Mafisadi watangaza vita dhidi ya watanzania..kama haupo nasi, tutakumaliza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi watangaza vita dhidi ya watanzania..kama haupo nasi, tutakumaliza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Sep 2, 2008.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mwanasiasa mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru(Pichani),amesema Chama Cha Mapinduzi(CCM), kitahakikisha kinawashughulikia wapinzani na kuhakikisha wanaumaliza kabisa upinzani. Kingunge ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM,aliyasema hayo mjini hapa wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pancras Ndejembi.
  Kingunge alisema nguvu ya chama kwa sasa inaelekezwa kwa wapinzani lengo kuu likiwa ni kuwamaliza licha ya kuwa tayari chama chake kimeshafanikiwa.“Sasa hivi hakuna kitu na tumefanikiwa kwa sababu ya kuwaunganisha wanachama wetu na kuwa kitu kimoja na haki ndiyo inayowaunganisha na ndio maana tumefanikiwa,”alisema mkongwe huyo. Alisema iwapo kiongozi wa CCM atashindwa kupambana na upinzani,ni lazima uongozi wake utakuwa na dosari na hivyo atanyang’anywa madaraka

  Duh, kama kiongozi mkuu wa CCM ndiye huyo huyo mkuu wa serikali, je watanzania wenzangu hao wapinzani ambao ni watanzania wenzetu nani atawalinda ? Hili ni jambo la hatari na linapaswa lilaaniwe na kukemewa kwa nguvu zote. Je wabunge wetu, hili mnalikubali ? Je tunatawaliwa kwa kufuata katiba ama maazimio ya CCMafisadi ? Maisha ya watanzania wasio na hatia yamo hatarini na dola limetupa mgongo, je tubadilishe uwanja wa mapambano ?
   
 2. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kaazi kweli kweli! Namuonea Muungwana huruma kweli ikulu sio pa kukimbilia
   
Loading...