Mafia: Ndege ndogo iliyokuwa inaelekea Dar es Salaam yapata ajali, watano Wajeruhiwa

Coolhigh

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
976
1,000
Wakuu, habarini za leo. Nimeona clip ya video inatembea mitandaoni ikionyesha ndege ndogo ikiwa inaungua na sauti za watu, na king'ora cha gari la uokoaji. Sauti ni za kiswahili na mtu ametaja Mafia. Kama kuna mwenye taarifa hapa JF na atujuze kilichojiri. Tuwaombee wahanga wote.

=====
Capture.PNG

Taarifa zinaeleza kuwa watu watano wamejeruhiwa na wengine watatu hawajulikani walipo, baada ya dege Ndogo ya Shirika la Tropical waliyokuwa wakisafiri kutoka Kisiwa cha Mafia kwenda jijini Dar es Salaam, kuanguka na kuwaka moto, uwanja wa Ndege wa Mafia.

cheusimangala_

Senior Member
Dec 1, 2018
117
250
Kumetokea ajali ya ndege ndogo iliyokuwa ikiruka kutoka uwanja wa ndege Mafia, Kamanda Polisi, Kanda Maalumu ya Kibiti, Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na atatoa taarifa zaidi baadaye. Video kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio.
 
Attachments

  • File size
    2.1 MB
    Views
    42

Nassibamry

JF-Expert Member
Jul 3, 2014
330
500
Habari zilizotufikia hivi punde, imeelezwa kuwa ndege ndogo iliyokua na abiria wapatao ishirini imedondoka pembezoni mwa uwanja wa ndega wa Mafia.

Ndege ilikua imeruka kutoka uwanja wa ndege wa Dar es salaam na kutua uwanja wa ndege wa Mafia ambapo abiria kumi na mbili walioshuka Mafia walieleza juu ya misukosuko waliyoipata wakiwa angani na kuonesha mashaka juu ya usalama wa mdege hiyo.

Hata hivyo baada ya mda mchache ndege hiyo iliruhusiwa kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Mafia ikiwa na abiria nane ambapo dakika moja na nusu baada ya kuruka ilidondoka pembezoni mwa uwanja huo na kuteketea yote kwa moto.

Taarifa zinaeleza kuwa majeruhi watano kati ya abiri nane waliokuwemo kwenye ndege hiyo wamepatikana na wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu na watatu waliobaki hawajajulikana walipo mpaka sasa.

Tunawapa pole ndugu familia, ndugu jamaa na marafiki wote wa waliohusika kwa ajalai hiyo.
 
Rusende

Member
Jul 27, 2016
97
125
Nami nimepata taarifa muda huu,jamaa yangu amepigiwa Simu na ndugu yake,ngoja tufuatilie,mungu atupe moyo wa subra
 
Nassibamry

JF-Expert Member
Jul 3, 2014
330
500
Habari zilizotufikia hivi punde, imeelezwa kuwa ndege ndogo iliyokua na abiria wapatao ishirini imedondoka pembezoni mwa uwanja wa ndega wa Mafia.

Ndege ilikua imeruka kutoka uwanja wa ndege wa Dar es salaam na kutua uwanja wa ndege wa Mafia ambapo abiria kumi na mbili walioshuka Mafia walieleza juu ya misukosuko waliyoipata wakiwa angani na kuonesha mashaka juu ya usalama wa mdege hiyo.

Hata hivyo baada ya mda mchache ndege hiyo iliruhusiwa kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Mafia ikiwa na abiria nane ambapo dakika moja na nusu baada ya kuruka ilidondoka pembezoni mwa uwanja huo na kuteketea yote kwa moto.

Taarifa zinaeleza kuwa majeruhi watano kati ya abiria nane waliokuwemo kwenye ndege hiyo wamepatikana na wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu na watatu waliobaki hawajajulikana walipo mpaka sasa.

Tunawapa pole ndugu, familia, jamaa na marafiki wote wa waliohusika kwenye ajalai hiyo.
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
12,323
2,000
Ndege ni usafiri wa haraka sana ila shughuli yake ikianzisha misukosuko,chini kunakuwa ni mbali,juu hakuendeki,kinachobakia ni kusubiria yajayo...
 
MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
2,835
2,000
SO SAD 😭 😭 😭
sipendi usafiri wa ndege ni bora nipande boti nipite pale nungwi ikimwagika naogelea...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom