Maendeleo au demokrasia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maendeleo au demokrasia?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kichankuli, Jun 2, 2009.

 1. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 857
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Wana JF ni kipi bora kinachowafaa wananchi wa Tanzania kati ya Maendeleo na Demokrasia? Hebu fikiria wananchi wa Busanda na Majimbo mengine yaliyofanya na yanayotarajia kufanya chaguzi ndogokwa Mfano, tayari walishatumia demokrasia yao na kuwachagua Wabunge kwa ajili ya kuwawakilisha. Bahati mbaya Wabunge wao wamefariki dunia. Chukulia wananchi wa majimbo hayo wangepewa fursa ya kuulizwa kwamba wanahitaji kuchagua iwapo wanahitaji kumchagua mtu mwingine kuwa mbunge wao au wapewe fedha za Ruzuku zinazopewa vyama vya siasa kwa ajili ya kugharamia kampeni za chaguzi ndogo, na pia mshahara na marupurupu ya marehemu Mbunge wao wao kwa kipindi kilichobakia kabla ya uchanguzi mwingine zikiwemo zile fedha za kumaliza miaka mitano ili zitumike kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendelea ya jimbo lao kama vile ujenzi wa barabara, Miundombinu ya Afya, Elimu, n.k. wangechagua kipi?
   
Loading...