Taifa letu linaangamia kwa mengi lakini hili la kuwakatalia wafanyakazi hasa wa sekta binafsi fao la kujitoa au la kukosa ajira linarudisha nyuma juhudi binafsi za watanzania za kujikwamua kutoka dimbwi la umasikini hasa kipindi hiki ambacho makampuni na mashirika yanapunguza wafanyakazi.
Haiingii akilini mfanyakazi ambaye tena ni kibarua tu sio mwajiriwa, amejinyima vimichango vyake vikaenda NSSF, PSPF nk anafukuzwa kazi ana miaka 30 asubiri mafao laki 8 hadi miaka 60? Je, baada ya miaka hiyo 30 kupita hili laki 8 itakuwa na thamani tena. Kwani pesa hii asipewe imsaidie hata ufugaji wa kuku?
Kama serikali inawakopesha vikundi vya vijana na wakinamama laki 2, 3 haiingii akilini mtu mwenye laki 5 yake kwenye mifuko ya jamii asipewe mpaka baada ya miaka ya 60 hasa nyakati hizi ambazo taifa linajigamba kuelekea kwenye viwanda vya kati.