SoC01 Mafanikio yapo mikononi mwako

Stories of Change - 2021 Competition

Elly Twix

New Member
Sep 22, 2021
1
4
Je umewahi kujiuliza ni kwa nini watu waliofanikiwa kwenye maisha ni wachache kuliko ambao hawajafanikiwa? Kwa nini idadi ya wanafunzi wanaofika chuo kikuu ni ndogo sana ukilinganisha na wenzao wanaoishia njiani? Kwa nini baadhi ya wajasiriamali wanaanza biashara ndogo na baadae itakuwa na kuwa biashara kubwa huku wakiwaacha wenzao hapo hapo miaka nenda rudi?

Je, ni kweli kuwa kuna watu wana bahati au wana akili kuliko wenzao?

“Mafanikio ni safari sio hatma. Unafanikiwa ukiwa njiani”

Mafanikio ni moja kati ya misamiati maarufu katika ulimwengu wa leo. Mwanafunzi anataka kufanikiwa ktk ulimwengu wa leo. Mwanafunzi anataka kufanikiwa katika mitihani yake ndio maana anakuwa tayari hata kuibia au kuiba mtihani au hata kutoa rushwa ili apate mafanikio katika taaluma yake. Mfanya biashara naye anatamani awe na biashara kubwa inayomwezesha kupata kipato kikubwa kutakachomfanya akidhi mahitaji yake naya watu wanaomzunguka. Hali kadhalika watumishi wa Mungu kama wachungaji, mitume, manabii na wengine wanatamani kuwa na washirika wengi kwenye makanisa yao, kuwa na nguvu ya Mungu inayojidhihirisha kwa matendo makuu na miujiza.

Shauku hii ya kutaka kufanikiwa iko katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu bila kujali taaluma au ujuzi alionao.

Mafanikio ya kweli hayaji kirahisi. Nyuma ya kila mafanikio ya kweli kuna MCHAKATO. Mara nyingi kinachomtofautisha tajiri na maskini, mwanafunzi anayefanya vizuri na anayefanya vibaya, na mafanikio ya kweli na yale yanayopatikana kwa njia za mkato ni utayari wa kupitia mchakato wa kufikia mchakato wa kufikia mafanikio ya kweli.

Kila mwanadamu anapenda kufanikiwa ila ni wachache walio tayari kupitia kwenye huu mchakato.

Siku moja nilikuwa nikisikiliza kipindi flani kwenye runinga. Bilionea wa kimarekani aitwaye Henry Ford ambaye anamiliki kampuni ya magari ya Ford aliulizwa kwenye mahojiano na mwandishi wa habari.”Ikitokea leo umepoteza utajiri wako wote itachukua muda gani kuurudisha?” Aliuliza mwandishi. “Itachukua miaka mitano tu” Alijibu.

Yule mwandishi akiwa na uso wa kutokuamini kama inawezekana utajiri ule mkubwa kurudi ndani ya miaka mitano ilihali umepatikana kwa miaka mingi aliuliza tena; Kwa nini unadhani utaweza kuridisha ndani ya miaka mitano wakati uliupata kwa miaka mingi zaidi? Ford akasema, kwa sababu najua nilikopita hadi kufika hapa nilipo. Niliweza kugundua kuwa Ford alikuwa na uhakika kuwa anaweza kupoteza utajiri wake wote lakini hawezi kupoteza ujuzi na uzoefu alioupata kwenye mchakato wa kupata utajiri wake.

Kilichomfanya awe tajiri ulikuwa mchakato alioupitia ili kupata utajiri wake. Hii inamaanisha angepoteza kila kitu angepita tu njia ile ile aliyopita mwanzo na wakati huu angepita tu njia ile ile aliyopita mwanzo alioupitia ili kupata utajiri wake. Hii inamaanisha angepoteza kila kitu angepita tu njia ileile aliyopita mwanzo na wakati huu angepita angepita kwa haraka zaidi kwa sababu alikuwa anajua ni wapi kuna mlima, wapi kuna bonde na wapi kuna utelezi. Inakuwa sawa tu na mtu anayerudi nyumbani kwake kwa njia ileile anayopita kila siku.

Wakati nipo kidato cha kwanza mwaka 2015 ni miaka mitano nyuma iliyopita nilimsikia mtanzania mmmoja aitwaye Mohamed Dewji ambaye ni mmiliki wa kampuni ya MO, alishinda tuzo ya mfanyabiashara bora kijana anayetoka bara la Afrika iliyoandaliwa huko marekani. Alihojiwa katika kipindi cha BBC Star TV na moja kati ya maswali aliyoulizwa na niliweza kuwa attention sana ni kwamba nin ilikuwa siri ya mafanikio yake? Nilikaa vizuri kabisa nikiwa tayari kusikiliza jibu lake. Dewji akajibu kwamba “Siri ya mafanikio yangu ni kuhangaika”.

Aliongeza pia kuwa tangu akiwa mdogo wakati waliporudi likizo wakati wenzake wanacheza mpira yeye alifanya biashara na baba yake kwenye miradi ya familia.

Alisema kwa msisitizo mkubwa “Mafanikio haya ambayo kila mtu ananipongeza kwayo leo ni matokeo ya mchakato nilioupitia tangu nikiwa mdogo”. Mchakato huu umehusisha mihangaiko mbalimbali na wakati mwingine kulazimika kufanya tofauti na watoto wa umri kama wa kwangu .

Mchakato huu ndo unaokujenga nidhamu ya kutawala mafanikio yako.

“Bingwa hatengenezwi ulingoni kinachofanyika pale ni kumtambua tu”.

Mwanafunzi wa kwanza kwenye matokeo hawi wa kwanza siku ile matokeo yakibandikwa, kinachofanyika pale ni kumtambua tu.

Mwanafunzi wa kwanza anatengenezwa tangu siku ya kwanza ya mwanzo wa muhula wa masomo. Jinsi anavyohudhuria vipindi, mahusiano yake na walimu, anavyofanya kazi za darasani kwa wakati na anavyotumia muda wake vizuri.

Kinachofanyika siku ya kutangaza matokeo ni kumtambua tu lakini alishakuwa wa kwanza kuanzia kwenye maisha yake ya kila siku.

“Championship is a lifestyle”

Mrisho Ngasa mmoja wa wachezaji soka wenye historia zilizotukuka katika ulimwengu wa wabongo hapa duniani aliwahi kusema na nitamnukuu, “Nilichukia kila dakika ya mazoezi, ila nikajiambia usiache. Teseka sasa hivi ili uishi maisha yako yote yaliyosalia kama bingwa”.

Kila mtu aliyefanikiwa unayemfahamu kuna kipindi flani cha maisha yake alifanya zaidi ya kawaida. Alisoma wakati wenzake wamelala, alifunga akamuomba mungu wakati wenzake wanakula vyakula wanavyovipenda, alisoma biblia kutoka kava la mbele hadi la nyuma wakati wenzake wanachati kwenye mitandao ya kijamii.

Mafanikio ya kweli hayaji kirahisi. Hata Yesu kristo aliweka wazi kabisa kuwa mtu yeyote anayetaka mafanikio katika safari ya kumfuata yeye lazima ajikane mwenyewe na ajitwike msalaba wake siku zote amfuate. Hii maana yake ni kuwa kufanikiwa au kutokufanikiwa kwako katika safari ya kumfuata kristo kunategemea sana utayari wako wa kujikana na kutwika msalaba wako siku zote. (Marko 8:34).

“Kupumzika wakati wa maandalizi utahangaika wakati wa mapumziko”

Watu wengi wanaota moto kwenye jiko lisilo na kitu. Wamekaa chini wakisubiri kupata joto kutoka kwenye jiko ambalo hawajawahi kuliwasha. Unamkuta mwanafunzi wa kidatocha tano au cha sita anasoma kama mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne anavyosoma magazeti na hadithi wakati akisubiri matokeo. Analala kabla ya wakati na kuamka kwa kuchelewa.

Mafanikio yana mdundo fulani kama mdundo wa muziki (Success has a rhythm) Wanaofanikiwa ni wale tu wanaoweza kuimba na kucheza kwa kufuata mdundo huo. Hivi nini kinatokea pale muimbaji anapokuwa anaimba wimbo wa taratibu alafu ghafla wapiga mziki wakapiga sebene?

Bila shaka huyu muimbaji atashindwa kuimba na atapaswa aidha kufuata mziki au kuacha kuimba.

Huwezi kufanikiwa bila kufuata kanuni za mafanikio.

Kama una ndoto fulani alafu ukakosa utayari wa kujitoa mzima kupitia mchakato wa kuifikia itaishia tu kuwa ndoto ya mchana . Kwa mfano, ukiona gari nzuri ukaipenda alafu ukaishia hapo ni wazi kuwa hutakuja kuwa nalo. Lakini uliliona, alafu ukalipenda na ukapiga hatua zaidi ukajua gharama la kuipata na ukafanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kuweka akiba ya kiasi flani cha fedha kwa mwezi au wiki ni wazi kuwa una uwezekano mkubwa zaidi wa kulipata.

Kama una ndoto fulani halafu hufanyi chochote ili kuifanya itokee hivyo ndoto itabaki kuwa ndoto siku zote. Haitakuja kutokea.

“ Watu wa kawaida wako kila mahali ila watu wa tofauti wako maeneo maalum, hawafanyi kila kitu na hawaendi kila mahali”

Ninapenda kumshukuru Mungu wa mbinguni kwa kunipa fursa hii adimu ya kufikiria na kuweza kuwashirikisha wanadamu wenzangu yale ambayo amenipa neema ya kuyajua. Namshukuru pia kwa kipaji alichoweka ndani yangu kwa ajili yangu na watu wengine.

Pia nimshukuru mama yangu nimpendaye sana kwa kuinua kipaji changu na kunisupport kwa kiasi kikubwa mno.
 
Back
Top Bottom