Mafanikio ya mwanaume!!

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,821
59,420
Kama wengi tunavyojua mafanikio ya baadhi ya wanaume hua yanategemea wanawake walio nao.Siwezi kusema wengi kwasababu wapo wengi wanaofikia kiwango kikubwa cha mafanikio bila wanawake...tho mwishoni hua wanahitaji/wanawatumia wanawake kuMAINTAIN mafanikio yao!

Binafsi hua nafikiria kwamba ntafurahi sana kukutana na mtu ambae ana potential ya kufika mbali ila anahitaji kusukumwa kidogo ili mimi ndo niwe hiyo ''force''. Mpaka nilipoongea na rafiki yangu mmoja kama wiki mbili hivi zilizopiata akaniambia kitu kilichonishangaza kweli.Nilishangaa kwasababu nilikua sijui wala sikuwahi kufikiria kwamba mambo yanaweza kua kama alivyoniambia!!

Aliniambia kwamba wanaume wanaosaidiwa (kusukumwa...kupewa mawazo...kupewa moyo na kuonyeshwa wanaweza zaidi ya wanavyodhani) na wanawake kufikia mafanikio yanayoonekana kwa kila mtu hua hawayafurahii kwasababu wao wanajua na kila mtu anaona kama sio mwanamke asingefika alipofika!Yani anaona kama amebebwa na mwanamke.

Maswali...
...Je ni kweli kwamba kina kaka (napenda kusema baadhi) hawayafurahii maendeleo yao kwasababu mwanamke ndie anaeonekana msababishi??
...Inawezekana kwa watu kama hawa wakashindwa hata kuwashukuru wenza wao hao kwasababu itadihirisha kwamba bila wao sio kitu??
...Kuna ubaya wowote kumENCOURAGE mtu kama unaona kabisa hajafikia kiwango ambacho anaonekana anaweza???

Hapa siongelei ile kumsema mtu mpaka ajisikie vibaya bali kumjulisha tu katika hali ambayo hata yeye ataifurahi!!!
 
Asante Lizzy kwa thread yako nzuri inayogusa moja ya sehemu muhimu katika mahusiano ya wenza.

Kwa uelewa wangu Lizzy ni kwamba ni muhimu kumpa a gentle push mumeo hasa kama anahitaji hio pushing (wanaume wametofautiana wengine bila gentle push hamfiki popote kimaendeleo). Ninaposema gentle push ni ile ambayo wewe kama mdada unamfariji mumeo na kuonesha you trust in him to reach his goals; unaona kabisa maamuzi anayotaka kufanya anachemka, but unatafuta njia na namna kupandikiza wazo linalofaa zaidi ili at the end of the day anafikiri ni yeye alilifikiria... hii ni muhimu sana katika ndoa kwa mwanaume ambae naturally kaumbwa hivyo kutokua na uelewa hivyo kumfanya afanye maamuzi ambayo yanaweza wakwamisha kimaisha.

Kwa upande wa ya kuonekana ndani ya jamii kua bila mwanamke huyo mkaka asingekua lolote mara nyingi inakua influenced kama inajulikana kabisa mwanamke ana kipato kikubwa sana zaidi ya mwanaume. But kwa wale wengine ambao wako level moja, au mwanaume ndo kazidi mnapo ongea mipango yenu ndani ni nani anajua kuwa mwanamke ndo alishauri au kumsukuma afanye hivyo?
 
baadhi ya wanawake huleta dharau au kujifanya miungu watu baada ya kushauri na mwanaume kupida hatua...hili haliwafurahishi wanaume....ukimpa ushauri au uwezo akasogea na heshima ikabaki pale pale na nafasi yake kama mwanaume,sidhani kama ataacha kufurahia.....otherwise, ni ego zao tu zinawasumbua,wanapenda kuwa in control ya maisha yao.....:bange:
 
Sidhani kama kuna ubaya wowote wa kumshauri mwenza/mume wako hata ikifikia ukaanza-kumpush ili afikie potentials zake kama ni kibiashara/kikazi/kimasomo etc etc.
Binafsi ningependa kuwa na mwanamke wa type hiyo, na sio kuwa na yes-womana ambaye hana ushauri wowote wa kimawazo yaani yeye ni mpokeaji wa kila kitu.
The bottom line ni uwe tu makini na lugha utakayoitumia wakati unajaribu kumshauri ama kumpush huyo mwenza wako. Avoid sana sounding too pushy, ama too bossy...hapo tutakosana kwani utakuwa ni kero. Tafuta muda mzuri ambao mwenza wako mood yake itakuwa poa na relaxed, then mwambie kiungwana...nitaelewa.
you made my day!!
 
Moja kati ya mambo ambayo mwanaume mara nyingi hujisifia ni kupata mwanamke aliyebora, mwanamke muelewe, anayejuwa shida ni nini, anayeweza kutoa msaada mzuri pale unapohitajika, anayeweza kupanga matumizi mazuri kwa kidogo kinachopatikana, anayejua kutumia njia nzuri za kukikuza kidogo mulichonacho. Mwanamke mwenye sifa kama hizo tunampenda. Na wanaume wengi hawawapendi/hawafurahishwi na wanawake ambao wanakuwa bize zaidi na kazi kuliko uangalizi wa familia zao, wenye kujiona (dharau) kutokana na vipato vyao, wanaopenda matumizi makubwa n.k

Kusaidiana ni kitu kizuri kwa wenza, anayepinga kitu hiki ni mjinga+/mbinafsi. Over
 
Sidhani kama kuna ubaya wowote wa kumshauri mwenza/mume wako hata ikifikia ukaanza-kumpush ili afikie potentials zake kama ni kibiashara/kikazi/kimasomo etc etc.
Binafsi ningependa kuwa na mwanamke wa type hiyo, na sio kuwa na yes-womana ambaye hana ushauri wowote wa kimawazo yaani yeye ni mpokeaji wa kila kitu.
The bottom line ni uwe tu makini na lugha utakayoitumia wakati unajaribu kumshauri ama kumpush huyo mwenza wako. Avoid sana sounding too pushy, ama too bossy...hapo tutakosana kwani utakuwa ni kero. Tafuta muda mzuri ambao mwenza wako mood yake itakuwa poa na relaxed, then mwambie kiungwana...nitaelewa.
you made my day!!

Hapo kwenye lugha ndo wengi hua wanafeli....
Siku zote ukitaka kumkamata mwanaume legeza lugha tu!!!
 
Hapo kwenye lugha ndo wengi hua wanafeli....
Siku zote ukitaka kumkamata mwanaume legeza lugha tu!!!

Sasa Lizzy mbona unaonekana mtaalam na unakataa hutaki mume, mana a lady anaejua sauti ina nafasi gani katika mahusiano ina maana tayari unaweza handle mume.... Ile dinner nilosema nitaandaa mapema iwezekanavyo
 
Raha ya sifa USIFIWE na sio UJISIFIE
Na mbaya zaidi ni kujisifia na kujitangaza kumletea mwenzako mafanikio (hata kama ni kweli)
Anaeona ni sifa mbaya kumsifia mwanamke aliyemsaidia kwa sababu ya jinsia yake tu, basi ana tatizo si dogo
Napenda sana mwanamke, na nina hamu sana kupata mwanamke wa kunishauri ktk mambo yangu, maana najua nikichanganya na mawazo yangu tunaweza kufanikiwa kwa asilimia kubwa kwenye kila jambo.
 
Hahahha....Asha bwana..wengi tu wanajua sheria za mchezo...wakati mwingine hata zaidi ya baadhi ya wachezaji ila hawataki kuingia ili na wao wasiishie kuanguka na kuvunjika miguu!!Still....that dinner will be very much appreciated!!Niambie siku niandae kagauni ka RED !
 
Kwahiyo tatizo ni mwanamke kujisia/kuonyesha kwamba yeye ndo kisababishi????

Ni vizuri kweli kuona mna utayari wa kutaka watu wa kuwashauri nakushirikiana nao!!
 
Hahahha....Asha bwana..wengi tu wanajua sheria za mchezo...wakati mwingine hata zaidi ya baadhi ya wachezaji ila hawataki kuingia ili na wao wasiishie kuanguka na kuvunjika miguu!!Still....that dinner will be very much appreciated!!Niambie siku niandae kagauni ka RED !

Nimekupata... LOL..Tafadhali hako ka RED utakakokatupia hakikisha unaachia breathing space walau kidogo, si unajua tunaalika wale rafiki zake bachelaz ina maana huby atakuwepo - mume wangu nae ana macho Lizzy, lakini ngoja nitafute solution.....
 
Hehehe...ntahakikisha sizidishi kipimo ili nisije nikapata mwaliko ya kua nyumba ndogo!!!Hao bachelaz hao...naweza kuwapa chakuangalia hata siku nyingine!!
 
Nimekupata... LOL..Tafadhali hako ka RED utakakokatupia hakikisha unaachia breathing space walau kidogo, si unajua tunaalika wale rafiki zake bachelaz ina maana huby atakuwepo - mume wangu nae ana macho Lizzy, lakini ngoja nitafute solution.....

Lizzy naomba unipitie twende dinner kwa Asha,nitavaa kale ka gauni kangu ka RED tulikonunua wote..please do not dissapoint me.:bange:
 
Lizzy unajua nitafanyaje? sitaki wajue nina lengo la kukutanisha.... hawa wakijua jeuri, watajidai - cause J2 ya mwisho wa mwezi i cook for him and his friends; kupitia kwako itakua kama zari ... kama vile kuna issue tunataka kujadili, nia yangu uje and make an impression, tule wote dinner and pretend that they are not there ... si unajua hawa singles. najua tu wataomba namba yako hapo ndo watukua wamepotea.... LOL
 
LOL...Michelle wapo wa kutosha... mradi tu mjipange ma impressions....

Lizzy naomba unipitie twende dinner kwa Asha,nitavaa kale ka gauni kangu ka RED tulikonunua wote..please do not dissapoint me.:bange:
 
Lizzy naomba unipitie twende dinner kwa Asha,nitavaa kale ka gauni kangu ka RED tulikonunua wote..please do not dissapoint me.:bange:

Hehehehhe....dearest usisahau kamkanda keusi kuongeza nashki!!Ila nahope hatutaangukia kwenye dimbwi moja!!!
 
Lizzy unajua nitafanyaje? sitaki wajue nina lengo la kukutanisha.... hawa wakijua jeuri, watajidai - cause J2 ya mwisho wa mwezi i cook for him and his friends; kupitia kwako itakua kama zari ... kama vile kuna issue tunataka kujadili, nia yangu uje and make an impression, tule wote dinner and pretend that they are not there ... si unajua hawa singles. najua tu wataomba namba yako hapo ndo watukua wamepotea.... LOL

Dah....yani umesemakweli kabisa...mpaka wajione wao ndo wenye bahati kumbe movie ilishaandikwa cast tu ndo hajakamilika!!!Lolzzz!Embu fanya fasta huo mpango bibie.....
 
Hehehehhe....dearest usisahau kamkanda keusi kuongeza nashki!!Ila nahope hatutaangukia kwenye dimbwi moja!!!

Dearest sikuelewi tangia utoe ile thread yako nimekuomba feedback umegoma kunipa.....sasa hao ma bachelor wa kwa kina Asha,tukidondoka dimbwi moja naomba uwe tayari kuniachia......kwanza we bado mdogo....:third:

kamkanda keusi sitasahau,somo lako limenikaa....!!
 
Back
Top Bottom