Mafanikio ya serikali ya AWAMU YA NNE katika MAPINDUZI YA KILIMO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafanikio ya serikali ya AWAMU YA NNE katika MAPINDUZI YA KILIMO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mujumba, May 21, 2012.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Zifuatazo ni juhudi zimezofanywa na serikali hii ya awamu ya nne chini ya Rais shupavu Mh.Jakaya Kikwete katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania.

  Lengo la kwanza: Kuweka misingi ya mapinduzi ya kilimo (Ibara ya 30-33)
  UTEKELEZAJI: Kwa kutambua nafasi maalumu ya kimkakati ya sekta ya kilimo katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini ,serikali iliyo chini ya chama cha mapinduzi imefanya yafuatayo:
  1) Kutayarisha na kuanza utekelezaji wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo (ASDP). Programu hii sasa imehuishwa na kufanyiwa marekebisho na kuiwezesha Nchi yetu kutia saini makubaliano ya programu kabambe ya kuendeleza sekta ya kilimo barani Afrika (COMPREHENCIVE AFRICAN AGRICULTURE DEVELOPMENT PROGRAMME (CAADP)
  2) Kutayarisha azma ya kilimo kwanza ambayo kwa sasa imekuwa ni ya mfano duniani.
  3) Kuanzisha dirisha la mikopo ya kilimo katika benki ya rasilimali (TIB)
  4) Kuanzisha mchakato wa kuanzisha benki ya kilimo.
  5) Kuanzisha mfumo wa kutoa ruzuku ya pembejeo kwa kutumia vocha
  6) Kufanyika kwa mikutano minne kati ya waziri mkuu na wadau wa sekta ya kilimo kuhusu mifugo, uvuvi na utafiti.

  LENGO LA PILI: KUBUNI MPANGO KABAMBE WA KUENEZA MATUMIZI YA PLAU NA ZANA ZA KISASA ZA KILIMO.(Ibara ya 31(b)

  UTEKELEZAJI:
  1. Matumizi ya majembe ya kukokotwa na ng'ombe yameongezeka kutoka 585240 mwaka 2005/2006 hadi kufikia 819360 mwa ka 2009/2010.

  2. Jumla ya matrekta 1737 yaliingizwa nchini yakiwemo makubwa 362 na madogo (power tillers)1379 kwa kipindi cha kuanzia 2006 hadi 2009.
  3. Mfuko wa pembejeo za kilimo umeongeza utoaji wa mikopo ya pembejeo za kilimo kutoka shilingi 4.9 mwaka 2005/2006 hadi shilingi bilioni 8.0 mwaka 2009/2010. Kwa wale wenye akili timamu naamini tumeona kuwa ni kwa kiasi gani serikali hii imefanya kazi juu ya suala hili.

  Karibuni tujadili bila jazba, matusi wala kejeli
   
 2. n

  ngoshas JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 710
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Asante sn kwa taarifu muhimu
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Mujumba,
  1. Kabla ya kuipiga bei CRDB, ilikuwa ni bank inayohusika na nini?
  2. Halafu kwanini tunafanya kazi ili tutake kusifiwa hata kama hatuja achieve kitu chochote? Tumesahau usemi kwamba megema akisifiwa, tembo hulitia maji?
  3. Mwisho wa yote kabisa, mafanikio na matatizo ya system yoyote ile yanapimwa kwa pamoja. Kilichozidi uzito ndicho kinachukuliwa kwa alama za juu kabisa. Ningependa kuachia muda upite wakati tunayaona na kutafakari kabla ya kusema nani ameshindwa na nani amefanya vizuri. Ila kujipigia debe si kitu kibaya maana hakuna uvunjaji wa katiba
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Haya mafanikio ni ya mezani. Bank TIB iko Dar, matrekta na power tillers ziko Dar, na hiki kiini macho cha vocha za ruzuku kinajulikana kwa watu wawili, Wassira na Prof Maghembe.

  "Kutayarisha azma ya kilimo kwanza ambayo kwa sasa imekuwa ni ya mfano duniani". Haya malengo ni ya Tanzania au dunia? Dunia ipi?

  Na mikutano nayo inakuwa mafanikio?
   
 5. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  hakuna mtu anayetaka kusifiwa, lakini pale inapotokea mtu mzima anakashifu hata yale mazuri yaliyofanyika na kwa namna moja ama nyengine amefaidika nayo then hatuna budi kuelezea mafanikio hayo
   
 6. m

  mamajack JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  The issue hapa sio kusifiwa tu,hayo yote uliyoeleza kama ni mafanikio,ni nani aliyefaidika nayo?

  mafanikio ya watu wachache ambao ambao kwanza hawajawahi hata kujua maisha ya mtanzania wa hali ya chini anaishi vipi ndo unayotaka tuyasifie, hebu tuache kuwa na sifa za mambo ambayo yapo kwenye makaratasi tufanye vitu vya kuonekana, wakulima wamekata tamaa, ila kwa vile wewe ni mkulima wa mfukoni ndio maana unaona kunahaja ya kusifu vitu ambavyo ndo kwanza vinawaumiza watanzania walio wengi na ambao wanaishi kwa kutegemea hicho kilimo.
   
 7. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  mkuu hebu rekebisha kidogo hapo kwenye caps letter halafu tuanze majadiliano!
   
 8. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  NAdhani sasa mnaweza kupata jibu kwanini Rais amekuwa akisafiri sana, leo tumeshuhudia jinsi alivofanikiwa kuendeleza KILIMO KWANZA, tayari SA wameshaonesha nia na wamarekani wanafuata!

  Heko na hongera Rais wetu JK, sisi wengine tunaona nini unafanya japo wengine hawataki kukubali! kweli WEWE NI JEMBE! tena jembe ulaya! Usirudi nyuma ! nashangaa watu kumponda JK, angalia pikipiki zilivojaa watu wwamepata ajira lakini hawamsifii, kitu kimoja tu ananiudhi JK kuwaondoa watu wa pwani kwa kisingizio cha miradi hilo linanikera!
   
 9. H

  Hume JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Haswaaaa mamajack,

  Mafanikio ya kwanza ya kilimo yalipaswa kuonekana kwenye masoko kwa bidhaa za kilimo kufurika na kupelekea bei zake kupungua kidogo kuliko ilivyo sasa.

  Haya mafanikio wanayoyapima kwenye makaratasi na takwimu zao hayana nafasi kwa Mtanzania, ndo maana sisi tunaona hakuna cha kusifia na wanabaki kusifiana huko marekani.
   
 10. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hivi haya mambo mbona huku kwetu kijiji cha mwamagigisi hatuyaoni? au ni kwa ajili ya watu wa dsm tu
   
 11. m

  mamajack JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ni kweli kunawalioona mafanikio kabisa,tena makubwa sana,angalia vijana wadogo wamemaliza masoma juzi wanamajumba ya kifahal,wanaendesha mavog,wakati wale walimaliza nao masoma hata kazi hawajapata maskini,na ndo hao wanateseka na familia zao huko vijijini,lakini wewe mkulima wa mjini,kilomo kwanza kimekutoa bila kuwa na shamba.heko kwako na kwa huyo mweshimiwa.
   
 12. pgasper

  pgasper JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 311
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hivi kuna mafanikio ya kusema?
   
 13. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Msitake tupigwe BAN mapema,mapinduzi gani haya ya kilimo watu wanakufa na NJAA???hivi tz inauchumi gani ambao unaipeleka KWENYE KIKAO CHA,G8,tatizo letu ni kupenda kusifiwa sana.
   
 14. w

  warea JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya mafanikio yanayoonekana kwenye hiyo mistari mbona hayaonekani sokoni na kwa mkulima?
  mnayaona ninyi peke yenu yamekuwa uchawi?
   
 15. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mafanikio ya kilimo kwanza mawakala wamekopwa fedha zao wengine mpaka wamefilisika,mbolea fake,pembejeo zinakuja wakati wa kuvuna,wale jamaa kuna kitu wanataka na kwa ujinga wetu tunachekelea mafanikio yako wapi?? Kg 1 ya mchele tsh 2,500/= wamepeleka powertiller vijijini huko zimepaki tu
   
 16. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mafanikio ya KILIMO KWANZA yataonekana kwa maisha ya wakulima sio takwimu.

  Mafanikio ya KILIMO KWANZA yataonekana kwenye idadi ya exportation sio ripoti.

  Mafanikio ya KILIMO KWANZA yataonekana kupitia jinsi kilimo kitakavyowezesha ukuaji wa sekta nyingi kama viwanda n.k na sio maneno ya Waziri, Katibu wa Wizara wala msemaji wa Ikulu.

  ACHENI POROJO.
   
 17. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Naam umenikumbusha, takribani watu laki 5 huko Arusha wanahitaji msaada wa chakula kuanzia sasa mpaka julai. Njaa inatoka wapi kama kilimo kwanza kimefanikiwa?
   
 18. m

  mamajack JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ndo hivyo mr bushman,and then watu ambao wameshiba wanakuja kutuletea habari za mafanikio ya kwenye vikao na posho za kamati,na nivijana ambao tunajua wanania ya kuijenga tanzania yetu iliyobomoka,
  tuwe wazalendo hata kwa asilimia chache,itatusaidia kabisa.

  kweli aloshiba ....................?

  lakini we hope yanamwisho.
  together we can.
   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Heading the thread inasema mafanikio ya serikali katika kilimo. Post iliyowekwa inaonyesha juhudu zinazofanywa katika kuleta mapoinduzi ya kilimo. Sasa

  1. Unataka kutuambia kuwa kwenu ninyi, kufanya juhudi tayari ni mafanikio?
  2. Kwa nini Mods wasiifute thread hii kwa sababu inapotosha?
   
 20. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Yah jibu tumelipata, alikuwa anatafuta walanguzi wenye bei nzuri waje kupora ardhi kwa mihela yao, na yeye apatiwe kajibanda huko ng'ambo.

  Ningekuona wa maana sana kama ungetoa takwimu za watanzania wangapi huko vijijini wamemilikishwa ardhi, wamepata hati za umiliki hivyo kuwa miongoni mwa wanaokopesheka. Wamenunua pembejeo za kisasa za kilimo, wameandaliwa mashamba darasa huko huko vijijini, ili wawe wazalishaji bora wa mazao ya chakula na biashara.

  Nchi iweze kuuza nje, tupate surplus balance of Trade. wewe unakuja na akili za kitumwa kama za huyo unaemsifia. Hopeless, Muarabu kuhitaji ekari laki tano ndio mafanikio? Laiti Mwl. Nyerere angeijua dhamira yenu angewazika wazima.

  Mtu mwenye damu ya kitumwa ni shida kujitambua, hata akipewa shamba lake na bwana wake, hatajiamini ni lazima arudi kwa bwana wake na kumuuliza "nilime nini?" Wewe ni mtumwa!!!!!
   
Loading...