Mafisadi muelewe kuwa Malipo ya uovu ni hapahapa Duniani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi muelewe kuwa Malipo ya uovu ni hapahapa Duniani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Jul 14, 2011.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu mafisadi ni wakati wa kujeukia Mungu kwani uovu wenu umekidhiri na umemfikia Mungu mwenyewe na malipo ya uovu wenu ni hapa hapa Duniani angalia mnafedha nyingi wala hamna amani nyie na familia zenu sisi wenzetu tunashindia mihogo lakini tunaamani hatujamdhulumu mtu. Huwezi kuamini jinsi mlivyowachafua wenzenu wakati mnautafuta urais mpaka Mzee wa Kuheshimika Salim A Salim mkamhusisha na vifo ambaovyo hakutenda mmefika wapi sasa je mlidhani hili ni sawa, tazama Mh Balali amezikwa kama nguruwe tena ughaibuni na kukimbia nchi pamoja na mapesa yake yote hayo. Ndugu zangu nataka nawambie kitu kimoja Money is not everything. Si nia yangu kuwahukumu lakini nataka kuwakumbusha heshima ya mtu haitokani na vitu alivyonavyo bali jinsi gani anavyowajali wengine na kuwaona wengine ni wa thamani kama yeye. Maisha yetu ya kuishi hapa ulimwenguni ni miaka 70 ukiwa na nguvu ni 80 ni vizuri kujiangalia sana tunavyoenenda wizi wa mali ya umma ni wizi kwa wanyonge wa nchi hii, kwanza tunahitaji chumba kimoja cha kulala na kitanda kimoja yanini kujiangaisha na mali za wizi ambazo hata ukiwarisisha watoto wako hawataishi kwa amani.

  Ndugu zangu naomba tuelewane sio dhambi mtu kuwa tajiri ilimradi utajiri wako unaelezeka na kuupata kihalali huo unakuwa baraka na mwisho wako utakuwa mzuri tuu. Watanzania wenzangu hebu tubadilike hasa wale tuliopata nafasi katika uongozi wa umma na wale ambao mpo kwenye private sector ambao mnaishi kwa biashara za kiujanja ujanja kwa kutumia rushwa kuwarubuni wale waliokatika uongozi wa umma tuwache haitatusidia hebu tuongeze uzalendo kwa nchi yetu.

  Nasiisi wananchi wa kawaida tusikubali kuendelea kufanywa mabwege kiasi hicho cha kuwaweka madarakani watu wenye maslai binafsi wao na watoto wao mpaka wanafikia hatua ya kutukejeli wanavyotaka wakijua sisi siku zote ni mabwege tuamke sasa.
   
Loading...