Hakuna mwanaume malaya ila huwa wanajipoza tu kuondoa stress

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
Hakuna Mwanaume malaya, Wanaume wengi wanapitia magumu kwenye utaftaji wanajinyima wasile ili familia zao zipate. Mwanaume ni mtawala wa Mwanamke siku zote ni lazima aheshimiwe. Wanawake wasitarajie kabisa kuwa sawa na Wanaume, Mwanaume siku zote ni mtawala wa Mwanamke

Wanaume wengi wanakimbia nyumba zao kwasababu ya midomo na maneno machafu kutoka kwa wake zao, Wanaume hawapendi. Lakini pia kuna wanaume wanapigwa na wake zao ila wanaogopa kusema, natamani niwe mtetezi wao na yote ni kwamba tatizo la Wanaume wengi wa hapa Bongo wanapenda sana kuteleza au kupewa vya bure na Wanawake, waache uvivu watafute pesa.

Sababu kubwa ambayo ilinipelekea nianze kutetea Wanaume, nakumbuka siku moja nilikuwa nipo ofisini Kariakoo, kuna kaka mmoja alikuja akaniambia ("unajua kuna wakati mwingine narudi nyumbani sina hela kabisa, au wakati mwingine sili mchana sili asubuhi ile hela ambayo naipata huenda ni elfu 5 au elfu 10 naibana nikampatie Mke wangu. Lakini nikirudi nyumbani labda nimempatia Mke wangu elfu 5 lakini Mke wangu hatosheki ananirudishia pesa na maneno ya kashfa kwamba ndio pesa gani hii unaniletea tangu ulipoondoa asubuhi unakuja na pesa kama hii!!)"

Kwahiyo yule kaka alikuwa anaishi kwenye maumivu alafu hasemi na hawezi kumwambia mtu yoyote kwasababu ni Mke wake. Nikamuuliza kwa mfano Mungu akisema waliopo kwenye ndoa watoke wewe utatoka? akaniambia yani mimi ndio nitakuwa wa kwanza kutoka kwenye ndoa kwasababu sasa hivi naishi kwenye ndoa kwasababu ya watoto.

Kuanzia hapo niliingiwa na huruma nikaamua kuwatetea Wanaume

Viola Mtetezi na msanii wa maigizo.
 
"Hakuna Mwanaume malaya, Wanaume wengi wanapitia magumu kwenye utaftaji wanajinyima wasile ili familia zao zipate. Mwanaume ni mtawala wa Mwanamke siku zote ni lazima aheshimiwe. Wanawake wasitarajie kabisa kuwa sawa na Wanaume, Mwanaume siku zote ni mtawala wa Mwanamke"
"Wanaume wengi wanakimbia nyumba zao kwasababu ya midomo na maneno machafu kutoka kwa wake zao, Wanaume hawapendi. Lakini pia kuna wanaume wanapigwa na wake zao ila wanaogopa kusema, natamani niwe mtetezi wao na yote ni kwamba tatizo la Wanaume wengi wa hapa Bongo wanapenda sana kuteleza au kupewa vya bure na Wanawake, waache uvivu watafute pesa"
"Sababu kubwa ambayo ilinipelekea nianze kutetea Wanaume, nakumbuka siku moja nilikuwa nipo ofisini Kariakoo, kuna kaka mmoja alikuja akaniambia ("unajua kuna wakati mwingine narudi nyumbani sina hela kabisa, au wakati mwingine sili mchana sili asubuhi ile hela ambayo naipata huenda ni elfu 5 au elfu 10 naibana nikampatie Mke wangu. Lakini nikirudi nyumbani labda nimempatia Mke wangu elfu 5 lakini Mke wangu hatosheki ananirudishia pesa na maneno ya kashfa kwamba ndio pesa gani hii unaniletea tangu ulipoondoa asubuhi unakuja na pesa kama hii!!)"
"Kwahiyo yule kaka alikuwa anaishi kwenye maumivu alafu hasemi na hawezi kumwambia mtu yoyote kwasababu ni Mke wake. Nikamuuliza kwa mfano Mungu akisema waliopo kwenye ndoa watoke wewe utatoka? akaniambia yani mimi ndio nitakuwa wa kwanza kutoka kwenye ndoa kwasababu sasa hivi naishi kwenye ndoa kwasababu ya watoto. Kuanzia hapo niliingiwa na huruma nikaamua kuwatetea Wanaume"-Viola Mtetezi na msanii wa maigizo.

Anaishi kwenye ndoa sababu ya watoto, ila Mungu akimwambia atoke atatoka, sasa Mungu akimwambia atoke hao watoto wataenda wapi?

Chukua hatua, haki Elimu
 
Mwanaume akikuhadithia wewe wa kike(ambaye sio ndugu yake) matatizo ya ndoa yake mixer kujitilisha huruma ujue anatengeneza mazingira ya kukukaza kwasababu anajua wanawake wana huruma

Eti akiambiwa atoke kwenye ndoa atakuwa wa kwanza loh!

Kama bado hujampa stuka
Huyo yuko kwenye ndoa yenye furaha tu
 
Yamewahi kukukuta?
Mwanaume akikuhadithia wewe wa kike(ambaye sio ndugu yake) matatizo ya ndoa yake mixer kujitilisha huruma ujue anatengeneza mazingira ya kukukaza kwasababu anajua wanawake wana huruma

Eti akiambiwa atoke kwenye ndoa atakuwa wa kwanza loh!

Kama bado hujampa stuka
Huyo yuko kwenye ndoa yenye furaha tu
 
Hakuna Mwanaume malaya, Wanaume wengi wanapitia magumu kwenye utaftaji wanajinyima wasile ili familia zao zipate. Mwanaume ni mtawala wa Mwanamke siku zote ni lazima aheshimiwe. Wanawake wasitarajie kabisa kuwa sawa na Wanaume, Mwanaume siku zote ni mtawala wa Mwanamke

Wanaume wengi wanakimbia nyumba zao kwasababu ya midomo na maneno machafu kutoka kwa wake zao, Wanaume hawapendi. Lakini pia kuna wanaume wanapigwa na wake zao ila wanaogopa kusema, natamani niwe mtetezi wao na yote ni kwamba tatizo la Wanaume wengi wa hapa Bongo wanapenda sana kuteleza au kupewa vya bure na Wanawake, waache uvivu watafute pesa.

Sababu kubwa ambayo ilinipelekea nianze kutetea Wanaume, nakumbuka siku moja nilikuwa nipo ofisini Kariakoo, kuna kaka mmoja alikuja akaniambia ("unajua kuna wakati mwingine narudi nyumbani sina hela kabisa, au wakati mwingine sili mchana sili asubuhi ile hela ambayo naipata huenda ni elfu 5 au elfu 10 naibana nikampatie Mke wangu. Lakini nikirudi nyumbani labda nimempatia Mke wangu elfu 5 lakini Mke wangu hatosheki ananirudishia pesa na maneno ya kashfa kwamba ndio pesa gani hii unaniletea tangu ulipoondoa asubuhi unakuja na pesa kama hii!!)"

Kwahiyo yule kaka alikuwa anaishi kwenye maumivu alafu hasemi na hawezi kumwambia mtu yoyote kwasababu ni Mke wake. Nikamuuliza kwa mfano Mungu akisema waliopo kwenye ndoa watoke wewe utatoka? akaniambia yani mimi ndio nitakuwa wa kwanza kutoka kwenye ndoa kwasababu sasa hivi naishi kwenye ndoa kwasababu ya watoto.

Kuanzia hapo niliingiwa na huruma nikaamua kuwatetea Wanaume

Viola Mtetezi na msanii wa maigizo.
Yaani kungekuwa na uwezekano wa kukutana KIKAO cha Wanaume wote nchini kwa dharura ingekuwa nafuu

Aidha, nashukuru uongozi wa Wanaume kupitia kikao cha mwisho wa kikao cha mwisho mwezi June kule Arusha ulivyosisitiza UMOJA wa Wanaume hasa katika suala la Ndoa na Malezi na kupeana mirejesho mbalimbali.
 
Mwanaume akikuhadithia wewe wa kike(ambaye sio ndugu yake) matatizo ya ndoa yake mixer kujitilisha huruma ujue anatengeneza mazingira ya kukukaza kwasababu anajua wanawake wana huruma

Eti akiambiwa atoke kwenye ndoa atakuwa wa kwanza loh!

Kama bado hujampa stuka
Huyo yuko kwenye ndoa yenye furaha tu
Labda hujajua tu, mfariji mkuu wa Mwanaume ni Mwanamke, kubali au kataa

Pale mke anapomsumbua akili na mwili Mume wake akienda kwa Mwanamke mwingine kuongea nae (Hata asipopewa) basi akili, mwili na moyo unatulia vizurii

Note: Hata asipokupa, ila maongezi mazuri tu yanaponya achana na caring zingine
 
Wala sikatai kwenye ufariji hapo,iko wazi jinsia tofauti zina namna yake ya pekee kupunguza matatizo

Shida ni faraja inapoamua kuzidi
 
Mnatuonea tu bure, sisi ni viumbe wapole sana na wanyenyekevu kwa wenza wetu
wa hivyo mpo ila wenye kero pia wapo, mimi hakuna kitu sipendi kama maneno yaaani sipendi mpaka sipendi tena. Ukitaka kuninyima kitu tanguliza maneno hata sitohangaika nawe. Nadhani ndio maana sipendi mwanamke muongeaji sana
 
Back
Top Bottom