Maelezo yamejitosheleza

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,515
2,000


UNAPOAMUA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI NA KWA WAKATI SAHIHI...

Baadhi ya watu hupenda kukukatisha tamaa!


STORY YA NAZI: Mnamo mwaka 1998 nilinunua miche 12 ya nazi (mbegu ndefu) maeneo ya kwa

mfipa, kibaha, mkoa wa Pwani kwa bei ya Tshs. 800 kwa kila mche. Nilisafirisha minazi hiyo hadi

Mwanza na yote ilifika salama. Nilijaribu kuomba ushauri jinsi ya kupanda vizuri miche ya minazi

kwa mzee mmoja wa
makamu ambaye ni jirani yangu. Alichoniambia sitasahau mpaka

sasa...."kijana kuna miti mingine ni mikosi tu, wewe ulishaona wapi aliyepanda miti ya minazi huwa

anakula matunda yake? utakufa kabla ya kuziona hizo nazi" Nilifikiri na nikafanya maamuzi ya

kuendelea na utaratibu wangu kupanda miche hiyo. Bahati mbaya miche 4 ilikufa baada ya

kupanda na ikabaki 8. Baada ya miaka 9 nilianza kuona nazi zinatoka na baada ya muda nikaanza

kuvuna nazi. Kama ilivyokawaida ya ujirani mwema, niliamua kumpatia nazi 8 baada ya mvuno wa

kwanza alishukuru sana. Baada ya muda kupita hivi toka nimpatie nazi nikamuona naye anachimba

mashimo na kuniomba ushauri afanyeje ili aweze kupanda vizuri hiyo miche ya minazi, nilistaajabu

sana!! Na wala hakukumbuka tena yale maneno alioniambia. Baada ya muda nikaona mwamko

mkubwa wa majirani zangu kupanda miti ya minazi na sasa karibu kila nyumba zinazonizunguka

wamepanda minazi.

Photo: Huuni mmoja wa mti wa mnazi, ambao naendelea kuvuna matunda yake....minazi hii ina

uwezo wa kuzaa mpaka miaka 100.

KILIMO KINALIPA. Chanzo.Copy and Paste
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom