Hivi ni kwanini hao jamaa wanaopima viwanja kila ukiwahitaji- wewe mwananchi ndo inabidi uingie gharama za usafiri?tena hawapandi daladala , wanataka ukodi taxi kama huna gari! Kwani si ndi kazi yao na huko field ndo kama sehemu yao ya kazi? Sasa kwanini tunaotaka kupimiwa viwanja tulipe kuwapeleka 'ofisini' kwao? Hii si sawa na kumkodia taksi polisi kwenda kukukamatia muhalifu?
Halafu kuna kidubwana kimoja wanakiita GPS, ni muhimu kwenye upimaji viwanja lakini cha kushangaza kabla hujawatoa jamaa ofisini kwenda huko field watakuambia wanahitaji hela ya kukodia hicho kifaa! Hivi kuna mtu anajua gharama za kupima kiwanja? Sidhani, manake kila ukitaka ufanyiwe hii shughuli inabidi u bargain, gharama zilizowekwa na serekali kama zipo basi ni siri kubwa sana.
Basi kiwanja nikakipata, tena chenye hati, lakini naenda kufanya 'searching' naambiwa 'rudi baada ya siku nne za kazi uchukue majibu', lakini naona watu wanapewa majibu yao hapohapo, kuulizia wadau pembeni nikaambiwa 'ongea nao vizuri' Na kweli, kutoa buku 10 -baada ya nusu saa majibu tayari! Hiki kingeweza kuwa chanzo cha mapato, waintroduce fee kubwa kwa watu wenye haraka zao kama mimi badala ya kuendelea kuwanufaisha wale wadada pale madirishani.