Mafisadi wa Tanzania wazuiwa kuingia Marekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi wa Tanzania wazuiwa kuingia Marekani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 8, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,413
  Likes Received: 81,454
  Trophy Points: 280
  Fisadi Mkapa naye apigwe marufuku kuingia Marekani na nchi zote za magharibi

  Date::9/8/2008
  Mafisadi wa Tanzania wazuiwa kuingia Marekani
  Na Kizitto Noya
  Mwananchi

  SAKATA la ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na mchakato wa utoaji zabuni kwa kapuni ya kufua umeme wa dharura likiwa halitoa majibu yanayokidhi kiu ya umma, serikali ya Marekani imetangaza kufungia mlango watuhumiwa wa ufisadi unaogusa maslahi yake kuingia nchini humo kwa matembezi kuwekeza au kutumia mali walizochota.

  Nchi hiyo pia imetangaza kuwafukuza maafisa wa serikali wanaotuhumiwa kwa ufisadi na ambao tayari wamewekeza nchini humo au kusafiri kwa ajili ya matumizi ya mali walizopata kinyume cha taratibu.

  Marekani imekuwa ikionekana kama kiota cha mafisadi ambao hujichotea mamilioni ya fedha kwenye serikali za nchi changa na kutowekea kwenye taifa hilo kwa lengo la kuwekeza, kutembea au kuanza maisha mapya.

  Lakini jana, balozi wa Marekani nchini, Mark Green alisema katika taarifa yake kuwa watuhumiwa wa ufisadi, waomba na wapokea rushwa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao wanaofaidika na ufisadi huo, hawataruhusiwa kuingia nchini humo.

  "Tangazo hili linawazuia watu hasa maafisa wa serikali wanaojihusisha na ufisadi wa mali ya umma kuingia Marekani na kufurahia matunda ya ufisadi wao na huu ni ujumbe kwamba Marekani imedhamiria kuungana na nguvu za kimataifa kupambana na ufisadi kokote duniani," alisema Green.

  Alisema uamuzi huo ni tangazo jipya namba PP7750 la rais wa nchi hiyo, George W. Bush na linawahusu maafisa wa umma na viongozi wa serikali wenye tabia ya kuomba na kupokea rushwa au kutumia madaraka yao vibaya kwa faida binafsi.

  "Hili ni tangazo la rais wa Marekani na linawahusu maafisa wa umma na serikali wenye tabia ya kupokea rushwa ya fedha au mali na wanaotumia vibaya madaraka yao. Pia linawahusu maafisa wa serikali wenye tabia ya kufuja fedha za umma, kuingilia uhuru wa mahakama, uchaguzi na shughuli nyingine za umma," alisema.

  Kwa mujibu wa Balozi Green, marufuku hiyo ya kuingia Marekani pia inawahusu wachumba, watoto na wategemezi wa wafanyakazi wa sekta binafsi wenye tabia ya kuwahonga watendaji wa serikali na maafisa wa umma ili wafanye mambo kwa maslahi yao badala ya umma wanaoutumikia.

  Green alisema Marekani haitakubali kuwa kiota salama cha mafisadi na walarushwa na mpango huo mpya wa kuwazuia mafisadi kuingia nchini humo, umelenga kuieleza dunia kwamba Marekani iko makini katika suala hilo.

  "Uwazi na vita dhidi ya ufisadi ni tunu za Marekani. Tunaendelea kufanya kazi kwa karibu na Tanzania ili kung'oa mizizi ya ufisadi na kumpeleka mbele ya sheria mtu yoyote anayetuhumiwa na kubainika kushiriki matendo ya kifisadi," alisema Green katika taarifa yake.

  Alisema mpango huo unawalenga watumishi walioshiriki ufisadi nchini mwao na kuathiri maslahi ya Marekani ambayo ni pamoja na shughuli za biashara za kimataifa na uchumi za nchi hiyo.

  Green alitaja maslahi mengine ya Marekani yanayopaswa kulindwa kuwa ni malengo ya misaada yake kwa nchi husika, usalama wa nchi hiyo, ujenzi wa demokrasia na mambo yanayokiuka sheria mpya ya rushwa inayofanyika katika matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

  Mpango huo wa Marekani umeanza kuwa maarufu duniani baada ya kuanza kutekelezwa na karibu nchi zote zilizoendelea (G8) kama sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya nchi hizo yaliyofikiwa mwaka 2003.

  Katika Mkutano huo wa Juni 2003, Rais George Bush wa Marekani na viongozi wengine wa nchi hizo walikubaliana kutoruhusu nchi zao kuwa kimbilio la Mafisadi kutoka nchi zinazoendelea.

  Marekani na wenzake pia wamekubaliana kushirikiana na nchi zinazoendelea kuwatambua, kuwatafuta, kufuatilia mali za mafisadi na kuzikamata kisha kuzirudisha kwa wahusika na kuwafungulia mashtaka.

  Hivi karibuni viongozi hao katika mkutano mwingine uliofanyika Hokkaido, walikubaliana kuendeleza ushirikiano huo unaoongozwa na Umoja wa Nchi za Amerika (OAS) na Jukwaa la Kiuchumi la Asia Pacific Cooperation (APEC)

  Uamuzi wa Marekani kuwazuia mafisadi kuingia nchini humo umekuja wakati Tanzania ikiwa inakabiliwa na changamoto kubwa ya baadhi ya maafisa wa serikali yake kushiriki ufisadi.

  Baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele kwamba maafisa wa serikali wanashiriki ufisadi ni kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA), ununuzi wa rada, mkataba wa kufua umeme wa dharura wa Richmond na mikataba mibovu ya madini.

  Baadhi ya tuhuma hizo za ufisadi zilisababisha rais Jakaya Kikwete kuvunja baraza lake la mawaziri kutokana na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kujiuzulu baada ya kuhusishwa katika kashfa ya Richmond.

  Rais pia alimvua madaraka aliyekuwa gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Marehemu Dk Daud Ballali kutokana na tuhuma za ufisadi uliofanywa kwenye akaunti ya madeni ya nje ya Benki hiyo (EPA).

  Ballali alivuliwa wadhifa wake na kukutwa na umauti akiwa Marekani alikokuwa ameenda kutibiwa muda mfupi baada ya kampuni ya Ernst&Young kumhusisha na ufisadi wa (BoT)

  Mbali na kumvua madaraka Gavana Ballali, Rais pia ameagiza kufungwa kwa akaunti hiyo na maafisa wa benki hiyo waliohusika na ufisadi kuachishwa kazi kisha makampuni yote yaliyochota fedha hizo kufilisiwa na fedha kurejeshwa Hazina.

  Pia katika kupambana na ufisadi huo, kitengo cha kushughulikia makosa makubwa ya jinai cha Uingereza (SFO), kiliendesha uchunguzi na kubaini akiba ya dola 1milioni kwenye akaunti ya aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali, Andrew Chenge ambazo walifanyia utafiti kama zinahusika na ufisadi uliofanywa kwenye ununuzi wa rada.

  Kitengo hicho kilimhoji Chenge kwa kumiliki akaunti hiyo na kumwachia bila kutoa taarifa ya uchunguzi wake.
   
 2. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  marehemu balali alifia huko kwao, watuletee kwanza ripoti kamili ya utata wa kifo chake, ili tuwaamini
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Hawa nao unafiki utawaua, mtandao wakubwa hawa hawana lolote wanafiki na waongo, unakumbuka waliyosema kuhusu Balali? Tutawaaamini saa hizi kuwa wanasema ukweli?

  toka yule balozi wao aliyeko Boston aje bongo, katengenza michuzi wee na kina Mkapa na Sumaye, basi wamekuwa ni mtandao tu! ndio maana Mkapa, Sumaye na muungwana hawaishi Boston, kila siku kutupiga kamba, eti wame-revoke viza ya Balali, huku mtu ana Permanent Residence, waende zao!
   
 4. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2008
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sisi ni wadanganyika mzee!!!!!!!!!

  Hata tukiambiwa ukweli tunakasirika.
  Tukidanganywa tunafurahi na kujivunia!!!!!!
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  I will believe it when I see it. Siku nikiona Mwungwana ananyimwa visa ndipo nitajua kuwa jamaa ni serious.
   
 6. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Huu ubalozi wa USA hawana lolote, wanatudanganya tu. Soma tena huo ubalozi ulisemaje kuhusu fisadi Ballali?

  Si ndio hao hao waliosema wamemfutia visa Ballali? Kisha wakasema Ballali hana uraia wala green card. Ulikuwa ni uwongo mkubwa.

  Si ajabu hata leo wanajua Ballali alikojificha.
   
 7. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  Wanajua aliko.

  Marekani na UK wanamtindo wao wa kupata fedha wakiona umeiba mabilioni ya fedha na umeyaficha kwao ,kitu wanachofanya ni kunyima VIZA na jamii yako yote kama aliwalivyosema hapo ili asiwepo next KIN.
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Sep 8, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Yaani maadam wanataka maslahi kwenye nchi ndogo watasema lolote waonekane wamo! Wakati tunailaumu serikali ya Tz kuhusu ufisadi leo , Ubalozi unataka kutuaminisha kuwa wao wanapigana na ufisadi wakati wamo humuhumu. Ningewaona wa maana wangesema wanafunga ubalozi wake mpaka mafisadi watakapochukuliwa hatua za kuridhisha!

  Waberoya
   
 9. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2008
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tusilaumu balozi za kina USA na UK hawa jamaa wanatuelewa watanzania ni watu wa kudanganywa siku zote si viogozi wala raia wa kwaida kubainisha hilo wangalie viongozi weu wanapokutana na viongozi wa nchi kubwa wanakuwa dhaifu kabisa pili ukiangalia upande wetu wananchi wengi akili hazifanyi kazi hazina upeo amini leo hii kuna watu bado wanamini Mwalimu yupo hai na wanahoji kwanini hajafika kuwatembelea ,kunawengine wanafika viwanja vya ndege kwa imani watafirishwa kwamiujiza hayo yote ni shahidi tosha tumekuwa na majigambo mengi lazimatubadili hali hii
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Hatuwezi kubadili hii hali hivi karibuni wakati kuna wenzetu wanaamini leo mwaka 2008 kwamba Nchimbi ni almost a God!

  Ndio maana tutaendelea kuchezewa na hawa wazungu, misafari kila siku isiyoisha, cha kuonyesha hakuna, watu wetu wanakwenda Europe kila siku na US,

  Wallahi tukisimamisha safari za nje kwa maofisa wetu bongo japo kwa one year tu, tunaweza kuongeza mishahara ya wananchi kufikia kiwango kinachotakiwa, lakini tumezidiwa na uzembe wa akili, hatuwezi kuona mbele maana viongozi wetu ndio hawa kina Makamba, katibu mkuu wa Chama kinachotawala taifa anamuogopa Lowassa, mbunge tu wa kawaida, hawa hata Mungu siku hizi wamemsahau kabisa ni ufisadi tu sasa wazungu watufanyie nini cha maana, na wao wanatufisadi tu!
   
 11. Nikifufukammekwisha

  Nikifufukammekwisha JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tumesikia kelele/tetesi nyingi mno kua ndugu Muungwana kafika hapo alipo baada ya kupigwa tafu na hao mafisadi. Ndugu yetu balozi Green leo anatueleza kwamba watu wanao/walio faidika na ufisadi nao watapigwa stop kuingia US........... Ukiuchukulia usemi huu kama ulivyoelezwa na balozi wa US unaweza ku-conclude kwamba ile safari ya Muungwana ya wiki mbili zilizopita kwenda US ndio ilikua ni ya mwisho kwake kuingia US, and probably katika nchi zote za G-8....

  Mhh, let's wait and see!!!!
   
 12. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Hmmm...hii order mbona ilikuwa issue miaka minne iliyopita.....kweli jambo usilolijua ni sawa na.....................

  President Bush’s "No Safe Haven" Policy


  On January 12, 2004, President Bush issued Presidential Proclamation 7750 (PP7750) to suspend entry into the United States for individuals involved in public corruption that has a serious adverse effect on specified U.S. interests.

  PP 7750 was issued, in part, under Section 212(f) of the Immigration and Nationality Act of 1952 (INA), which allows the President by proclamation to "suspend the entry of all aliens or any class of aliens as immigrants or nonimmigrants" into the United States whenever such entry "would be detrimental to the interests of the United States."

  PP 7750 provides specific legal authority for the Secretary of State to identify persons who should be denied entry because they are involved in public corruption that has serious adverse effects on the national interests of the United States, including: (1) the international economic activity of U.S. businesses, (2) U.S. foreign assistance goals, (3) the security of the United States against transnational crime and terrorism, and (4) the stability of democratic nations and institutions.

  PP7750 prevents such people from coming to the United States to enjoy the fruits of their corruption, and sends a strong message that the United States is committed to supporting international efforts to combatting public corruption wherever it occurs. Implementation of PP7750 has sent shock waves that have reveberated across the world that signal that the United States is committed to cracking down on corrupt officials.

  Source
   
 13. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ....Huyu mwandishi inaonekana ameshinikizwa kuandika kinamna hiyo ili ku-cover ziara ya Mh. Rais hivi karibuni nchini Marekani.

  ....Kama ameandika kwa hiari na ni mwandishi mzoefu, kwa maoni yangu hafai kulipwa hata kidogo kwa hii article. Habari yote ni marudiorudio tu. Kwa sababu zisizoeleweka, habari ya azimio la Marekani kuzuia mafisadi kuingia nchini humo kaiandika as if ni habari mpya. Kama nilivyosema, iwapo hajashinikizwa basi huyu mwandishi ameamua kupotosha wasomaji.
   
 14. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  MWANANCHI wameiandika kama ilivyo kwenye tovuti ya ubalozi wa US, kwamba ni ubalozi umesema ni habari mpya. Tangazo PP5570 la Rais wa US lilitolewa mwaka 2004, lakini Balozi Green hajaeleza kwa nini anasema hii ni habari mpya. Kwa hiyo kosa nadhani ni la ubalozi zaidi.

  Hata hivyo,kitu ambacho MWANANCHI wamekosea - lakini ambacho sitegemei kabisa kigazeti kama MWANANCHI kingepatia, na kwa hiyo hata siwalaumu - ni kutokutuambia kama walifuatilia ubalozini kuelewa kama ubalozi ulikuwa una respond kwenye matukio yoyote mpaka wakatoa tamko hilo. Yani, ni nini kime chochea hii development.

  Huwa nawacheka crummy press ya Tanzania kwa kushindwa kumuuliza mwenzao Waziri Membe maswali anapokuwa anatoa matamko ya ajabu ajabu, lakini nitakuwa nawaonea mno kwa kushindwa kumswalisha mwanadiplomasia wa Kimarekani. Hawamuwezi. Na yeye balozi Green anajua yuko Tanzania, kwenye mazingira ya third rate press, ndio maana anaweza kutoa vitamko vya ovyo ovyo.
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Sep 9, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  We Pimbi vipi "investigation" yako kuhusu dokta Masau?
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hii bongo inawezekana kweli, nchi ambayo kila siku unaweza kujiita jina jipya na wala isiwe tatizo. Unaweza kuwa na passport hata tano zenye majina tofauti tofauti na wala hao immigration pamoja na kudai kwamba wana new tech wasigundue. Unaweza kufoji whateva document kiasi kwamba hata mtoa document halali akiletewa the forged one na ile halali akashindwa kutofautisha. Sasa je fisadi say Njake akiamua kujiita Abdallah Mhagama, na pasipoti yake safiiii yenye jina hilo huku akiwa na panki iliyotengenezwa maridadi hao wamarekani watajuaje??????????
   
 17. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Duh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 18. W

  WildCard JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hivi Marekani pamoja na "UNUSAJI" wao wa nguvu wanaweza wakawa hawajui "WALIOMUWEZESHA" Rais wetu ni akina nani kwenye kampeni za kuwania Urais?
  Hawajui mapesa ya EPA yalifanya kazi gani kwenye uchaguzi uliopita?
  Wamarekani ni wakali pale tu MASLAHI yao yanapotibuliwa basi!
   
 19. C

  Chuma JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nyani naona hajaacha matusi...!!! Kama wewe umekubali kuitwa Nyani, usiwaite wengine Pimbi!!!
   
 20. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hawa Viongozi wa Marekani watuendolee UTOPIAN HAPA. Wanafiki wakubwa hawa, hizi ni mbinu tu. Mbona wanajifanya kuipenda Tanzani kwa mialiko ya kila namna ili tu kuweza kufanikisha dili zao. Kwa taarifa yako Marekani haina interest na nchi yoyote duniani kama haina kitu. Ilishajua Tz Barrick ipo ambayo Baba wa Bush in one of the Directors, Wanataka kuja kuchimba mafuta na gas, kuna kujenga Presidential Lodge, you name them all. Sasa mbona wasiende Sudan, Durfur na kwingineko kusikokuwa na Resources. Halafu JK anawakenulia meno.

  Jameni mlioko huko Marekani tupostieni taarifa za mafisadi kusafiri kama kweli watakuwa banned. Danganya toto hiyo,
   
Loading...