Hivi ni sahihi mtu kuharibu nyumba yake kwa makusudi na kisha kuhamia nyumba ya jirani. Mimi ni mwana ccm tena ukimichanja damu yangu ni ya ccm. lakini nasema hivi wanao dhani ccm ni mbovu wao ndo wabovu na wahame wote watuachie chama chetu tubaki wapenzi na watu tulio jazwa na misingi na sera nzuri za chama cha mapinduzi tuendelee kukiboresha. Kishinde kisishinde sisi hatung`oki. Watatukuta wakiharibu huko waliko kimbilia, najua watarudi tena baada ya sisi kukisafisha.