Mafiga matatu yaepukwe kama ukoma, yanadumaza maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafiga matatu yaepukwe kama ukoma, yanadumaza maendeleo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIDUNDULIMA, Oct 18, 2010.

 1. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 776
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu kauli mbiu ya mafiga matatu ya CCM iepukwe kama ukoma maana inadumana maendeleo ya nchi, wilaya na kata.

  Miaka mitano iliyopita tumeshuhudia mafinga matatu jinsi yalivyopitisha mambo nyeti ya nchi kibabe ukianzia na hitimisho la EPA, Richmond, ETC. Hivi sasa tung'ang'ania kauli mbiu ya figa mojamoja maana kwenyer bunge na halimashauri.

  Hakutakuwa na siri tena, mambo yote yatakuwa hadharani na wananchi watajua nini kinaendelea kuhusu mstakabali wa maendeleo ya maisha yao, halmashauri na nchi yao.
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Mafiga matatu, ni kauli imtokayo zuzu, huku akizani anaowaambia ni mazuzu wenzake. Hakuna kitu cha namna hiyo mwaka huu.

  Na katika hili sisi tunawasidia CCM ili, matapeli wote wawe na uwoga kwenda kugombea CCM, wakizani kwamba wakishatumia rushwa kushinda kura za maoni basi wamemaliza kazi, Hapana tunataka waelewe waziwazi kabisa wakichaguwana kwa rushwa huko CCM kwao, basi kuna hukumu ya wananchi wote inawasubili. Huko ndiko tunakoelekea.:nono:
   
 3. KYAMTUNDU

  KYAMTUNDU JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2013
  Joined: Mar 7, 2013
  Messages: 1,821
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa miaka mingi na hasa hasa mwaka 2010, makada wa Chama cha Mapinduzi (CcM), walibuni na kuendeleza falsafa ya kuwashawishi wapiga kura wa Tanzania kuchagua diwani, mbunge na Rais aliyegombea kwa bandera ya CcM…Utekelezaji wa Falsafa hii ulibandikwa jina la "mafiga matatu" ikilenga kuishikamanisha na hali halisi ya teknolojia ya jamii nyingi ambazo upishi wa chakula (kwa mujibu wa CcM) hutegemea mafiga matatu ili chungu kiweze kuwa katika hali linganifu (balanced).

  Kwa mujibu wa CcM, kuiva kwa chakula ni sawa na kupata maendeleo kwa kuichagua CcM..! Pasipo kuchagua mafiga matatu ni kuyadidimiza maendeleo..Kwa maana hii, maeneo yote walikochagua mafiga matatu BASI maendeleo yanazidi kule walikoasi dhana hii…!Kwanza, CcM na makada wake wanaendelea kuonesha uchache wa ubunifu kwa kudhani kwamba ili ule ni LAZIMA upike! Na kwamba pasipo kupika,hauli.

  Nijuavyo mimi; SI kila kiliwacho kwamba lazima kipikwe…vipo vyakula vyingi vinavyoliwa vikiwemo matunda kama ndizi mbivu, chungwa, papai, nanasi, embe, ambavyo kuliwa kwake hakupitii utegemezi wa mafiga (achilia kuwa matatu au moja)…Kuna kuchoma mhindi, mhogo, kiazi, gimbi, samaki, nyama, pia kuna kuhoka, kuvumbika, nk. Huko kote hakuna haja ya kuwepo mafiga (achilia mbali matatu)
  Lakini katika hali ya kawaida, nimeshuhudia kwamba wanazi wa falsafa kama si mbumbumbu basi watakuwa na uchache wa kutathimini athari ya kule mafiga matatu yalikofanikiwa kuwekwa na wapiga kura walioweza kukumbwa na utamu wa maneno ya makada wa CcM. Nitatoa mifano michache kuonesha namna hali ilivyo kinyume.

  Mwaka 2005 na 2010, Bukoba Vijijini walichagua asilimia 99 ya madiwani wa CcM, mbunge ni kutoka CcM, na Rais aliyetangazwa ni kutoka CcM. Leo hii shule za kata nyingi katika maeneo hayo ziko hoi bin taabani katika matokeo ya kidato cha nne 2012. Maeneo mengi hayana vituo vya afya,achilia mbali zahanati, hakuna nishati ya umeme, kwenye maeneo mengi barabara ni mbovu tena za vumbi tangia mkoloni, kilimo kiko hoi nk.

  Niseme kwa tarafa Bugabo yenye kata tano (Rubafu, Kishanje, Kaagya, Buhendangabo, na Nyakato ) zote zina madiwani toka CcM, srikali za vijiji nyingi ziko chini ya CcM lakini ni tarafa ambayo haina cha kujivunia kutokana na mafiga manne (achilia mbali matatu). Kwa miaka takribani 25, barabara inayoelekea Bugabo kutokea Bukoba Mjini; imejengwa lami kwa kilometa zisizozidi tano kutoka Machinjioni ya zamani hadi Nshambya-msikitini.

  Kwa miaka hiyohiyo, umeme umevutwa kwa mita zisizozidi mia mbili kutoka kituo cha masista wa Kanisa Katoloki ( Nyaigando) hadi Kibengwe.
  Shughuli za uvuvi zimedumaa, bei ya mazao iko chini, kilimo na ufugaji vimeporomoka, magonjwa ya wanyama na mazoa yameshamiri LAKINI koote walichagua mafiga matatu! Linganisha pia mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga, Dodoma,Singida, Tabora na utuambie wananchii wana hali gani?

  Sasa nataka kujua, tatizo ni uduni wa fikra za waliobuni falsafa hii?

  Je, tatizo ni waliochaguliwa hawawezi kuiwezesha falsafa hii (madiwani, mbunge na Rais)?

  Je, ni dalili kwamba CcM inabuni vitu ambavyo haijavitafiti na hivyo imeishiwa akili?
   
 4. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2013
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Mafiga 3 ndiyo mpango mzima. Kinachoifanya Arusha kurudi nyuma ni uwepo wa mbunge wa Chadema. Kama wangelichagua wa CCM, Arusha ingekuwa juu sana leo.
   
 5. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2013
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Radhia, we wasema!
   
 6. Azizi Mussa

  Azizi Mussa Verified User

  #6
  Jun 12, 2013
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 7,601
  Likes Received: 2,241
  Trophy Points: 280
  Dear miss Radhia Sweety ;wewe unaposema sasa Arusha iko chini unakusudia nini? Ili uweze kupima ;Lazma ufanye "Comparative Analysis".
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2013
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 44,523
  Likes Received: 25,351
  Trophy Points: 280
  Mleta uzi ameandika kwa Mifano ya kueleweka , sasa kama unakanusha basi ingekuwa vema kama ungetuletea kautafiti hata ka kata moja tu ya mfano wa mafanikio ya 'UJINGA ' wa mafiga matatu .
   
 8. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2013
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hii sio falsafa ni porojo
   
 9. KYAMTUNDU

  KYAMTUNDU JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2013
  Joined: Mar 7, 2013
  Messages: 1,821
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mifano niliyokupa inaongozwa na CcM...Waweza kunambia kwa nini watu wa huko wana hali ngumu?!
  Au unamaanisha waliochaguliwa wako CcM ila mioyo yao iko upinzani?!
  Kama sivyo kwa nini hali iko ilivyo?
  Kama ndivyo,Rais wa nchi ni CcM au upinzani?
  Mwisho toa jibu kuhusu hiyo mikoa mingine tajwa!
  Usikimbie hoja kwa maneno ya njaa njaa!
   
 10. KYAMTUNDU

  KYAMTUNDU JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2013
  Joined: Mar 7, 2013
  Messages: 1,821
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sina uhakika kama aliwahi kulisikia hilo neno "comperative analysis" ndugu Betlehem
   
 11. Msulibasi

  Msulibasi JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2015
  Joined: Dec 2, 2014
  Messages: 4,492
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hii kauli toka mwaka 2000 tumeaminishwa kuwa tukichagua diwani na mbunge kutoka chama kimoja mambo yataenda kwa kasi kuliko ukichanganya impurities. Hebu tufanye tathmini kwa pale tulipo na kwa kulinganisha maeneo mengine wapi panaenda kasi kati ya mafiga matatu na maeneo yenye mchanganyiko tukianza mitaani, tukija bungeni hadi serekali kuu.
   
 12. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2015
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,758
  Likes Received: 6,064
  Trophy Points: 280
  Tuache ujinga watanzania, MAFIGA MATATU kutoka magamba ni maangamizi ya taifa; tusiwape nafasi wahuni hawa kuendelea kuliharibu taifa hili. Chagua UKAWA kuondokana na dhana ya kishenzi ya mafiga matatu kwani ndani ya UKAWA ni mchanganyiko wa vyama vinne. Mafiga matatu ni ujinga uliopitiliza; nahau za Pwani zisizo na maana yoyote zaidi ya kuwaza ndani ya zipu.
   
 13. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2015
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Hivi yale ya kukanyagia kwenye choo cha shimo nayo ni mafiga au? Nauliza tu mie mgeni huku bara.
   
 14. k

  kingukitano JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2015
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,971
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tips mfano hai mahali ambapo hakuna mafika matati maendelea kadha wa kdha yametokea vinginevyo kakojoe ulale
   
 15. Msulibasi

  Msulibasi JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2015
  Joined: Dec 2, 2014
  Messages: 4,492
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama hii kauli ni feki mbona sisikiagi mtu yeyote akkiihoji au kuichallenge kiasi kwamba ni mwiba kwelikweli kwa wapinzani utasikia kwenye kampeni mafiga mangapiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii----hata wapinzani wanaitikia kwa faida ya tune----------matatuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu. utasikia basi msifanye makosa kuchanganya visvochanganyika CCM hoyeeeeeeeeee.UKAWA hoi. Hebu jipangeni na hii kauli maana inatoa madiwani wengi wasio na sifa
   
Loading...