Mafuriko: Mama Tibaijuka adai hakukuwa na dhamira ya kisiasa kulinusuru bonde Msimbazi wakati yuko Ardhi

Anaandika Mama Prof. Anna Tibaijuka;
Bila nidhamu ya kuheshimu Mipango miji mafuriko yatakuwa common feature ya jiji la DSM. Regrettably.

Tatizo siyo mvua kubwa. Tatizo ni kuziba natural drainage system hivyo maji ya mvua kushindwa kwenda baharini.

Nilipokuwa Ardhi nilijitahidi sana kuokoa bonde la msimbazi kwa mujibu ya 1979 master plan. Call it the Nyerere Master plan.

Sikufanikiwa. There was no political will for it. Bonde likaendelea kujengwa. Kwa hiyo maji hayana njia za kufika baharini.

Mind you Bonde la Msimbazi ndiyo njia pekee kwa maji yote yatokayo Pugu Hills Ukonga Airport Tazara Tabata Kigogo magomeni Ilala kufika Jangwani grounds hadi salender bridge yanapoingia baharini. Pia maji kutoka ubungo Manzese Tandale magomeni Kagera kinondoni hananasif Muhimbili hadi jangwani njia ni hiyo tu moja.

Kwa upande wa chuo kikuu mto mbezi na mto mlalakuwa na mto Mdumbwi ( Kawe) imejengwa na njia za maji kuifikia kuzibwa.

You do not need to be an expert in urban planning to know that WATER FINDS ITS OWN LEVEL. ALSO TO KNOW THAT IN SOME YEARS HEAVY RAINS SHALL BE EXPERIENCED. ALL THESE THINGS ARE PREDICTABLE.

Mfano at Jangwani grounds Tulisema lakini uharaka wa kukamilisha mradi wa DART uka overide any other consideration. Nilisikitika sana knowing it was a recipe for disaster lakini urban planning is a political activity. Without the support of political power, all knowledge and expertise go to waste. They cannot help much.

Nimeona nielezee hili kwa watu wanaotaka kujua kwa nini wataalam wametufikisha hapa. Sio wataalam. Ni interests. Na utamaduni wa kutoheshinu utaalam. Na wananchi kutaja quick solutions.

Going forward lazima kurejea plan ya Mwalimu ya 1979. To salvage the Msimbazi Valley as THE CENTRAL CITY PARK. Waliojenga wawe resettled with compensation kama wanastahili. New developments in this valley ziwe arrested.

Serikali Irejee huku kwa haraka. Najua Mhe Rais Magufuli ni mtu imara sana katika kusimamia sheria na ushauri wa wataalamu hivyo basi hili atalitazama.
 
[
Asante Mama Tibaijuka. You said it all tena kwa lugha ya 'kwetu'. Ningependa kuona watu wakiacha kuwalaumu wataalamu kwa hili. Wote tuna makosa. Wanasiasa wameshindwa kutoa usimamizi unaotakiwa. Watu tumetaka suluhu za haraka na nyepesi! Lakini kubwa watu tumejenga ustaarabu wa kutotii sheria, kanuni na taratibu isipokuwa tu pale zinapooana na matakwa yetu.
 
Haaa ndio mnagundua leo ikiwa kosa n la muda mlefu baada ya kuwafukuza watu jangwan mkawapa wawekezaji wa mwendo kasi nao wakaweka makao yao hapo selikali hii ni yaajabi sana
 
Ukipewa Madaraka Fulani Halafu uka kwamishwa kwenye Utendaji Jukumu lako la Mwisho Ni kujiuzulu

Ukisubiri ufurushwe Kwa Wizi ndio uje useme hayo utaonekana Ni Mnafiki tu!

Mto always huwa unabadili uelekeo Na Kwa waliosoma Geograph Hata level ya Nursey school watakuwa wanajua kitu kinaitwa Meanders kwenye Mito!

Leo Watu w Pembezoni wanaweza kuwa ndani ya hifadhi ya Mto kesho wanaweza wasiwepo!

Leo unaenda kumbomolea Mtu Eti kujenga ndani ya hifadhi ya Mto 60 meter Kumbe Miaka 20 iliyopita wakati anajenga alikuwa 120 meter kutoka kwenye kingo Na Pengine aliejenga kwenye kingo wakati huo Leo hii yupo nje ya hizo kingo Kwa kuwa Maji yamebadilisha uelekeo

Wizara ya Ardhi chini ya Mama Escrow ndio ilikwamisha Mradi wa uboreshaji wa Mto Msimbazi Kwa kujengea River Banks zake mwanzo Mwisho
Duh! Ama kweli tembea uone. Nenda (au hata soma tu) majiji makubwa duniani iliwrmo London, Amsterdam utagundua kuwa yana mito iliyojengewa kuimarisha their natural direction na mito hii ni moja ya mjia za usafiri(ikiwemo utalii). Mimi ninashangaa aliyeruhusu kujenga jengo la mwendo kasi pale jangwani!
 
Raisi wetu wa sasa amewahi kuwa Waziri wa ardhi kwa kipindi kifupi, naamini anajua ulichoeleza kwenye ujumbe wako huu.
Kwa kweli kama ulivyoeleza kumaliza tatizo hili si suala la mchezo linahitaji dhamira ya kweli ya kisiasa. Linatakiwa lifanyiwe kazi kama janga. Kumaliza tatizo hili si suala la kupeleka motor graders kuchimba chimba mto msimbazi kwa wiki mbili kuaminisha watu kuwa serikali inalifanyia kazi suala hili. Ni jambo linalohitaji proper planning na financing kama ilivyofanyika kwa miundombinu ya DART
 
Sasa mama kwako kila kitu kilifeli au? political will kutoka kwa nani tena wakati wewe ulikuwa kwenye baraza la mawaziri? vipi na ile project ya kigamboni satellite mliyotuaminisha nayo tena hakukuwa na political will au?
 
Tunaomba sasa Waziri wa Ardhi wa sasa kufuata master plan iliyokuwepo Na hii iwe ni nchi nzima . Tusije tukasikia hizi hadithi tena
 
Hizi ni nondo nzito, ila huyu Mama nae alikuja na mcheche sana na mkwala wa kusimamia, sheria taratibu na kanuni za mipango miji akidhani ataweza!.

Alipoingia tuu, akatia mkwala wa kubomoa wote waliovamia open spaces, akianza na ile open mbele ya Palm Beach.

Nilifanya nae mahojiano, recorded, nikamuuliza, kwa vile CCM ndiye mvamizi mkuu wa viwanja vya wazi, na vigogo ndio wamejimegea mapande manono, jee ataweza?. Alinijibu yeye haangalii sura wala hajali nani ni nani, yeye ni kufuata tuu sheria.

Nilipanga kumtafuta kupata mrejesho, lakini akatumbuliwa kabla!.

P
Brother lini unaelekea Kwa spika
 
Huruma, siasa, upendeleo vinatakiwa vikae kando, mvua ikiisha grader lipite hapo bonde LA msimbazi kuanzia segerea hadi jangwani litoe nyumba zote zilizoingiliwa na maji. Wahusika wapewe viwanja bagamoyo huko
 
Back
Top Bottom