Maeneo mazuri ya kuishi Morogoro

Maeneo mazuri ya kuishi Morogoro

Varbo

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
1,124
Reaction score
895
Wana JF natamani sana kumalizia maisha yangu Morogoro ni maeneo gani mazuri kujenga nyumba ya kuishi na mtu anaweza kuishi kwa utulivu, mie Morogoro napitaga tu na kama kukaa nimeshakaa hotel moja kwa wiki mbili tu na sikua mtembezi hivo sina ufahamu wowote wa mji huo ila napapenda kutokana na hali yake ya hewa! Hivo naomba ushauri wenu mnaoujua huo mkoa vizuri!!
 
Perry mie namaanisha Morogoro mjini!!
 
Last edited by a moderator:
jamani na mie niko moro mjini kwa muda naomba mnielekeza sehemu ya ku-spend nyakati za jioni.
 
Tafuta kiwanja bigwa au sehemu za mgolole , misongeni. Kama una pesa nzuri/ndefu tafuta sehemu za Kigurunyembe na forest hill. Hata hivyo waone jamaa wa ardhi kupata kiwanja
 
Matombo na sehem ambazo watu wanajenga sana nyumba mpya mpya maana kila mkoa sasa unasehem Kama hizo kwa Moro ni wapi!?
 
georgeallen kwani viwanja mfano bigwa vinasimamia ngapi?!
 
Last edited by a moderator:
georgeallen kwani viwanja mfano bigwa vinasimamia ngapi?!
kwa bigwa/mgolole na misongeni weka budget ya m5-10 kwa kiwanja cha size - nusu ekari au ekari moja. Hata hivyo bei inaweza kupungua au kuongezeka kutegemea na muuzaji-dalali au mwenye kiwanja. kesho nitakupa bei halisi ya bigwa au mgolole au misongeni kwa kiwanja chenye ukubwa sawa.
 
Aksante sana mtu wangu nashukuru kwa Msaada mkubwa nadhani tutakua majirani Mungu akiwezesha! Ukipata jibu ni pm
 
Jamani na maeneo ya nanenane bei za viwanja kule ikoje? Na je ni pazuri?
 
Swali limekuja mda muafaka ukifanikiwa njoo utuabarishe nami napenda kuishi kwenye ule mji
 
chipukizi na kaumba ziko wapi mkuu? Na-drive

simama hapo kituo cha dalala mjini ulizia kaumba utaonyeshwa baada ya round about ya kati ya mji mbele kidogo ingia kushoto chipukizi ipo kulia barabara ya kushoto ni kaumba night park
 
simama hapo kituo cha dalala mjini ulizia kaumba utaonyeshwa baada ya round about ya kati ya mji mbele kidogo ingia kushoto chipukizi ipo kulia barabara ya kushoto ni kaumba night park

asante mkuu ngoja niende nikifika nitaku-pm kama upo moro tuonane
 
Back
Top Bottom