bingu wa m
Member
- Aug 10, 2011
- 20
- 7
kwa muda wa miaka nyingi tumekua tukisikia serikali ikizungumza kilimo kwanza,ukimwuuliza mwananchi maana yake ni nini wengine wasema ni powertiler wengine ruzuku wengine hata wanayaita landcruiser new model kilimo kwanza,sishangai kwani wakala wengi wamechakachua mpaka haieleweki inamaanisha nini,kuna usemi unasema sera nzuri inatungwa tanzania inasomwa uganda na kutekelezwa kenya.tukirudi kwenye sera ya kilimo kwanza kwa mtazamo wa haraka tunazungumzia mkulima kubadilika kutoka kilimo cha jadi na kwenda kilimo cha kisasa cha kuzalisha gunia 40 kwa eka moja kama nchi zilizo endelea,sasa serikali yetu inadhani inaweza kumbadilisha mkulima huyu bila kurudi kwenye misingi kuu ya kilimo,kwanza ni kujua hali ya watu wako kua ni masikini mbegu ya 45000 kwa eka mbolea 120000,hatoweza na serikali haitoweza kutoa ruzuku milele huo niukweli,pili tuweze kuzalisha mbegu bora hapa nchini na kwa bei nafu tuepukane na uagizaji wa mbegu nje,ni aibu kwa nchi kama yetu eti asilimia 85 ya mahindi ya mbegu inatoka nje,tuhakikishe kila kata au wilaya yenye mito inatenga eneo la ku zalisha mbegu,tuinunue upya kiwanda cha mbolea na kuiboresha na hatimae wananchi masikini watapa mbegu na mbolea kwa bei nafuu,tunao wehu wanaodhani uchumi unaweza kukua bila mikakati ya dhati tumeishi kwa miaka mamia na kilimo cha jadi bila mabadiliko,tunafuga kwa kuzurura huku tunataka kubadilika tunadhani kutenga eneo la wakulima na wafugaji tumebadilika vita vya wakulima na wafugaji vitaongezeka kama hatutaki kujifunza kwa dhati kutoka nchi zilizo endelea leo hii marekani kwa siku moja wanachinja n'gombe laki moja na je wanapatikana kwa kuzurura,unamkuta mfugaji katoka katesh leo yuko anakimbizwa kwenye mpaka wa malawi na haelewi amefika mwisho wa tanzania ana mifugu hata familia yake haiwasaidii watoto hawaendi shule yeye amezeeka kwa kuzurura.tunahitaji serikali iliyo serious kama heart attack,badala ya kuongeza wizara tupunguze.mfano kuna hajagani ya kua na wizara ya ardhi na makazi,na ya kilimo.na mifugo.na huku huwezi kulima na kufuga bila ardhi hii ingekua wizara ya ardhi kisha ingekua na katibu wakuu wa tatu makazi,kilimo,mifigo.kama mtu ana ardhi ya kulima au kufuga au ya mkazi na hatumii wizara hiyo inaweza kua na mamlaka ya kuomba hati hiyo ifutwe na apewe anayeweza kutumia.