Maendeleo ya watu au vitu?

L7 at work
ndio mimi ni lasaba, Sasa wewe uliesoma mbona unalialia humu, Au ulisomea kupewa pesa? Pambana ujenge nchi sio kulialia. Au wewe ni wale waliosoma ili wapate ajira? Ok karibu kitaa Kuna ajira kibao 😄. Kuna kazi zakupara samaki, hata kuparamiwa ikikupendeza.😎
 
Mkuu naamini haupo serious.
 
Maendeleo ya watu ndo kila kitu ,unajenga reli ambayo haina faida kwa nchi, unarudia uchaguzi asubui na jion Rais asiyekuwa na uwezo ndo anafanya hayo.
Wananchi wanapata majanga ya mafuriko njaa anasema hajaleta yeye majanga. Lakini uchaguzi unarudiwa jimbo hilo hilo anatoa bilioni 5 za uchaguzi tena harala sana.

Sijawahi kuona Rais mbinafsi kama Jpm
 
Wananchi wanapata majanga ya mafuriko njaa anasema hajaleta yeye majanga. Lakini uchaguzi unarudiwa jimbo hilo hilo anatoa bilioni 5 za uchaguzi tena harala sana.

Sijawahi kuona Rais mbinafsi kama Jpm
Truly
 
Tahadhari tusiingize sana siasa tujaribu kujenga hoja.

Sio siasa mkuu.
Ni utabiri wa Franz Fannon(The Wretched of the Earth) unatimia.
Ila nalikubali angalizo lako.
 
Well stated mkuu
 
Jamani eleweni hakuna maendeleo bila vitu pitieni kipindi cha industrial revolution ulaya na mataifa mengine. China,Malysia,vietnam,South Korea zimeendelea kwa ajili ya miundo mbinu nk ingawa pia elimu, afya, maji navyo vilipewa umuhimu. Watu na vitu huwezi kuvitenganisha. Awamu hii ya tano vyote vimeshughulikiwa ipasavyo, na tusichukulie pesa mfukoni zilizozagaa wakati wa awamu ya nne kutokana na rushwa kubwa,ufisadi,etc ndiyo pesa mnayotaka irudi. Haitawezekana. Mzunguko wa pesa una kanuni zake ili kuzuia inflation etc
 
Unajua sio kila jema analolifanya usiempenda ulitangaze kwa ubaya
Hii ni kutokuwa na uzalendo
Ndugu zangu maendeleo ya vitu nchini kwetu ni mwanzo mzuri wa kufikia hatua kubwa ya maendeleo ya watu
Tuseme ukweli miundombinu ya vitu ikaachwa honyo tutakawa fedha kwa kila mtu tutafikiaje maendeleo kama nyie si waongo
Muacheni mh rais asimamie miradi ya maendeleo.
 
bravo.
 
Labda WanaJF mtasaidia kujibu swali langu hili, Je, wapiga kura, wengi wao (70%) wanaishi vijijini, watapenda kusikia nini kutoka kwa Wagombea, ili waridhie kuwapa kura yao?
Vijijini Sasa hivi hawahitaji kuambiwa ili wampigie kura mtu wanahitaji kuonyeshwa siasa za kuwaambia watu kitu ili wakupigie kura zimepitwa na wakati

CCM tukienda hatuwaambii tunawaonyesha kuwa barabara hiyo imnaiona? Hospital hiyo nzuri mnaiona tumejenga.Umeme huo mnauona hapa kijijini ? Shule hizi nzuri watoto wenu wanasoma bure mnaziona? Na watoto wanaenda kusoma bure mnaona? Miradi hii ya maji ya hapa kijijini mnaiona? Nk ndio tunatamka tunwomba kura zenu tufanye makubwa zaidi

Ambaye hajafanya kitu ndie ahangaike kutunga vitu hewa ambavyo Watu wa vijijini wala hawana muda navyo[/QUOTE]
 
kila mtu yupo sahihi.. ila tunatofautiana usahihi kulingana na muda na hali halisi ya kimazingira.. kuna wakati maendeleo ya vitu ni sahihi zaidi kuliko maendeleo ya watu and vice versa is true too.
kwa uchumi tulionao sasa tukiwekeza kwa watu pekee tutajikuta tuna jopo la wataalamu ambao watabaki kuhangaika na elimu zao bila kuepo na nyenzo au mazingira rafiki ya wao kutumia huo uwezo wao binafsi hivo kupelekea lengo la maendeleo kutofikiwa ipasavyo ndani ya kuda stahiki,. ila pia tukiwekeza kwenye vitu kama ilivyo sasa inarahisisha na kujenga mazingira rafiki kwa watu kufika mbali kiuchumi maana shughuli zao hazitakua zikikwama kwa kisingizio cha miundombinu.

mimi naona maendeleo ya vitu ni urahisishaji wa maendeleo ya watu hvyo hzi concept 2 zinatakiwa ziende sambamba kisianze kimoja kifate kingine. maendeleo ya watu kwa ajili ya nchi yanahitaji kujituma ari na uzalendo, vinginevyo tutaishia kupiga kelele maendeleo yetu huku tumekaa kwenye vijiwe vya kahawa kusubiria kila kitu.
 
Hakuna ccm mpya ndugu ila ccm yasasa imerudi ya azimio la Arusha, CCM yakati hapo ilikuwa ccm ya wapenda ufisadi, wala rushwa nk kiukweli ccm ndan ya miaka 30 nyuma ilikosa uongozi imara na iliyumba na kuchukiwa sana na wanaochi mmoja wapo mi mwenyewe.

Kuhusu maendeleo ya vitu:- Miundombinu ndiyo kichocheo kikubwa cha uchumu Duniani, na kipindi cha JK wachumi wote wanakubaliana kuwa hakukuwa na udhibiti wa fedha, fedha nying zillikuwa haramu kias zilikuwa haziingii kwenye mzunguko wa uchumi zaid zikizagaa tu.
 
[/QUOTE]
Kama amhitaji kuwaambia Bali kuwaonyesha nguvu mnazotumia kuwadhibiti wapinzani ni za Nini??

Wekeni uwanjani uliosawa katika siasa tuone haya mnayoyasema Kama Yana ukweli.
 
Maendeleo watu hujiletea wenyewe kupitia miuondo mbinu wezeshi na rafiki na wakishaendelea uchangia maendeleo ya Taifa Kama kulipa Kodi vizuri na stahiki zitakazotumika kujenge miradi mikubwa Kama inayoendelea lakini tukianza mwisho ndiyo turudi nyuma yaani kwa wananchi Basi tutakuwa tumeendeleza vitu badala ya watu! Maana huyo mtu atakalia kulipia mikopo ya miradi iliyojengewa!!
 
Nakupa formula waliyo tumia mataifa [emoji2]

Kodi = maendeleo.

Vitu (havilipi kodi)
Watu (wanalipa)

Wanalipa watu gani? Wazalishaji

Mzalishaji ni yupi? Mwenye ujuzi wa kuzalisha yaani mwenye elimu.

Je tunaweza kutoa elimu kwa kila mtu? Ndio, si lazima iwe formal, hata non-formal. Yaani ya vyuo vya kati.

Vyuo vya ufundi vitazalisha wajuzi wengi; kodi nyingi, serikali itajenga vitu kwa namna itakayo. Rejea Uchina [emoji4]
 
Maendeleo ya vitu ni muhimu ili watu watumie hivyo vitu kupata maendeleo ya watu
 
Hizi ni fikra chanya kabsa. Pongezi kwako mheshimiwa
 
1. Nadhani tunahitaji barabara nzuri zaidi kuliko ndege. Barabara zetu za vumbi hasa zile zinazounganisha wilaya ni mbaya sana. Na ubaya wa barabara hizi zinaleta matatizo mtambuka. Tulidhani baada ya mh. Kikwete kuunganisha mikoa kwa lami, tulifikiri dhana hiyo ingehamia kuunganisha wilaya kwa lami
2. Wananchi na serikali wamejenga zahanati, vituo vya afya na sekondari za kutosha. Tulidhani kuajiri watumishi wa taasisi hizi ni bora kuliko SGR
3. Huko nyuma wanafunzi wote wa elimu ya juu walipata mkopo kwa sasa ni tofauti. Tulidhani mikopo kwa wanafunzi hawa ni muhimu kuliko fly over.
Nk. Nk.
Na hapa lawama ni kwa wabunge wetu ambao hupitisha bajeti ambazo haziakisi mahitaji ya wapiga kura wao.
 
ITAPENDEZA pia ukashuri aina ya chanzo cha mapato endelevu kugharamia mahitaji hayo uliyoyataja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…