Maendeleo ya watu, huleta mahitaji ya vitu! Maendeleo ya vitu badala ya watu, tutakuwa kama North Korea!Ni hoja ambayo imegeuzwa na Wanasiasa kama mtaji wa kisiasa na huenda ikatumika kama agenda kuu katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu. Kuna dalili ya kuelekea huko kutokana na jinsi Wanasiasa wanavyotafsiri taarifa ya Benki ya Dunia kuitambua Tanzania kama moja ya nchi yenye Kipato cha Kati.
Labda WanaJF mtasaidia kujibu swali langu hili, Je, wapiga kura, wengi wao (70%) wanaishi vijijini, watapenda kusikia nini kutoka kwa Wagombea, ili waridhie kuwapa kura yao?
Chige kaja na dhana ya microeconomics vs macroenomics ambayo kiasi inashabiana na hiyo yako jmushi1.
Kumekuwepo na mjadala mpana sana kuhusu mantiki mbili za maendeleo kwenye mitandao ya kijamii, nami ningependa kutoa maoni yangu kuhusu jambo hili, Kuhusu maendeleo ya watu na maendeleo ya vitu. Jambo la kwanza ambalo tunapaswa kutambua ya kwamba maendeleo ya vitu ni kwaajili ya watu. Watu ndio wanaotumia vitu na ndio walio vitengeneza kwaajili yao. Kwahiyo maendeleo ya vitu ni muhimu sana...
Kumekuwepo na mjadala mpana sana kuhusu mantiki mbili za maendeleo kwenye mitandao ya kijamii, nami ningependa kutoa maoni yangu kuhusu jambo hili, Kuhusu maendeleo ya watu na maendeleo ya vitu. Jambo la kwanza ambalo tunapaswa kutambua ya kwamba maendeleo ya vitu ni kwaajili ya watu.
Watu ndio wanaotumia vitu na ndio walio vitengeneza kwaajili yao. Kwahiyo maendeleo ya vitu ni muhimu sana. Na ndio hasa yanayofanya watu wafanye kazi kwa bidii ili wabadilishe mazingira yao na kuitawala dunia. Maisha yamekuwa rahisi zaidi kuliko karne kadhaa zilizopita kwasababu ya maendeleo ya vitu yaliyoletwa na vumbuzi kadhaa...
Watu hawajaendelea kama hawawezi kujenga madaraja kwa kutumia watu wao wenyewe, kujenga reli kwa kutumia watu wenyewe, ndege kwa kutumia watu wao wenyewe, barabara, bunduki na vifaa vya kijeshi kwa kutumia watu wao wenyewe na mambo mengine mengi wanayotumia kwa maisha yao wenyewe ya kila siku. Tunapima uwezo wa nchi na maendeleo yake kwa uwezo wa raia wake kutengeneza vitu wanavyotumia kila siku na sio kutumia wasichozalisha.
Hakuna maendeleo ya watu bila vitu. Dunia ilianza na vitu na hata Mungu alianza kuumba dunia na kisha mtu. Meli itasaidia watu kusafiri na kupunguza adha ya kusafiri kwa mateso hata kama wana pesa kama hamna vitu utazifanyia nini ingawaje ili uwe na vitu unahitaji watu na pesa kama mtaji tu kuzalisha ikiwemo ardhi...
Awamu hii inaboa sana, propaganda zimezidi wananchi hatuoni maendeleo ya maana, hali imekuwa ngumu sana. Tutajaribu wapinzani tuone mambo yatakuwaje.Ni hoja ambayo imegeuzwa na Wanasiasa kama mtaji wa kisiasa na huenda ikatumika kama agenda kuu katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu. Kuna dalili ya kuelekea huko kutokana na jinsi Wanasiasa wanavyotafsiri taarifa ya Benki ya Dunia kuitambua Tanzania kama moja ya nchi yenye Kipato cha Kati.
Labda WanaJF mtasaidia kujibu swali langu hili, Je, wapiga kura, wengi wao (70%) wanaishi vijijini, watapenda kusikia nini kutoka kwa Wagombea, ili waridhie kuwapa kura yao?
Swadakta, ndiyo nchi tajiri zilivyotajirisha watu wake na kuchochea Maendeleo ya Watu.
Tofauti na CCM Mpya yenye ufinyu wa mawazo kwa kukopi na kupesti reli SGR, madaraja na flyover za China kununua bombadier Canada au Dreamliner USA ili tu zionekane angani bila tija, kujenga stendi mpya za mabasi ambazo ni kubwa kuliko hospitali za rufaa za kanda ....listi ni ndefu
Na kujenga viwanja vikubwa vya michezo badala ya ghala za kuhifadhi chakula cha tahadhari.
Uwekezaji kama upi?Mimi kama hakuna uwekezaji wa kweli kwenye kilimo, hayo maendeleo mengine naona ni ya vitu zaidi.