VoiceOfReason
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,194
- 1,375
Siwezi kusema ni mbaya kwa vile wasipofanya huwa wana furaha na wameridhika kwa hiyo kwa definition niliyoitoa (mmmh!!??) wanajiona kuwa weshafanikiwa though sisi tuliomzunguka tunaewza kuona kuwa ni wasted talent
Mi inaonekana siridhiki, na sitakaa nifanikiwe kimaisha (sijui wenzangu), maana;
Mwaka 1995 (form 1); niliamini siku nikiweza kusoma hadi nikafika chuo kikuu cha SUA nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha...
Mwaka 1998 (form 4); wakati wa kombe la dunia, niliamini siku na mimi nikwa nakaa kwenye nyumba yangu (hata chumba cha kupanga), huku nikiwa na TV yangu naangalia kombe la dunia, nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha...
Mwaka 2000 (form 6, bado sijafika SUA, sina TV), nikaongeza 'hitaji', kuwa siku nipate kazi, niwe najitegemea nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha
Mwaka 2002 (first year SUA); niliamini siku nikifanikiwa kuajiriwa kama mwalimu wa chuo kikuu nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha
Mwaka 2006 (4th yr, SUA); niliamini siku nikiwa na ajira inayonilipa kama laki nne hivi nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha
Mwaka 2007 (graduating SUA), niliamini siku nikiwa na ajira, nikaoa mke ninayempenda, nikawa na gari aina ya chaser, nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha
Mwaka 2008 (nimeshaajiriwa, nimeshaoa), niliamini siku nikiwa na mtoto, nikiwa na Masters, nikiwa na ajira nzuri zaidi... nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha...
Mwaka 2010; ninaamini siku nikiwa na nyumba yangu mwenyewe (ghorofa), kipato cha kutosha niende ninapopenda wakati wowotena mke wangu, nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha...
2011; ???
2012; ???
n.k ...
Conclusion; Asilimia 99 ya vitu nilivyokuwa natamani hadi 2008 nimeshavipata, lakini kwa sasa najiona niko duni sana kimaisha, natamani, natamani natamani, na natamani niibadilishe Tanzania ifanane na Netherlands (can you imagine?!!)
Nikiwaza watu 'waliofanikiwa' kimaisha (kifedha), wanavyoendelea kufight kutafuta pesa, nikiangalia watu waliofanikiwa kijamii na kisiasa wanavyoendlea kutafuta kufanikiwa zaidi, inabidi niamini hakuna siku nitakokaa 'nifanikiwe kimaisha'
Decision; Nimeamua kuwa nitatumia 60% ya kipato changu 'kuifurahisha nafsi yangu na ya familia yangu na 40% kuwekeza kwa ajili ya baadae, maana nimeshaona kuwa hakuna siku nitakayorizika eti nimeshavuna sasa nianze kula...
...?
...nini tafsiri yako ya mafanikio (yako) kimaisha kiasi kwamba unaamini kwa kufikia hayo utakuwa umefanikiwa!
...nawashukuru sana nyote kwa michango yenu jumapili ya leo...
kiukweli nimefaidika na mawazo yenu nyote na ningependa kutoa hitimisho hili
kwa jinsi nilivyowasoma na kuwaelewa na mtizamo wangu ulivyokuwa...;
mafanikio nm matokeo mazuri ya jambo, ustawi, fanaka
maisha nm muda wa uhai wa kiumbe
....nimejiridhisha hakuna binadamu ambaye atakuwaa na mafanikio kwa
asilimia 100%...lazima patatokea mapungufu sehemu mojawapo ya maisha yake.
...ndio kusema, kila mmoja wetu anawajibika kufurahia sehemu yoyote ya mafanikio yake maishani,
hata iwe ni ndogo kama mdudu chungu, mfano yule anayebahatisha hewa, mlo na maji...au yule aliyejaaliwa mali,
watoto, na upendo wa hali ya juu lakini moyoni mwake ameshindwa kuuondoa, wivu, chuki, na katika na hayo.
mwenyezi mungu atuongoze katika njia iliyo sahihi, na atuzidishie nuru ya kutambua neema zake alizotujaalia.
- amen -
king'asti umesema la maana sana...the higher we climb the harder we fall...!
unajua, nikiwa nje ya jiji hasa dar....huwa nawa admire furaha yao hawa wenzetu wanaoishi
maisha ya kijijini...
wakishajitosheleza kwa mazao na mifugo tu...wanaonekana 'hawana' presha nyingine za maisha.
...correct me if am wrong, otherwise i bet am going nutter huh!
usijali mwj1...nimeshamuelewa...anazungumzia self actualization kwenye maslow hierachy!
...lol!
Nt so fast moskwito,hivi mukulu aliposema Maisha bora kwa kila mdanganyika labda hatukumuelewa stds zake...
tulitakiwa kwenda msoga nu kutazama maisha bora yalivyo lol
...nawashukuru sana nyote kwa michango yenu jumapili ya leo...
Kiukweli nimefaidika na mawazo yenu nyote na ningependa kutoa hitimisho hili
kwa jinsi nilivyowasoma na kuwaelewa na mtizamo wangu ulivyokuwa...;
mafanikio nm matokeo mazuri ya jambo, ustawi, fanaka
maisha nm muda wa uhai wa kiumbe
....nimejiridhisha hakuna binadamu ambaye atakuwaa na mafanikio kwa
asilimia 100%...lazima patatokea mapungufu sehemu mojawapo ya maisha yake.
...ndio kusema, kila mmoja wetu anawajibika kufurahia sehemu yoyote ya mafanikio yake maishani,
hata iwe ni ndogo kama mdudu chungu, mfano yule anayebahatisha hewa, mlo na maji...au yule aliyejaaliwa mali,
watoto, na upendo wa hali ya juu lakini moyoni mwake ameshindwa kuuondoa, wivu, chuki, na katika na hayo.
mwenyezi mungu atuongoze katika njia iliyo sahihi, na atuzidishie nuru ya kutambua neema zake alizotujaalia.
- amen -
nadhani definition ya "mafanikio kimaisha" inatofautiana mtu na mtu kwa sababu inakuwa influenced na vitu vingi sana ikiwemo malezi, mazingira mtu aliyokulia, utamaduni wa eneo husika, pamoja na elimu
hahahaaaaa.. mbu, i took some time kufikiria hii kitu
usijali mwj1...nimeshamuelewa...anazungumzia self actualization kwenye maslow hierachy!
...lol!
Wapo ambao watatumia fedha kama kigezo cha kupima mafanikio yao. Wengine watatumia mali (tangible or intangible) walizonazo kama kigezo cha mafaniniko. Wengine legacy yao ni mafanikio tosha kwenye maisha. Ukweli ni kwamba watu wengi wana-equate mafanikio kimaisha na mali walizonazo (materialism). Lakini kuna watu wengi ambao wamefanikiwa kimaisha bila kuwa na mali nyingi. Wanaweza wasiwe matajiri kifedha lakini ni matajiri in life and values.
Katika tafisiri yangu ya mafanikio kimaisha naangalia zaidi sincerity kwenye matendo yangu, kuwa genuine kwenye mambo ninayofanya (actions speaks louder than words), wholehearted, honest, heartfelt, hearty, humility, personal integrity, kusimamia kile ninachokiamini na kutouza my morals, values na matendo yangu (japokuwa hii ni ngumu sana Tanzania - mfano unampeleka mgonjwa hosipitali unalizimika kutoa rushwa ili kuokoa maisha yake).
Pia naangalia uwezo wa kutenganisha emotions in my judgments (this is difficult but it worth a lot), kuwa focused on what I want in my life na kuwa na good manners hata kwa wale ambao hawana good manners na kuto-dominate mazungumzo (let the others speak whilst I listen to them).
Kuelewana na watu hasa wale ulio karibu nao ni mafanikio makubwa sana kimaisha. Kusaidia wengine (hasa wale wasiojiweza) bila kujali kama nao watakusaidia. You don't need to be rich to be charitable. Mafanikio mengine kimaisha ni kutambua na kuzingatia kuwa kila mtu ni tofauti na anaweza kuwa na values na beliefs tofauti ya ulizonazo.
.....there is a conflict between both our conscious and unconscious mind. Our conscious mind tells us that we can succeed but your unconscious mind has a list of all of the reasons why you can't succeed. ..........
Mafanikio=success
mahitaji=needs.
Is someone trying to define mafanikio kama "kutimiza mahitaji"? coz this is the oly reason the malsow pyramid would be used.Needs can be considered as a valley, mafanikio as a hill. some make a hill with the waste from the hole, some keep the two separate, a little hill here, a little hole there. kuna mtu ana mahitaji kibao ila ana mafanikio pia, kuna mtu mafanikio yake humuongezea mahitaji, na kuna mtu ambae anafanikiwa kwa kutimiza mahitaji, moja baada ya nyingine, etc. this comparison is not relevant I think... or sijaelewa point yake