa huo kuhusu mabasi ya usafiri wa umma yanayotoka na kuingia mkoani humo. Abiria wote wanapaswa kushuka stendi ya NANENANE kilometa 1o kutoka Nyerere Square, kati kati ya Dodoma, au Dodoma Mjini, ambako ni kituo cha kawaida cha mabasi. Kisha, daladala zilizopo stendi ya NANENANE zinabeba abiria kuwapeleka kati kati ya jiji. Basi lililoshusha abiria linaingia kati kati ya jiji likiwa tupu kuwaletea mizigo yao.

Ni vivyo hivyo kwa mabasi yaliyo na vituo kati kati ya Dodoma. Abiria wanapandishwa daladala mpaka NANENANE, wakati basi watakalolipanda linakuwa likiwasindikiza nyuma likiwa tupu. Abiria wanalipanda basi hili baada ya kuwa wameshushwa stendi ya NANENANE.

Madereva na Makonda wameniambia kuwa Mkuu wa Mkoa ametoa maelekezo hayo kusudi hata bodaboda na daladala za Dodoma zipate riziki. Nilimsikia kondata mmoja akisema "ama kweli viongzi wahenga wana mambo."

Pili, hapa Dar es Salaam, tangu stendi ya Mwenge ihamishiwe Makumbusho, na pia tangu stendi ya Simu/2000 (Mawasiliano) ijengwe, kumekuwa na ruti za ajabu jijini Dar es Salaam. Sijawahi kuelewa ni mantiki gani ilisababisha stendi ya Mwene kuhamishwa. Hata Makonda aliwahi kuonyesha kukerwa na jambo hili. Akaahidi kuirudisha stendi ya Mwenge haraka iwezekanavyo. Ahadi ya Makonda mpaka leo haijatekelezwa.

Na tatu, nakumbuka kuwepo kwa taarifa kuwa Prof. Anna Tibaijuka aliitwa kutoka Nairobi, Ofisi za UN-HABITAT, ili aje Tanzania kusimamia Wizara ya MIpango Miji, chini ya Rais Jakaya Kikwete. Lakini, wakati JK anaunda Wizara zake akabadili mawazo na kufuta mpango wa Wizara hiyo. Prof Tibaijuka akaishia kuwa Waziri wa Ardhi.

Hata hivyo, bado tatizo la mipango miji ni kubwa. Hapo juu nimeonyesha shida katika upangaji holela wa vituo vya mabasi. Lakini kuna ujenzi holela, uvundo wa taka ngumu, na mambo kama hayo.

USHAURI KWA BOSI KUBWA: Iundwe Wizara ya Mipango miji ili kurekebisha hali hii. Sisema kuwa Prof Tibaijuka awe ndiye Waziri wake, lakini kama anazo sifa sio vibaya akapewa Wizara hiyo. Hata hivyo, wako wataalam wengi wenye ujuzi huo, japo uzoefu utakuwa chini ya ule alio nao Prof. Tibaijuka. Kama aliyoyasema juzi Msemaji wa Serikali, Mr. Abbas, kwamba Bosi Kubwa siku hizi anashaurika, ni maneno ya kweli, basi ushauri huu usibaki unaelea.

Tukumbuke: Mafuriko haya sasa ni threat to national security kama ambavyo tetemeko la ardhi limekuwa huko Kanda ya Ziwa...
 
Ameongelea vitu viwili: Kusikiliza watalaam na political will-watalaam hawasikilizwi na hiki kwa nchi hii si cha ajabu, kwa ujumla hawasikilizwi. Political will hili amelielekeza huko "juu" ikiashiria mamuzi ya pamoja si kawaida hapa-hata mawaziri hawana sauti kwa ujumla. hata baba alipokuwa "Rome" alitenda kama "warumi" na sasa nayeye anafanya yake na wengine wote wanakwenda na muziki huo. Nimemuelewa le profeseri jembe la JK.
 
kwa nini hukusema then lakini unasema now?
hauaminiki bana, tupishe uko!!
 
Pale mwanasiasa anapocheza ngoma ile ile ya wanasiasa. Kwani na vile vijisenti ulihitaji political will ya wana siasa.
 
Bila kutafakari kwa kina maneno ya mama Tiba utamtolea povu tu sababu alikuwa waziri husika, mnasahau kwamba kipindi cha nyuma serikali na maamuzi yake hayakuwa yakifanywa na wenye mamlaka katika vitengo husika bali na wenye pesa.

Niulize tu swali lingine hapo, kilimtokea nin Maghufuli alipowatangazia kurudisha Masaki, Oysterbay na Capripoint serikalini?
 
Na makonda anasemaje....mana hajapewa ukuu wa mkoa leo....!!! ni mwaka wa tatu sasa na ameshakuwa billionea
 
Wacheni porojo simvua zinanyesha kiangazi kikija yatakauka, ulaya muda huu kuna barafu mbona hawajaambiwa wahamie africa au latin america? Acheni wakae juu ya mabati na miti yakikauka watarudi wadeki na maisha kusonga.
 

MKuu kwa jinsi bomoa bomoa ya tanesco ilivyofanyika, Naamini labda huyu mama kwenye awamu hii angeweza.
By the way unaikumbuka Ripoti ya Lukuvu ya viwanja vya wazi?
Ripoti ilivyofika mezani Viwanja asilimai 90 vya wazi vinamilikiwa na mtu mmoja(CCM), wakapiga kimyaa!
na Mkoa akahamishwa nakumbuka.


Dar ina maeneo ya wazi 180 yaliyovamiwa’


JIJI la Dar es Salaam lina maeneo ya wazi 180 ambayo yamevamiwa, ambapo 111 yapo Halmashauri ya Kinondoni, 50 yapo Ilala na Temeke yapo 19. Hayo yamebainishwa wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, walipozungumza na waandishi wa habari.
 
Ikishindikana hamia Dodoma achia Dar wenyewe.
Mama ulikuwa na nguvu ndani ya Serikali na Chama chako,ungekuwa mwalimu mzuri kama ungewaelemisha hadi wakakuelewa,yaonekana ulifikiri wanakuelewa kumbe your were reading different pages.

Sasa tumeishachelewa akiamka leo Raisi Magufuli akasema anataka kuibomoa na kuisuka upya bila compesation ndio uchuro mwingine.

Political will itatoka wapi wakati fedha ndio sabuni ya roho kwa wenye nazo?
Tusubiri magonjwa ya kuambukiza kama kipindupindu na malaraia,hata mtenge pesa ngapi za Wizara ya Afya bila kinga ya kuzuia mafuriko na madhara yake ni kazi bure.
 
sijui kilitokea nini, lkn kwa masikio yangu nilimsikia mh raisi wa wakati huo Jakaya Kikwete akikataza kujengwa vile vijumba vya mwendokasi pale jangwani.
 
Kwa hiyo anamsema Kikwete au nani? Maaana yeye alikuwa Waziri, political will kutoka kwa nani zaidi yake?
 
Kama political will ilikosa angejiuzulu uwaziri. Ktk siasa unapokuwa mwanasiasa na ukawa kiongozi pakikosa political will ya kufanyika kinachotakiwa kufanyika kiwe na ukakataliwa unatakiwa u protest kwa kuwajibika kwa kujiuzulu.

Kwa mtalaam ambaye anaona utaalam wake unakuwa disregarded na authority njia ya msomi kuonesha usomi wake ni ku resign hiyo position na si kubuluzwa. Msomi wa kweli hawezi kubuluzwa na mwanasiasa under any possible pretexts.

Ukiona msomi anamlaumu mwanasiasa kumubuluza huyo siyo msomi, bali amepita darasani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…