Maelfu ya watu wasio na makazi wamefariki dunia mjini London

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Maelfu ya watu wasio na makazi wamefariki dunia mjini London
Dec 16, 2019 12:12 UTC

Vyombo vya habari nchini Uingereza vimetangaza habari ya kufariki dunia maelfu ya watu wasio na makazi mjini London, mji mkuu wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, jumla ya watu elfu tatu wamepoteza maisha kwa kukosa makazi mjini London pekee katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Aidha takwimu hiyo iliyotolewa na asasi za misaada imeonyesha kwamba hadi sasa karibu watu laki tatu na elfu 20 hawana makazi nchini Uingereza wakiwemo watu laki moja na elfu 70 wanaoishi mjini London. Asasi za misaada ya kibinaadamu nchini Uingereza pia zimetangaza kwamba, karibu watu elfu tano hawana mahala popote pa kujihifadhi ambapo majira ya usiku hulala barabarani hadi asubuhi.

Tarehe saba ya mwezi huu kundi moja la wakazi wa mji wa London kwa lengo la kutangaza mshikamano wake na watu wasio na makazi mjini humo, lililala katika barabara za medani ya Trafalgar ya katikati mwa mji huo.

Hatua hiyo ilibuniwa na kundi moja la kujitolea kwa ajili ya kukusanya misaada ya kifedha ili kuwasaidia watu wasio na makazi kote duniani. Matatizo ya kiuchumi ambayo yameikumba Uingereza katika miaka ya hivi karibuni, yamebadilisha mfumo wa maisha ya wananchi na kuwalazimisha wengine kukimbia makazi yao kutokana na kushindwa kumudu gharama za kupangisha nyumba au kutokana na kudaiwa na benki.
4bso976a02ac231k0zu_800C450.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelfu ya watu wasio na makazi wamefariki dunia mjini London
Dec 16, 2019 12:12 UTC

Vyombo vya habari nchini Uingereza vimetangaza habari ya kufariki dunia maelfu ya watu wasio na makazi mjini London, mji mkuu wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, jumla ya watu elfu tatu wamepoteza maisha kwa kukosa makazi mjini London pekee katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Aidha takwimu hiyo iliyotolewa na asasi za misaada imeonyesha kwamba hadi sasa karibu watu laki tatu na elfu 20 hawana makazi nchini Uingereza wakiwemo watu laki moja na elfu 70 wanaoishi mjini London. Asasi za misaada ya kibinaadamu nchini Uingereza pia zimetangaza kwamba, karibu watu elfu tano hawana mahala popote pa kujihifadhi ambapo majira ya usiku hulala barabarani hadi asubuhi.

Tarehe saba ya mwezi huu kundi moja la wakazi wa mji wa London kwa lengo la kutangaza mshikamano wake na watu wasio na makazi mjini humo, lililala katika barabara za medani ya Trafalgar ya katikati mwa mji huo.

Hatua hiyo ilibuniwa na kundi moja la kujitolea kwa ajili ya kukusanya misaada ya kifedha ili kuwasaidia watu wasio na makazi kote duniani. Matatizo ya kiuchumi ambayo yameikumba Uingereza katika miaka ya hivi karibuni, yamebadilisha mfumo wa maisha ya wananchi na kuwalazimisha wengine kukimbia makazi yao kutokana na kushindwa kumudu gharama za kupangisha nyumba au kutokana na kudaiwa na benki.View attachment 1294986

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa faida ya wengi unaweza kutuwekea hiyo habari kwenye hicho chombo cha habari? Nitarudi baadaye na hii inaonekana kama ni uzushi tu.
 
Wengi wao wamejitakia kwani wanapewa nyumba za bure halafu hela za kujikimu wanaamua kulewa tu matokeo yake wanashindwa kulipa council tax na umeme, maji na gas
Hapo akifukuzwa anaamua kulala barabarani na kuombaomba kwa wapita njia.
Wengine ni wagonjwa wa maradhi ya akili wengi tu na wengine ni wale wametoka jela na hawana pa kwenda
Maisha kila mtu anachagua anavyotaka
Hizo takwimu sizishangai kabisa

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kwanini mnakubali kuporwa?
Aliyeileta amekusudia kuleta ile mitazamo yake Kiirani ili ku justfy yanayotokea huko anakokutetea.
Asichokijua ni kwamba hao wanaokufa kwa kukosa makazi wamekimbilia huko wakitokea katika nchi hizo hizo anazozipamba.
 
Back
Top Bottom