ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,115
- 49,833
Wote tumeona na kusikia Kikichotokea Hanang na maeneo mengine kama Arusha, Geita na Baadhi ya Nchi jirani Kwa kukumbwa na Mafuriko na maporimoko ya Mawe na uongo.
Kwa tahadhari tu, unapochagua kiwanja cha kujenga na kuweka makazi ya kudumu au taasisi ni vyema maeneo yenye sifa zifuatazo yaepukwe Kwa usalama zaidi.
1. Maeneo ya Kando Kando ya Bahari/Maziwa na Mito Mikubwa
Watu wengi wanapenda kuishi kando ya maeneo hayo ila Kwa taarifa Yako tuu hayo ni maeneo hatari zaidi Kuweka Makazi kwa sababu hukumbwa na Mafuriko(kuongezeka kwa ukubwa wa Maji na kuzamisha maeneo ya mwambao au jirani), Mafuriko yanayoletwa na vimbunga (Libya) au matetemeko ya Ardhi(Indonesia)
2. Mabondeni na maeneo Chepechepe (Mikondo ya Kupitisha na Kutunza Maji)
Watu wamekuwa wakijenga Mabondeni na maeneo yenye Asili ya maji Kwa kujifariji kwamba mkiwa wengi maji yatakimbia. Kwa taarifa yenu tuu ni kwamba Kuna siku maji yatarudi kama ilivyo hapo Jangwani na pia chemchem za kutosha zitatokea na kusababisha majumba kuporomoka.
3. Maeneo Jirani au Kando ya Milima Mikubwa
Maeneo kama haya hata yawe na Misitu ikiyopamba ila ni hayafai Kwa sababu Kuna siku Ardhi itazidiwa na maji(Saturated) na hivyo kusababisha maporimoko ya udongo na mawe. Katesh,Cameroon ,DRC nk.
4. Maeneo ambayo ni prone na Matetemeko na Active Volcano.
Mwisho Majanga ya Asili hayaepukiki (nature balancing) ila tunaweza punguza athari Kwa kuchukua hadhari.