Mafisadi kuhamia CHADEMA?

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2008
Posts
4,773
Reaction score
2,383
Lisemwalo lipo, kama halipo laja.

Kuna tetesi kuwa baadhi ya mafisadi wana uhusiano wa karibu na uongozi wa juu wa CHADEMA.

Nukuu ya gazeti la Raia Mwema la leo linaeleza kwa undani jinsi vikao vya mafisadi vitakavyofanyika huko Arusha Pasaka hii.
Arusha ndiko wanatoka Dr Slaa na E Lowassa, sijui kama kuna uhusiano hapo!

Nape Nnauye alitonesha suala hili la uhusiano kwa mbali kati ya genge la mafisadi na CHADEMA, wakati akituhumu kuwa kuna magezeti, chama fulani na viongozi fulani wa dini wameanza kutumiwa(taarifa za kiintelijesia?).

Jamani pesa hiyo inatembea.

Ikija thibitika CHADEMA will have lost all credibility.

============

Umechanganya kiswahili na kingereza.Kingereza ulichotumia hakifai kutumiwa kwenye mtandao ambao unaaminika ya kuwa unatumiwa na watu makini.
 
Arusha ndiko wanatoka Dr Slaa na E Lowassa, sijui kama kuna uhusiano hapo!

Nape Nnauye alitonesha suala hili la uhusiano kwa mbali kati ya genge la mafisadi na CDM.

Jamani pesa hiyo inatembea.
CDM hamna siasa za undugu (Lowassa asingetajwa na Dr Slaa katika list of shame)

Pesa inaweza nunua kila mtu CCM ila sio CHADEMA.

vikao ARUSHA???? vya EPA, RICHMOND, DOWANS, MERIMETA vilifanyika magogoni viwanja vya tausi kwa hiyo usishangae hili (eboo DAR jirani yake msoga BGMY)
 
umekalia upupu muwasho tu unakusumbua. Unaona Silaa(Dkt wa Ukweli) ni wa kukaa na fisadi meza Moja?
 
umekalia upupu muwasho tu unakusumbua. Unaona Silaa(Dkt wa Ukweli) ni wa kukaa na fisadi meza Moja?
na ikiwa wakipigiana simu itakuwa Dr SLAA anampa EL,RA,AC mbinu ya kulizamisha lichama la magamba ile design ya tukose wote kwani haiwezekani watatu tu waondolewe halafu ccm ijidai ni chama safi.
 
na ikiwa wakipigiana simu itakuwa Dr SLAA anampa EL,RA,AC mbinu ya kulizamisha lichama la magamba ile design ya tukose wote kwani haiwezekani watatu tu waondolewe halafu ccm ijidai ni chama safi.

Ndio maana orodha ya mafisadi imeongezeka!
 
Umechanganya kiswahili na kingereza.Kingereza ulichotumia hakifai kutumiwa kwenye mtandao ambao unaaminika ya kuwa unatumiwa na watu makini.

Jaribu kuchangia hoja na c kujifanya mwl wa kiingereza..ok!
 
wewe uliyeanzisha hii mada inaonekana jinsi gani hauna umakini,fanya utafiti kabla ya kuongea au uvccm?
 
Sioni shida hao mafisadi kuhamia CHADEMA. Ila wakubali kutubu na kuacha ufisadi ndo wahamie huko!
 
wewe uliyeanzisha hii mada inaonekana jinsi gani hauna umakini,fanya utafiti kabla ya kuongea au uvccm?
Mkuu umakini gani zaidi ya kusoma?
Tena gazeti linaloheshimika la Raia Mwema, lisome and also read between the lines, kama una upeo wa kuelewa utaelewa tu.
 
Mkuu umakini gani zaidi ya kusoma?
Tena gazeti linaloheshimika la Raia Mwema, lisome and also read between the lines, kama una upeo wa kuelewa utaelewa tu.
wewe huoni ccm walitaka kutuchezea mchezo wa maigizo kwa kuwaondoa mapacha huku wengine wengi wakisalia?ufisadi serikalini mbona JK asiwaondoe wahusika???
ccm wangetembea kifua mbele kwa kuwaondoa mapacha na wangewadanganya watu kwamba na wao ni safi kama cdm
Alichofanya slaa ni kuzidisha ugumu wa mambo ndani ya ccm
Ili cdm izidi kukua lazima mafisadi wabakie ndani ya ccm
Dont u appreciate mchango wa MAKAMBA baba kwa kuikuza CDM kwa pumba zake??? MAFISADI SHOULD RETAIN THEIR SEATS NDANI YA CCM
 
sijui kitawaleta nn ?watakuja na dhamira gan ?nadhani ni fikra fupi zisizonamashiko hasa ukiangalia ktk uhalisia wake,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…