Maendeleo ya China yaliletwa na Katiba Mpya?

Maendeleo ya China yaliletwa na Katiba Mpya?

usilinganinshe China na Tanzania kwa sababu zifuatazo

1) China hakuna wajinga kama bongo
2) level ya maendeleo kijamii na kielimu ni tofauti kabisa
3)China hakuna dubwasha linaloitwa ccm
4) Katiba yao sio mbovu kama yenu vile vile raisi wao haamkia asubuhi na kutoa matamko au kukirupuka kwenda kujenga airport bush kwao
5)raisi hateui watu hovyo hovyo hasa wananchi wakionesha kutokumkubali mfano bashite wenu
Mengine waweza ongezea maana unayajua sema unaleta uhayawani
 
Hatuji ila tutasema. Maendeleo ya China yameletwa na uongozi bora. Maendeleo ya Rwanda yameletwa na uongozi bora. Mwalimu alisema: "Ili tuendelee tunahitaji watu siasa safi na uongozi bora." Hakusema na katiba mpya. Maendeleo ya Tanzania yataletwa na uongozi bora. Watu wakiuunga mkono uongozi wa Awamu ya 5, kama walivyounga mkono uongozi wa awamu zote tutapata maendeleo. Tunaona itihada za Raisi wa awamu ya 5 katika kuleta uongozi bora nchini.Bial shaka hatua za kuelekea kupata maendeleo zimekwisha anza kuonekana.
Though sitaki kuamini,kweli hujui kuwa Tanzania tuna MTU anaitwa rais kwa kuwa katiba yetu ya 1977 inatoa cheo hicho? Sasa huyo kiongozi bora na siasa safi unavipataje kama hauna katiba bora? Jamani sometimes tufikirie na kutanda kama watu wenye akili
 
Mbona Tanzania haina katiba mpya! Na sasa ni zaidi ya miaka 50.....!

Tuna maendeleo gani?
 
Ndio mabadiliko ya katiba yao kuruhusu uchumi wa soko huria ndio yaliyochochea ukuaji wa uchumi wao. Kabla ya hapo walikuwa na uchumi hodhi wa kijamaa.
 
Hawa wasomi wanaosomea keypads ni shida kabisa! Mleta hoja huwezi hata siku moja kuilinganisha nchi yako na China kwani utapoteza muda na ama utajidanganya! Katiba nzuri na yenye kusimamiwa na kuheshimiwa ndiyo huwapa wananchi wenye katiba yao amani na ari ya kujiletea maendeleo. Hivyo china walifundishwa elimu ya uraia tena kwa lazima na ndio maana kule China nchi kwanza mengine yanafuata na wanaamini viongozi watapita kama alivyopita Mao lakini nchi inabaki!
Hapa kwenu mtu kwanza taifa baadaye si ndio? Hayo maendeleo yatakujaje huku mkiwa mnaongoza nchi kwa ilani badala ya katiba! Fikiri kama uliyekwenda shule angalau kunywa uji!
 
Katiba haileti maendeleo, lakini ni kwa namna gani Katiba mpya itazuia maendeleo unayoyaongelea? Ni kubadili tu maandishi na kupunguza nguvu kwenye taasisi moja na kuongeza kwenye taasisi nyingine. Labda sababu iwe si kipaumbele na haipo kwenye ilani ya chama tawala kwa sasa. Kama jinsi ambavyo Katiba haihusiki na kuleta maendeleo hivyo hivyo haizuii hayo maendeleo kuja. Maendeleo yanaletwa na Watz tena wa kawaida, Wachapakazi na Walipa Kodi. Katiba hata tukiibadili Watz Wachapakazi na Walipa kodi wataendelea kufanya majukumu yao kama kawaida.
 
Hatuji ila tutasema. Maendeleo ya China yameletwa na uongozi bora. Maendeleo ya Rwanda yameletwa na uongozi bora. Mwalimu alisema: "Ili tuendelee tunahitaji watu siasa safi na uongozi bora." Hakusema na katiba mpya. Maendeleo ya Tanzania yataletwa na uongozi bora. Watu wakiuunga mkono uongozi wa Awamu ya 5, kama walivyounga mkono uongozi wa awamu zote tutapata maendeleo. Tunaona itihada za Raisi wa awamu ya 5 katika kuleta uongozi bora nchini.Bial shaka hatua za kuelekea kupata maendeleo zimekwisha anza kuonekana.
Uongozi bora huu wa vituko vya kudanganya wananchi yakuwa umeokota vichwa vya treni Bandarini kisha ukavinunua? Au ungozi bora huu wakuongopea wananchi yakuwa wanaume Accacia wamekubali kutulipa mabillioni yetu ambapo imebaki kuwa historia? Au huu wa watu wasiojulikana wanaeua na kuteka watu bila kukaripia? Au huu wa kubagua wananchi kwa tamka hawa ndio walio nipigia kura hivyo wana haki zaidi ya wale? Au wa hivi vituko vya kutotaka kukosolewa pale unapokosea? Au wakudanganya wale wa Tanzania wapumbavu kuwa nchi yetu inapesa nyingi hatuitaji misaada kutoka nje wakati tunaomba mikopo kila siku? Au uongozi huu unaye mkataza mtoto wa kike aliyobakwa na kupata mimba kutoendelea na masomo? Au uongozi huu wakuwatolea maneno yakejeli na kuwanyima pesa za misaada wahanga Tetemeko huko Bukoba? Hivi unahisi Watanzania wa leo bado ni vilaza kiasi hicho? Kwa uwezo wako wakufikiri hapa JF siyo sehemu yake, hapa wengi wameelimika ukitaka kuamini angalia comments za humu utagundua vilaza mpo wachache sana.
 
Nani alikuambia katiba pekee inaleta maendeleo? Maendeleo yanategemea vitu vingi ila vya muhimu ni kufanya kazi na kuhakikisha pato linalopatikana linatumiwa kwa uangalifu. Hapa ndipo linapokuja suala la vitu kama katiba nk. Bila kuwa kanuni nzuri ya kupangilia mapato yako hata ufanye kazi kwa bidii namna gani hufiki mahali.

Kwa mfano kama unatumia matumizi yako kwa kufanya ujinga wa kununua 'wapinzani'' wako na kuendesha uchaguzi fake wa marudio unaotumia fedha nyingi kazi uliyofanya inakuwa ni bure. Hapa ndipo suala la sheria (katiba) nzuri za kukubana ili usifanye ujinga kama huu inakuwa na muhimu
 
Upo sahihi kabisa , Je unadhani kiongozi bila sapoti ya wananchi anaweza leta maendeleo. Chukulia familia ya watoto wavivu, wenye utapiamulo eti baba unahangaika kuwatengezea life
 
Kwa hiyo akikaa miaka 7 ndio tutapata maendeleo?

Wala, hata asikae miaka yote hiyo. Mbeya wanasema hajawatembelea tangia aingie madarakani. Akikaa miaka mingi madarakani maana yake sehem zingine za nchi zitakuwa zinasubiri kutembelewa kipindi cha kampeni tu, na rais wao.

Na kuna watu wanalalamika anachukua watu wa sehem moja ya nchi na kuwapa madaraka makubwa makubwa. Akikaa muda mrefu ikulu ya bongo wanaotoka mbali na ziwa la malkia watakuwa hawana bahati. Mwacheni akae yake 5 akapumzike
 
Huyu ndiye rais safi Kabisa kwa Maendeleo yetu, mambo ya katiba mpya haina maana tusipojitambua kuwa kufanya kazi kwa bidii na kusimamia vema rasmali zenu ndiyo msingi imara wa katiba tunayotaka, makanisani hawana muda wa kuhubiri kazi, kutwa sadaka nautoaji sasa wameanza katiba mpya
 
China ni China na Tz ni Tz, pia shida ya Africa hususani Tanzania tu nadhani kuwa njia iliyo tumika kutatua matatizo Ulaya au Asia ndio njia sahihi inayo faa kutatua matatizo yetu hapa.
Hii ni njia mbaya sana, kwasababu mazingira ya huko ni tofauti na sisi kabisa.
 
usilinganinshe China na Tanzania kwa sababu zifuatazo

1) China hakuna wajinga kama bongo
2) level ya maendeleo kijamii na kielimu ni tofauti kabisa
3)China hakuna dubwasha linaloitwa ccm
4) Katiba yao sio mbovu kama yenu vile vile raisi wao haamkia asubuhi na kutoa matamko au kukirupuka kwenda kujenga airport bush kwao
5)raisi hateui watu hovyo hovyo hasa wananchi wakionesha kutokumkubali mfano bashite wenu
Mengine waweza ongezea maana unayajua sema unaleta uhayawani
Hahaaaa yamboo:
 
Huyu ndiye rais safi Kabisa kwa Maendeleo yetu, mambo ya katiba mpya haina maana tusipojitambua kuwa kufanya kazi kwa bidii na kusimamia vema rasmali zenu ndiyo msingi imara wa katiba tunayotaka, makanisani hawana muda wa kuhubiri kazi, kutwa sadaka nautoaji sasa wameanza katiba mpya
Asieee nakushauri soma watu huko nyuma wamemwaga madini
 
Huyu ndiye rais safi Kabisa kwa Maendeleo yetu, mambo ya katiba mpya haina maana tusipojitambua kuwa kufanya kazi kwa bidii na kusimamia vema rasmali zenu ndiyo msingi imara wa katiba tunayotaka, makanisani hawana muda wa kuhubiri kazi, kutwa sadaka nautoaji sasa wameanza katiba mpya

Haya ni maoni yako aisee,...

Na maoni haya ni kutokana na level ya kiwango chako cha akili!

Ninakushauri uyasome maoni yako mara ya pili kama wewe mwenyewe utayakubali.

Maana nina uhakika uliandika kwa kukurupuka
 
Sawa leteni hayo maendeleo basi mpo madarakani over fifty years, bado nchi inategemea mawazo ya mtu mmoja.
 
Kumekuwepo na kelele kiasi toka kwa baadhi ya Watu ambao wanataka kufunganisha maendeleo ya Nchi yetu na Katiba Mpya au kwa kifupi maendeleo yanaendana na Katiba wanazofikiria wao zitawapa ''fursa''
Kwa mfano ndani ya KKKT tumeshihudia migogoro kadha sasa sijui wao Hiyo katiba mpya wataianzisha lini?? Na kuna viongozi wa Kiroho ambao utajiri wao unatokana na kuwadhulumu waumini wao kwa njia moja au nyingine ndio Maana hutakuta vitabu vyao vya mahesabu kuwa wazi zaidi ya kuwa somea waumini wao taarifa wanazo taka wao.
Ukija kwenye vyama vya siasa hadithi ni Hiyo Hiyo wakati wao wenyewe demokrasia wanayo ipigia kelele hawaienzi.
Ukija kwenye Suala la Maendeleo mfano china na mabadiliko Yao ya kiuchumi tunaona wame weza kufanya hivyo bila vyama vingi Bali kwa kuimarisha mifumo Yao ya kiutendaji wakati urusi walikwenda na Glasnot matokeo yake sote tunayajua Gorbachev akakosa nchi na Yeltsin na ulevi wake Ndio aka tawala nchi , matokeo yake nchi ilipojitambua wakamleta Putin ambaye Yupo madarakani kwa miongo miwili sasa.
Ukija hizo nchi za ulaya iwe Germany ya Hitler na wengineo tuangalie walivyo piga hatua za maendeleo ilikuwa kwa sababu ya katiba mpya au demokrasia au lilikuwa ni suala la uzalishaji na usimamiaji wa itikadi inayolenga ktk maendeleo.
Mimi nionavyo tupate maendeleo kwanza Ndio tutaweza kuweka hizo rangi zingine kulemba maendeleo yetu na sio kulemba kitu ambacho hatuna.
Unachanganya mambo. Ulipaswa ujikite kuelezea uhusiano kati ya maendeleo na katiba.
 
Wewe wasema ndio sera zenu Ndio Maana hamtaki mabadiliko ndani ya nyumba zenu au vyama vyenu. Akitawala fulani hakuna demokrasia lakini akiwepo Yule wa darasa la saba la zamani basi uwepo wake ni demokrasia tosha.
Tofautisha chama na nchi hii ni nchi ya watanzania wote tusio na vyama kama ww mwanaccm na tusio na dini vilevile maendeleao hayaji bila ya utaratibu mzuri utaratibu huo ambao unapatikana kwenye katiba hata nyerere mwanzilishi wachama chako alizungumza juu ya kuheshimu katiba
 
Hatuji ila tutasema. Maendeleo ya China yameletwa na uongozi bora. Maendeleo ya Rwanda yameletwa na uongozi bora. Mwalimu alisema: "Ili tuendelee tunahitaji watu siasa safi na uongozi bora." Hakusema na katiba mpya. Maendeleo ya Tanzania yataletwa na uongozi bora. Watu wakiuunga mkono uongozi wa Awamu ya 5, kama walivyounga mkono uongozi wa awamu zote tutapata maendeleo. Tunaona itihada za Raisi wa awamu ya 5 katika kuleta uongozi bora nchini.Bial shaka hatua za kuelekea kupata maendeleo zimekwisha anza kuonekana.
Uongozi bora wakibaguzi unaobaguwa baadhi ya wananchi wake kisa wanatofautiana kiitikadi huo ni uongozi gani rais anafanya shughuli za uenezi wachama chake kwenye shughuli za serikali kama kupokea wanachama ktk shughuli za serikali polepole anafanya siasa na mikutano ya hadhara wala polisi hawamshiki lkn vyama vyingine vikifanya mikutano polisi inawashika kwahiyo katiba inatakiwa ili rais yeyote atakayevurunda ashitakiwe baada ya uongozi wake
 
Back
Top Bottom