Maelezo ya Waziri Faustine Ndugulile kuhusu WhatsApp calls yanaturudisha nyuma

Yaani watanzania sijui ni nani aliyeturoga wakati dunia za wenzetu uko wanawaza kwenda kufana utafiki mwezini sisi ndio kwanza tunaongelea wasap wakati wao teknolojia iyo wanatumia watoto wa shule,Yaani sasa Tanzania wakati tuwaze mambo ya dunia inavyokwenda bado tunakampeni ya kuhamasisha kampeni ya nyumba ni choo yaani hao wazungu wacha watuzarau kwakweli
 
Naona waziri hajazingatia kwamba ukipiga simu kwa WhatsApp unatumia mb za internet ambazo umeshalipia kwa kampuni ya simu kwa hivyo awe makini asicheze ngoma ya watoa huduma. Watoa huduma ni mabepari walaku kama fisi.
 
Signal, Viber, Delta Chat, Wickr me, Dust, Wire, Threema, Briar, Bridgefy na zingine nyingi Sana Na kama Telegram, Microsoft Teams, Zoom na Google Duo zipo kwenye simu yangu. Wablock tu WhatsApp waone tunavyotumia hizo hapo juu. Wenzetu wanazungumzia Mars, Bitcoin na Tesla yeye anakuja kuumiza raia. Duuh we are doomed.

Sent from my N20 using JamiiForums mobile app
 
1615411146327.png
 
Hahaha....yaani hii nchi hii!!!

Kila kiongozi anajifanya ni think tank, utadhani hiyo whatsapp inatumika bure, hivi hajui kuna watu wanaendesha biashara zao kupitia conf calls ambazo zinahitaji video au hata hiyo audio ambayo huwezi ifanya kwa kupiga simu kawaida...

Hebu huyo Waziri ajulishwe kuwa teknolojia inahama kutoka ile ya utamaduni wa zamani wa voice kwenda data...

Wakati sasa hivi dunia inakimbilia kwenye 6G na 5G, sisi bado tunataka kukomaa na ma old tech...
 
Huyu Waziri atakuwa mchawi. Yaani lengo lake wizarani ni kuongeza ugumu kapandisha MB, bado na WhatsApp. I think hii Wizara ni useless na huyu Waziri anajipendekeza kwa kuongeza ugumu wa maisha. Bora tu Bashite angeshindaga huko Kigamboni.
 
Kwa sasa Ndugulile ndiye waziri duni kabisa kuwahi kuhudumu kwenye awamu ya sasa akiwazidi kidogo Lugola na Mwigulu .
 
Hivi hii nchi ni kutunga sheria tu daily za kuumiza mwananchi.Uki like ama kucoment ,whatsapp call ,watoa hduma za usajili wawe leseni n.k. Nadhani hii ndio Wizara inayoshinda kutunda sheria zinazokandamiza mwananchi hebu watanzania tuwe tunaonea huruma huduma zinapo boreshwa kupunguza gharama ya maisha nyinyi mnaona hapana.

Mnataka tu wananchi mkate hela tu ya kodi sasa mbona shirika la posta nalo mapato yamepungua maana barua watu hawatumi wanatumiana kwenye e mail zao tu na huko nendeni mkakate mapato.

Wanakigamboni naona tulifanya makosa sana kuleta mtu huyu maaana huku kigamboni kuna changamoto kibao km wilaya mpya mfano huduma za maji,shule za msingi,barabara nk.lakini mbunge yuko busy kuwaza whatsapp call inauma sana.
 
Back
Top Bottom