Mafao ya Wafanyakazi vipi, NSSF, PPF.... Are we serious!!!!!

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Nashangaa ni nini kinaendelea?

Huduma za afya ni duni, Hospitali hazina vifaa,madaktari wana migomo baridi (mishahara duni katika sekta ya afya), mfumuko wa bei, stress za maisha, elimu duni, mishahara haitoshi, sekta binafsi kunyanyasa wafanyakazi.

Je, ni nani anajua kuwa atafikisha hiyo miaka 55??????

Kama wameshindwa kuwalipa wazee hao wa Africa mashariki, je itakuwaje warithi wa hiyo pension watapewa hela ama wataishia kupigwa mabomu?

Wafanyakazi tukiwa Dhaifu, na serikali lazima iwe dhaifu.

Chonde chonde wafanyakazi tuzungumze.

Na Bila kutoa jibu la Haki, SENSA haifanyiki. TUGOMEEE SENSA.
 
Kwa taarifa Wafanyakazi wa mgodi wa Bulyang'ulu wameacha kazi na leo shughuli za mgodi zimefungwa isipokuwa zile za utawala. Sababu za wafanyakazi kuacha kazi ni sheria kandamizi za mafao (Miaka 55-60)
 
Mungu awape heri wafanyakazi bulyangulu hakika ni mfano bora na sasa wachukue kitendo cha uzalendo 04 -08-2012 tuanze mgomo wetu wote
 
Tusifanye mambo kwa jazba, kwani hii imepitishwa au bado inajadiliwa!! Ila nchi ya kijinga hii sijui hata hili swala la kijinga hivi linajadiliwa vipi.
Jamani tutakuja shikiana mapanga hapa, kodi yangu tu nayokatwa inanitoa machozi leo hii mniambia NSSF mpaka nifikishe 55! Ebo kama sitaki kufika huko je?
 
Wafanyakazi wote, TUCTA what is happening

Tuache uoga, tujipange
 
Tunasubiria kwa hamu sana hiyo Oct 30 Bunge lianze,yaani wakifanya mzaha bunge zima hakuna kurudi maana haiwezekani bunge zima halina taarifa muswada ulipitishwaje kazi yao kusinzia na kupiga makofi wakiwa wanasinzia...aibu sana,
 
Tunasubiria kwa hamu sana hiyo Oct 30 Bunge lianze,yaani wakifanya mzaha bunge zima hakuna kurudi maana haiwezekani bunge zima halina taarifa muswada ulipitishwaje kazi yao kusinzia na kupiga makofi wakiwa wanasinzia...aibu sana,

Mimi ni msikiliozaji mzuri wa Bunge lakini hili la mafao sikulizikia, inaonekana walikuwa wote wamekula wamevimbiwa halafu wanajambiana ndo wakapitisha hii kitu maana haiingii akilini hata kidogo
 
Back
Top Bottom