ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 19,630
- 44,898
Kwanza kimsingi Kabisa kilimo cha nchi zetu hizi za kimaskini return yake huwa ni ndogo sana tunalima basi tu ku jikeep busy na walau kupata chakula ila kutoboa ni uongo ndo maana wakulima ni wengi miaka yote maisha yao unayaona yalivyo. Kwa wale wakazi tunaoishi mikoa ya pwani na hasa pwani ya kusini Lindi, Mtwara na pwani yenyewe kuna mazao mawili maarufu sana mikorosho na minazi.Kwa mawazo yangu mimi nimeona kuna faida kuwekeza kwenye minazi zaidi kwa sababu.
1. Minazi haithariwi na mabadiliko ya hali ya hewa hata mvua inyeshe isinyeshe yenyewe itazaa kama kawaida, halafu minazi unaponunua tu shamba instantly unaanza kuvuna ila mikorosho ukisema uipande leo itabidi ukae miaka mitatu ukiihudumia ndipo ianze kutoa korosho.
2. Operation cost za minazi ni ndogo mfano shamba la minazi 100 unaweza ukawa na wakwezi wawili tu wanaosafisha minazi na kupanda na kuangua na hata malipo yao yanatokana nazi hizohizo utakazoangushiwa ila mikorosho yenyewe gharama kwenye kuandaa shamba, madawa na hata kwenye kuvuna yaani kila kipengele kinahitaji watu kama shamba kubwa lazima ulete kikundi cha watu 40 na wote wanahitaji hela.
3. Bei ya nazi inazidi kupanda maradufu na kila baada ya miezi mitatu unavuna nazi imagine mnazi mmoja ukatoa nazi 50 na una minazi 200 kila baada ya miezi mitatu unavuna nazi 1000 tufanye kila nazi unauza 700 maana yake una 700000 sio haba sana kama una mishe zako nyingine. Ila mikorosho haileweki kuna mwaka chali hupati kitu kisa mvua kubwa na bado bei inabadilika badilika.
NB: Shamba la minazi mikubwa kuanzia minazi 50 unaweza kuuziwa kwenye million 5 hivi mtu akiwa na shida.