Maelezo ya Padri Privatus Karugendo juu ya Uchumi na Utamaduni wa Kulalamika Tanzania

Zee la shamba

Member
Oct 17, 2007
55
4
Na padri privatus karugendo

Baada ya kuona kwamba si wote wanaoimba yale yanayompendeza kama alivyotarajia, sasa mkubwa ameamua kutoa amri na maelezo ambayo kwayo yatawakatisha tamaa wanaomkaba au yatawafanya wafikirie mara mbilimbili kwanza kabla ya kuandika. Zifuatazo ni amri kuu na maelezo yake kwa wote wanaongalia utendaji wangu kwa jicho la husda kuliko ya wale ambao Spika anaomuomba Mungu ailinde nchi hii dhidi yao anapofungua mkutano wa bunge kila asubuhi.

Amri ya kwanza: Mimi ni kiongozi wako niliyeshinda uchaguzi kwa nguvu ya tsunami hivyo hata mkiandika kunidhihaki ni kazi bure. Watanzania wananipenda na wanafahamu usafi wangu na uzalendo wangu. Sijajilimbikizia mali. Hata wale waliokuwa wamenitaja kwenye orodha ya mafisadi, wamegundua walifanya makosa. Kelele zenu ni kama za mwizi ambazo hazimkoseshi mwenye nyumba usingizi. Niliwaahidi kuwatoa wananchi katika umasikini nikijua kabisa haiwezekani kwani nchi hii imeshindikana; nilijua kabisa kwamba umaskini hauwezi kuondoka bila ya watu kuwa na elimu ya kutosha na bila watu kufanya kazi, sasa kama watu hawataki kufanya kazi, basi kila mtu na lwake. Nilikuwa sijaingia ikulu kujionea jinsi ilivyo ngumu kwa mambo kutekelezeka. Unaweza kutoa maagizo na waliopo chini yako wakakataa kutekeleza, sasa utafanya nini hasa kama anayekataa kutekeleza alishiriki katika kampeni za kukupamba ili uingie madarakani. Inabidi unyamaze tu.

Ndugu zetu wafanyabiashara tunajua kabisa unyama wanaofanya ili kujipatia faida kubwa lakini hatuna cha kuwafanya kwa sasa kwa vile walituchangia. Kwa hivyo fedha ambazo zingesaidia kuondoa umasikini haziwezi kutosha mpaka hao jamaa wamalize kurudisha kile walichochanga. Sasa ninayakumbuka maneno ya Mwalimu; alisema wanaochanga, kesho yake wanataka urudishe! Ningelifahamu ujanja huu wa wafanyabiashara, basi ningekataa kabisa michango yao. Na kama nitagombea tena baada ya miaka mitano, nitakataa kabisa michango hii yenye masharti ya kishetani. Namshukuru Mungu, kwa vile nimefumbuka macho na kuuona ukweli. Nitaulinda ukweli huu kwa gharama yoyote ile.

Muache kunikaba kwani hata mkizungumza mpaka midomo iwapasuke sina cha kufanya. Sasa hivi mtindo ni kulalamika tu kuanzia mkubwa hadi mdogo kabisa. Mkulima analalamika mazao yake hayapati bei nzuri, balozi wa nyumba kumikumi anamlalamikia mtendaji, mtendaji anamlalamikia mbunge, mbunge anamlalamikia waziri, waziri anamlalamikia Rais, Rais naye anawalalamikia wote hawa wa chini yake pamoja na wananchi kwa kutotekeleza wajibu wake. Ndipo tulipofikia.

Tumejenga utamaduni wa kulalamika. Sina hakika utamaduni huu utaendelea hadi lini. Badala ya kuchukua hatua, badala ya kuwajibika, tunabaki kulalamika. Sina hakika tunasubiri muujiza gani wa kutuondolea matatizo yetu. Mwaka jana si mlimsikia Waziri wa Fedha akilalamika kwamba makampuni ya simu hayataki kushusha gharama licha ya kupewa vivutio kibao na hivyo njia iliyopo ni kupandisha tu kodi? Na kama kuna wawekezaji wanaotukamua sana ni hawa wenye makampuni ya simu. Ujanja wao ni mwingi. Wanatufumba macho kwa bahati nasibu wanazozichezesha, ambazo ukiangalia zawadi zinazotolewa, zinakuwa zimechangiwa na Watanzania wenyewe. Kutumia ujumbe mfupi wa maneno kuingia kwenye mashindano, ni njia ya kukusanya fedha nyingi kutoka kwa Watanzania. Badala ya kuchukua hatua na kupambana nao, tunabaki kulalamika. Hapo ndio tulipo kila mtu analalamika hivyo muelewe hivyo mkinilalamikia na mimi nawalalamikia.

Amri ya pili:
Msilikebehi bure jina la kiongozi wenu kwani naye si malaika. Hamuoni aliyenitangulia alikuwa akiitwa Bwana Msafi, lakini amemaliza muda wake. Sijuhi kama amebaki na usafi wake. Mimi mwenyewe nilijua usafi wake singeweza kuukaribia lakini angalia aliyoyafanya. Mnadhani mimi nitafanya nini cha ajabu ambacho mtangulizi wangu alishindwa? Nasisitiza zaidi: Msilitaje wala kuandika hovyo jina la mrithi wangu mtarajiwa, ni afadhali hata wakati mwingine mtaje la kwangu, kwa sababu nimeshaingia madarakani na kipindi kijacho nitaendelea kuwako. Mkiendelea na huo utaratibu mlioanza wa kumzodoa, wakati mwanzoni tulikubaliana tusimcharure, mtakuwa mnakiuka makubaliano, halafu mtakuwa mnasababisha vipesa kidogo ambavyo vingeweza hata kujenga visima kadhaa kupunguza adha ya maji, viishie kuandika makala na kuzitangaza kwenye magazeti. Mimi naona ni busara mkamwacha na yeye afikie malengo yake, kama mimi nilivyofikia. Aidha, hali ikiwa mbaya na mkiendelea kutosikiliza, tutawashughulikia wote wenye vidomodomo.

Amri ya tatu:
Waandikeni viongozi wenu vizuri ili muweze kupata nafasi ya kupunguza umasikini wenu binafsi. Baadhi yenu ambao vichwa ni vigumu mtakufa masikini kwa vile mnajitia mnawapenda sana wananchi wote. Ni kweli mnawapenda wanachi? Mkipata madaraka mtafanya tofauti? Acha uongo. Ninyi ambao bado mnajitia vichwa ngumu mtakufa masikini. Kubali kuijenga nchi, ili nayo iwajenge. Toeni michango yenu. Mwalimu Nyerere, alisema: Inawezekana, timiza wajibu wako. Ni lazima kila Mtazania kuwajibika, ni lazima kila Mtanzania kulijenga taifa, kila mtu kwa nafasi yake. Hivyo hii ni amri muhimu sana.

Amri ya nne: Msiwe na wivu na wale ambao nimewapa kazi ili waijenge nchi. Mmekuwa mkipiga kelele kwamba serikali yangu ni kubwa sana kuliko wakati mwingine wowote. Hapa ndio nawashangaa. Mawaziri pamoja na naibu wao wako 60 tu. Kusema ni wengi huku ni kuwaonea. Mawaziri 60 na idadi ya Watanzania ni zaidi ya milioni 35. Wingi wa mawaziri uko wapi? Angalieni kazi wanazozifanya. Baadhi yao ni wachapakazi kweli kweli. Wengine ndio hivyo wanafanana kama Watanzania wengine. Kutowajibika ni jadi ya Mtanzania. Amri hii ni ya kuwataka Watanzania wote kubadilika na kuanza kuwajibika. Kama kuna uwajibikaji baraza la mawaziri 60 ni dogo sana.

Amri ya Tano: Msiwasakame viongozi wastaafu katu. Kuna baadhi ya wadodosoji wameanza mtindo wa kuwasakama viongozi waliopita kwa kuwa walianza miradi ya kuwaondolea umasikini wakiwa ikulu. Wengine bila aibu mnawaita machinga au wachuuzi. Mnataka mimi nifanye nini? Kila mtu anatumia ofisi yake. Hivi hamuoni maafisa wadogo tu wa serikali wana mali nyingi za ajabu ambazo hazielezeki, na sasa mnataka rais yeye afe masikini akishastaafu? Mzigo huu ni mkubwa na una usumbufu mkubwa. Kwa miaka miwili nimegundua jinsi mzigo huu ulivyo mzito. Kumbe ndio maana Mzee Mwinyi, aliuita "Zigo". Haiwezekani afisa yeyote tu akawa na ulaji mkubwa kumshinda rais wa nchi. Najua mtasema Rais ataendelea kutunzwa mpaka afe. Lakini lazima awe na mali za kumtosha si kusubiri takrima ya serikali. Mambo pia yanaweza kubadilika akaja kiongozi mwendawazimu akasema kwamba serikali inatoa fedha nyingi kwa wastaafu akazipunguza. Ikifikia hapo si mstaafu atakufa?

Narudia kwamba kila mmoja ale kwenye ofisi yake na hakuna mabadiliko ya katiba kuruhusu mstaafu ashtakiwe yatakayofanyika leo. Mnataka mje mnishtaki na mimi. Tutaendelea kubaki hivyo, hivyo mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo. Mnapoteza muda wenu kwani hata mkiwasakama wastaafu haisaidii, hakuna mamlaka inayoweza kuwashtaki au kuwafanya lolote, wataendelea kupeta.

Amri ya sita: nilitaka kutoa amri kumi, lakini kwa leo niishie kwa hizi sita. Baada ya miaka mingine miwili, nitatoa amri nyingine tatu. Msitamani maendeleo ya nchi jirani, wala elimu yao wala chochote walicho nacho. Angalieni taifa lenu, jengeni taifa lenu bila kuangalia mataifa mengine. Kuna vijimaneno kwamba sisi licha ya kupata uhuru mapema ukilinganisha na nchi zinazotuzunguka bado tupo nyuma kimaendeleo ukilinganisha na wao. Mbaya zaidi wengine wanasema zile nchi tulizoshiriki kuzikomboa sasa ziko mbele kuliko sisi, pia kuna nchi zilizopigana vita vya wenyewe kwa wenyewe lakini bado wameweza kurudi katika mstari na sasa chumi zao zimepaa. Kielimu ni kwamba jirani zetu wote wametuzidi, hasa elimu ya juu. Nashangaa wengine kusema vita; sisi tuna mtaji mkubwa wa amani, utulivu na mshikamano, tena nisisikie mtu akitulinganisha na waliopigana vita. Amani yetu imesifiwa duniani kote na watu wanakuja kujifunza amani hapa.

Ni lazima twende hatua kwa hatua. Ni muhimu kwanza kujikomboa kifikra. Ni muhimu kuangalia kila kitu kwa jicho la uzalendo.

Mtuache tuendelee na amani na mshikamano wetu ambao wananchi wengi wanaipenda kuliko kitu chochote. Mtanzania akiuliza sifa ya nchi yake, ni lazima atangulize haki na amani. Kenya kuna mashamba makubwa na viwanda vikubwa. Uganda kuna shule na vyuo. Tanzania kuna utulivu na amani. Watu wako radhi kula mlo mmoja tena wakipikia maji machafu au wanayochota kilomita saba lakini waishi kwa amani. Hivyo msipande mbegu mbaya kwa wananchi wakaanza kuchukia amani na mshikamano wao. Watu wetu hawataki kusikia wakuu wao wanapingwa hata kidogo, wale wanaozomea viongozi wanalipwa na makaburu kutoka nje, hata mkiwaambia waandamane hawataki. Wakati mwingine kuna haja ya kuandamana, lakini Watanzania wanajua huku ni kuvunja amani na mshikamano uliotujengea heshima duniani kote. Watanzania wako tayari kupata shida za kila aina, lakini walinde utulivu na amani.

Nimeanza kwa kutoa amri chache za awali na maelezo yake ambayo inabidi wenye vidomodomo wazingatie. Kama mkitaka kuendeleza mapambano ya maneno mtakwama itafika mahali tuwadhibiti. Siku chache zijazo nitatoa amri nyingine hasa baada ya kuona kama mtazingatia haya niliyowaamuru kufanya.
 
Pundamilia07,
You have every right not to be impressed, after all it's satire my good sir, and some people are just not cut out for it! Different strokes for different folks I suppose...
 
Of course. Mwakilishi. In short he is talking about usanii na ushikaji wa JK ktk Gvernment. So long as he is the president he believes in absoluteness. May be dictatorship grains are just about to be sawn. Who knows ? That may be his kast resort.
 
hata nasindwa kuelewa essence ya hii kitu,kwa jinsi ninavyomfahamu huyu mwandishi sidhani kama anaweza kuandika "utumbo" huu,pili huyo JK mwenyewe sidhani kama ana mawazo ya namna hii ingawa ni msanii by nature,whoever wrote this is st**d enough,his brains drowned with Mv. Bukoba and lastly tuacheni mtindo wakutumia majina ya watu kuandika makala za kipuuzi.
 
kuna kitu kinaitwa "jargons" hii ni aina ya lugha ambayo watu wa fani moja huitumia kuwasiliana, mfano lugha ya madaktari, lugha ya wachumi, lugha ya wanafizikia.

Inaelekea mwandishi kwa kuwa ni mtu wa Theolojia, basi kwa kiasi fulani hiyo imechangia kumsukuma kuandika makala kwa mtindo huu.
 
Kwa nyie wenye uelewa mdogo, badala ya kuponda mngejibidisha kutaka kuelewa anazungumzia nini.

Big Up karugendo, A very nice piece of work.
 
Narudia kwamba kila mmoja ale kwenye ofisi yake na hakuna mabadiliko ya katiba kuruhusu mstaafu ashtakiwe yatakayofanyika leo. Mnataka mje mnishtaki na mimi. Tutaendelea kubaki hivyo, hivyo mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo. Mnapoteza muda wenu kwani hata mkiwasakama wastaafu haisaidii, hakuna mamlaka inayoweza kuwashtaki au kuwafanya lolote, wataendelea kupeta.

Ugumu hasa wa kumwajibisha mtangulizi wake unakuja hapa. Kwamba na yeye alikuwa miongoni mwa watendaji wa utawala uliopita, kwa hiyo akimwajibisha mtangulizi wake atakuwa anajiadhibu mwenyewe. Of course hawezi kupitisha sheria ya kuwashataki wastaafu wa nafasi yake, kwani Buzwagi ama Richmondi itamuandama sana.
Mungu Ibariki Tanzania.
 
kuna kitu kinaitwa "jargons" hii ni aina ya lugha ambayo watu wa fani moja huitumia kuwasiliana, mfano lugha ya madaktari, lugha ya wachumi, lugha ya wanafizikia.

Inaelekea mwandishi kwa kuwa ni mtu wa Theolojia, basi kwa kiasi fulani hiyo imechangia kumsukuma kuandika makala kwa mtindo huu.

It is senseless. Haihitaji kwenda shule kujua kama ni makala ya ovyo. It is time lazima tuseme kama mtu ameandika utumbo ambiwe.
 
Mbona yana make sense?
nadhani kuna ujumbe zaidi ya hapo aliouandika na kama kuna mtu alifuatilia kwa makini ile hotuba basi ataelewa kilichododoswa pale. Nadhani ni hotuba iliyowakatisha tamaa watanzania wanaopenda maendeleo. Kuna maneno mengi ya kujikosha na hoja ngumu zilijibiwa kwa dhihaka hivyo naamini kuwa labda imetumika mbinu hiyo kuwahadaa wabongo lakini mwenye akili na afahamu. la sivyo wabongo mmeumia.zile zama za proppaganda zimepita and hakika ukweli hufukuza uongo.
 
It is senseless. Haihitaji kwenda shule kujua kama ni makala ya ovyo. It is time lazima tuseme kama mtu ameandika utumbo ambiwe

Kinachotatiza hapa ni ujumbe au mtindo?. Si unajua tena unapotumia fasihi andishi kuwasilisha ujumbe kuna kufanikiwa na kutokufanikiwa kwa mwandishi. je mwandishi kafanikiwa/hakufanikiwa kivipi?
 
...hiyo ndio halisi ya hii serikali,wengine mtatetea ufisadi tuu na kufa na njaa zenu
 
na padri privatus karugendo

Baada ya kuona kwamba si wote wanaoimba yale yanayompendeza kama alivyotarajia, sasa mkubwa ameamua kutoa amri na maelezo ambayo kwayo yatawakatisha tamaa wanaomkaba au yatawafanya wafikirie mara mbilimbili kwanza kabla ya kuandika. Zifuatazo ni amri kuu na maelezo yake kwa wote wanaongalia utendaji wangu kwa jicho la husda kuliko ya wale ambao Spika anaomuomba Mungu ailinde nchi hii dhidi yao anapofungua mkutano wa bunge kila asubuhi.

1. Amri ya kwanza: Mimi ni kiongozi wako niliyeshinda uchaguzi kwa nguvu ya tsunami hivyo hata mkiandika kunidhihaki ni kazi bure. Watanzania wananipenda na wanafahamu usafi wangu na uzalendo wangu. Sijajilimbikizia mali. Hata wale waliokuwa wamenitaja kwenye orodha ya mafisadi, wamegundua walifanya makosa. Kelele zenu ni kama za mwizi ambazo hazimkoseshi mwenye nyumba usingizi. Niliwaahidi kuwatoa wananchi katika umasikini nikijua kabisa haiwezekani kwani nchi hii imeshindikana; nilijua kabisa kwamba umaskini hauwezi kuondoka bila ya watu kuwa na elimu ya kutosha na bila watu kufanya kazi, sasa kama watu hawataki kufanya kazi, basi kila mtu na lwake. Nilikuwa sijaingia ikulu kujionea jinsi ilivyo ngumu kwa mambo kutekelezeka. Unaweza kutoa maagizo na waliopo chini yako wakakataa kutekeleza, sasa utafanya nini hasa kama anayekataa kutekeleza alishiriki katika kampeni za kukupamba ili uingie madarakani. Inabidi unyamaze tu.

Ndugu zetu wafanyabiashara tunajua kabisa unyama wanaofanya ili kujipatia faida kubwa lakini hatuna cha kuwafanya kwa sasa kwa vile walituchangia. Kwa hivyo fedha ambazo zingesaidia kuondoa umasikini haziwezi kutosha mpaka hao jamaa wamalize kurudisha kile walichochanga. Sasa ninayakumbuka maneno ya Mwalimu; alisema wanaochanga, kesho yake wanataka urudishe! Ningelifahamu ujanja huu wa wafanyabiashara, basi ningekataa kabisa michango yao. Na kama nitagombea tena baada ya miaka mitano, nitakataa kabisa michango hii yenye masharti ya kishetani. Namshukuru Mungu, kwa vile nimefumbuka macho na kuuona ukweli. Nitaulinda ukweli huu kwa gharama yoyote ile.

Muache kunikaba kwani hata mkizungumza mpaka midomo iwapasuke sina cha kufanya. Sasa hivi mtindo ni kulalamika tu kuanzia mkubwa hadi mdogo kabisa. Mkulima analalamika mazao yake hayapati bei nzuri, balozi wa nyumba kumikumi anamlalamikia mtendaji, mtendaji anamlalamikia mbunge, mbunge anamlalamikia waziri, waziri anamlalamikia Rais, Rais naye anawalalamikia wote hawa wa chini yake pamoja na wananchi kwa kutotekeleza wajibu wake. Ndipo tulipofikia.

Tumejenga utamaduni wa kulalamika. Sina hakika utamaduni huu utaendelea hadi lini. Badala ya kuchukua hatua, badala ya kuwajibika, tunabaki kulalamika. Sina hakika tunasubiri muujiza gani wa kutuondolea matatizo yetu. Mwaka jana si mlimsikia Waziri wa Fedha akilalamika kwamba makampuni ya simu hayataki kushusha gharama licha ya kupewa vivutio kibao na hivyo njia iliyopo ni kupandisha tu kodi? Na kama kuna wawekezaji wanaotukamua sana ni hawa wenye makampuni ya simu. Ujanja wao ni mwingi. Wanatufumba macho kwa bahati nasibu wanazozichezesha, ambazo ukiangalia zawadi zinazotolewa, zinakuwa zimechangiwa na Watanzania wenyewe. Kutumia Ujumbe mfupi wa maneno kuingia kwenye mashindano, ni njia ya kukusanya fedha nyingi kutoka kwa Watanzania. Badala ya kuchukua hatua na kupambana nao, tunabaki kulalamika. hapo ndio tulipo kila mtu analalamika hivyo muelewe hivyo mkinilalamikia na mimi nawalalamikia.

2. Amri ya pili: Msilikebehi bure jina la kiongozi wenu kwani naye si malaika. Hamuoni aliyenitangulia alikuwa akiitwa bwana msafi lakini amemaliza muda wake sijuhi kama amebaki na usafi wake. Mimi mwenyewe nilijua usafi wake singeweza kuukaribia lakini angalia aliyoyafanya. Mnadhani mimi nitafanya nini cha ajabu ambacho mtangulizi wangu alishindwa. Nasisitiza zaidi: msilitaje wala kuandika hovyo jina la mrithi wangu mtarajiwa, ni afadhali hata wakati mwingine mtaje la kwangu kwa sababu nimeshaingia madarakani na kipindi kijacho nitaendelea kuwako. Mkiendelea na huo utaratibu mlioanza wa kumzodoa wakati mwanzoni tulikubaliana tusimcharure mtakuwa mnakiuka makubaliano halafu mtakuwa mnasababisha vipesa kidogo ambavyo vingeweza hata kujenga visima kadhaa kupunguza adha ya maji viishie kuandika makala na kuzitangaza kwenye magazeti. Mimi naona ni busara mkamwacha na yeye afikie malengo yake kama mimi nilivyofikia. Aidha hali ikiwa mbaya na mkiendelea kutosikiliza tutawashughulikia wote wenye vidomodomo.

3. Amri ya tatu: Waandikeni viongozi wenu vizuri ili muweze kupata nafasi ya kupunguza umasikini wenu binafsi. Baadhi yenu ambao vichwa ni vigumu mtakufa masikini kwa vile mnajitia mnawapenda sana wananchi wote. Ni kweli mnawapenda wanachi? Mkipata madaraka mtafanya tofauti? Acha uongo. Ninyi ambao bado mnajitia vichwa ngumu mtakufa masikini. Kubali kuijenga nchi, ili nayo iwajenge. Toeni michango yenu. Mwalimu Nyerere, alisema: Inawezekana, timiza wajibu wako. Ni lazima kila Mtazania kuwajibika, ni lazima kila Mtanzania kulijenga taifa, kila mtu kwa nafasi yake. Hivyo hii ni amri muhimu sana.

4. Amri ya Nne: Msiwe na wivu na wale ambao nimewapa kazi ili waijenge nchi. Mmekuwa mkipiga kelele kwamba serikali yangu ni kubwa sana kuliko wakati mwingine wowote. Hapa ndio nawashangaa. Mawaziri pamoja na naibu wao wako 60 tu. Kusema ni wengi huku ni kuwaonea. Mawaziri 60 na idadi ya Watanzania ni zaidi ya milioni 35. Wingi wa mawaziri uko wapi? Angalieni kazi wanazozifanya. Baadhi yao ni wachapakazi kweli kweli. Wengine ndio hivyo wanafanana kama Watanzania wengine. Kutowajibika ni jadi ya Mtanzania. Amri hii ni ya kuwataka Watanzania wote kubadilika na kuanza kuwajibika. Kama kuna uwajibikaji baraza la mawaziri 60 ni dogo sana.

5. Amri ya Tano: Msiwasakame viongozi wastaafu katu. Kuna baadhi ya wadodosoji wameanza mtindo wa kuwasakama viongozi waliopita kwa kuwa walianza miradi ya kuwaondolea umasikini wakiwa ikulu. Wengine bila aibu mnawaita machinga au wachuuzi. Mnataka mimi nifanye nini? Kila mtu anatumia ofisi yake. Hivi hamuoni maafisa wadogo tu wa serikali wana mali nyingi za ajabu ambazo hazielezeki, na sasa mnataka rais yeye afe masikini akishastaafu? Mzigo huu ni mkubwa na una usumbufu mkubwa. Kwa miaka miwili nimegundua jinsi mzigo huu ulivyo mzito. Kumbe ndio maana Mzee Mwinyi, aliuita “Zigo”. Haiwezekani afisa yeyote tu akawa na ulaji mkubwa kumshinda rais wa nchi. Najua mtasema Rais ataendelea kutunzwa mpaka afe. Lakini lazima awe na mali za kumtosha si kusubiri takrima ya serikali. Mambo pia yanaweza kubadilika akaja kiongozi mwendawazimu akasema kwamba serikali inatoa fedha nyingi kwa wastaafu akazipunguza. Ikifikia hapo si mstaafu atakufa?

Narudia kwamba kila mmoja ale kwenye ofisi yake na hakuna mabadiliko ya katiba kuruhusu mstaafu ashtakiwe yatakayofanyika leo. Mnataka mje mnishtaki na mimi. Tutaendelea kubaki hivyo, hivyo mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo. Mnapoteza muda wenu kwani hata mkiwasakama wastaafu haisaidii, hakuna mamlaka inayoweza kuwashtaki au kuwafanya lolote, wataendelea kupeta.

6. Amri ya Sita: Nilitaka kutoa amri kumi, lakini kwa leo niishie kwa hizi sita. Baada ya miaka mingine miwili, nitatoa amri nyingine tatu. Msitamani maendeleo ya nchi jirani, wala elimu yao wala chochote walicho nacho. Angalieni taifa lenu, jengeni taifa lenu bila kuangalia mataifa mengine. Kuna vijimaneno kwamba sisi licha ya kupata Uhuru mapema ukilinganisha na nchi zinazotuzunguka bado tupo nyuma kimaendeleo ukilinganisha na wao. Mbaya zaidi wengine wanasema zile nchi tulizoshiriki kuzikomboa sasa ziko mbele kuliko sisi, pia kuna nchi zilizopigana vita vya wenyewe kwa wenyewe lakini bado wameweza kurudi katika mstari na sasa chumi zao zimepaa. Kielimu ni kwamba jirani zetu wote wametuzidi, hasa elimu ya juu. Nashangaa wengine kusema vita; sisi tuna mtaji mkubwa wa amani, utulivu na mshikamano, tena nisisikie mtu akitulinganisha na waliopigana vita. Amani yetu imesifiwa duniani kote na watu wanakuja kujifunza amani hapa.

Ni lazima twende hatua kwa hatua. Ni muhimu kwanza kujikomboa kifikra. Ni muhimu kuangala kila kitu kwa jicho la uzalendo.

Mtuache tuendelee na amani na mshikamano wetu ambao wananchi wengi wanaipenda kuliko kitu chochote. Mtanzania akiuliza sifa ya nchi yake, ni lazima atangulize haki na amani. Kenya kuna mashamba makubwa na viwanda vikubwa. Uganda kuna shule na vyuo. Tanzania kuna utulivu na amani. Watu wako radhi wale mlo mmoja tena wakipikia maji machafu au wanayochota kilomita saba lakini waishi kwa amani. Hivyo msipande mbegu mbaya kwa wananchi wakaanza kuchukia amani na mshikamano wao. Watu wetu hawataki kusikia wakuu wao wanapingwa hata kidogo, wale wanaozomea viongozi wanalipwa na makaburu kutoka nje, hata mkiwaambia waandamane hawataki. Wakati mwingine kuna haja ya kuaandamna, lakini Watanzania wanajua huku ni kuvunja amani na mshikamano uliotujengea heshima duniani kote. Watanzania wako tayari kupata shida za kila aina, lakini walinde utulivu na amani.

Nimeanza kwa kutoa amri chache za awali na maelezo yake ambayo inabidi wenye vidomodomo wazingatie. Kama mkitaka kuendeleza mapambano ya maneno mtakwama itafika mahali tuwadhibiti. Siku chache zijazo nitatoa amri nyingine hasa baada ya kuona kama mtazingatia haya niliyowaamuru kufanya

Heehe jamani

Hata Padri Karugendo aliyekuwa anamshabikia Kikwete amemgeuka na kumuona msanii na sasa anaandika kumdhihaki! Ama kweli handsome wetu ana hali mbaya

Asha
 
Rare and yet down-to-earth nuggets of political wisdom from someone with a sensible and reflected mind. More power to Padiri Karugendo!
 
Back
Top Bottom