Maelezo muhimu kuhusu majini!

Mi nilikuwa naona una upeo kiasi kumbe waquote pumba mpo wengi siku hadi siku
 
Ndio akili yako imekutuma hivyo na upeo wako umeishia hapo sasa wewe amini unga wa sembe na mwingine akiamini unga wa ngano kila mtu na maisha yake acha kupotosha watu kwa kuamini unavyoamini wewe unavyomuona mwenzio kapotoka ndio na yeye anavyokuona wewe umepotoka kiasi gani.
Si ajabu kwa kichaa kumuona mwenye akili ni kichaa na yeye ni mzima
 
Mi nilikuwa naona una upeo kiasi kumbe waquote pumba mpo wengi siku hadi siku
We ndo mweupe ungekuwa unayo elimu kuhusu ulimwengu usioonekana,ungejua nani yupo nyuma ya hitter, Iddi Amin, Bokasa
 
Noma sana!
 
Nyuma ya KILA dikteta ipo nguvu ya shetani nyuma yake, kwa makubaliano ya damu na madaraka.
 
Ukitaka kuyaona majini, mapepo mengi yanaonyeshwa kwenye katuni za watoto, katuni nyingi za watoto ni picha halisi za majini yanayooneka katika ulimwengu usioonekana. Mfano katuni ya Monster University. Watengenezaji wa katuni wanajua wanachokipandikiza kwa watoto, maana watoto ndio walengwa wakuu kama Jamii ijayo. Hivyo ni lazima wapande wa watakacho.

 
Hahaha [emoji23] mi sijui
 
Hahaha [emoji23] mi sijui
Ukiingia kwenye ulimwengu wa giza utaona nani waliokuwa nyuma yao, Hittler alikuwa anabadilika sura hata zumarid anabadilika sura pindi yule aliye nyuma yake akimvaa na kutamka maneno ya kufuru.
Hittler akisisitiza jambo baada ya ile roho au yule mtu wa nyuma yake kumvaa mwilini na kutamka ule ujasiri.
 
Elimu ya falaki inabeba nini na nini
Duu [emoji3], ni elimu pana sana na inavitu vingi lakini kwa uchache ni elimu ya giza kuhusu majini na utendaji wao katika ulimwengu wa roho, lakini pia ndani yake kuna elimu ya nyota, ila sio hizo za angani, maana kuna aina 12 tu za binadamu duniani na hii ni kwa sababu ya nyota zao, lakini pia elimu ya maumbo na mambo mengine kama haya, kugeuka roho nk, inshort ni elimu pana sana na ni wachache walio hata na masters yake mfano mzuri ni huyo sheikh uliyenitajia inbox maana yeye ndio alikuwa mkufunzi mkuu kwenye hio idara, na yeyote aliyepita pale chuoni lazima atakuwa anamjua hata kwa kusikia tu, nashangaa hata na wewe umemjuaje au umepita pale nini [emoji3], wengi wao ni beginners au wanayo ya kawaida sana wamejifunza ila sio darasani labda kwa kusikia kama humu jf, au kwa watu wao wa karibu.
 
Huyu siku hizi ni mtumishi wa Mungu alitaka kuuliwa na majini salama yake akakimbilia kanisani akaacha uislamu na kuokoka.Amejaa youtube anafundisha kuhusu Yesu Kristo na sio shetani,ameeleza historia yake episode kuanzia alipozaliwa pangani Tanga, kuwa mchawi , mganga hadi alivyomuua Mwalimu wake kwa uchawi shehe Mwaimu na hadi alivyotekwa na alshababu na akatoroka somalia, alipata bilioni moja kwenye Kazi ya uganga akaenda zitumbua dubai na Miami beach USA aliporudi akataka kuacha uganga majini yakapanga kumuua akaamua kukoka. Pia ndie aliyeshiriki tambiko la mwaka 1990 mkoani lindi anazijua siri zote za nchi kuhusu ulimwengu wa giza, yakiwemo mambo ya Mwenge nk. Mtafute YouTube jina Shehe Omari Mnyeshani utapata episode zake mamia kwa mamia akizungumza kuhusu mambo mbalimbali kuhusu dini.
Unamjua Katekela chief wa wageregere Huyu nae alifundishwa falaki na huyu, sasa hivi wote wamemgeuka shetani wanamuhibiri Kristo.
 
Hakuna haja ya makasiriko ndugu yangu, tunachofanya hapa ni kutoa katika elimu zetu tulizonazo kuwapa wale wasiojua mambo haya, sasa shida inakuja pale wenye elimu moja kupingana kwenye maeneo fulani huku mmoja akinadi elimu ya mwenzake ni changa tena sana [emoji16] kuhusu hayo maswala, anyway wanasema za kuambiwa changanya na zako [emoji3], nafikiri mahakimu wazuri ni wasomaji na wauliza maswali ili kupima ufahamu wa kila mmoja.

Labda nikuambie kitu usichojua Messiah, Masiha, masihi ni neno lenye asili ya kiebrania maana yake ni mpakwa mafuta au unaweza kusema (anointed one) tafsiri yake ya kigiriki ndio Kristo au Old Latin Kristus na wapakwa mafuta katika maandiko (maana tunamzungumzia Yesu) walikuwa ni wafalme, Manabii na Makuhani kwa hiyo unaposema Kristo unakuwa too general ni yupi unamaanisha na ndio maana ili ku specify, mfano lazima useme Yesu Kristo, Kwa hiyo Yesu ndio jina lake specific na Masihi au Kristo au Kristu ni Sifa yake maana Kristo waliku wengi na ni wengi hata sasa maana wote waliopakwa mafuta ya Roho wake wanaitwa masihi Wake.
Na kuhusu kwanini iwe jesus wengine waite Yesu wengine Yeshua hayo ni matamshi tu kulingana na lugha lakini kinachomaanishwa ni kitu kile kileo. Mfano kwani Tanzania hakuna watu wanaitwa Omar, haya niambie katika kiarabu kuna irabu "O" au neno Sheikh katika kiarabu kuna "e" Kwanini watamke kitu ambacho hakipo ni kwa sababu ya lugha tuanayoitumia na nature ya matamshi yake lakini kinachomaanishwa ni kilekile kama jina la asili la kiarabu.

Lakini kuhusu malaika, haimanishi malaika kumuasi Mungu ni kwa sababu ni mdhaifu, kwani wanadamu wanapoasi kwa kufanya dhambi inamaasha aliyewaumba ni mdhaifu?. Iko hivyo kwa sababu Mungu aliwaumba wakiwa na free will of choice kama ulivyo wewe na mimi na ndio wakaweza kuchagua njia yao ya giza, lakini haimanishi hakuweza kuwaumba kama Robots wafuate tu maelekezo yake, Maana asili ya Mungu ni mwenye upendo hufurahia zaidi na huridhika na huduma au ibada ya hiari kuliko ya lazima, na hata kama angetaka iwe hivyo ingewezekana bado,kama mwanadamu tu anaweza kumtengeneza mwanadamu mwenzie(msukule au limbwata) na kumtumikisha anavyotaka unafikiri kwa Mungu aliyeumba vyote hilo ni swala dogo kiasi gani lakini ni kinyume cha asili yake.

Source: Elimu changa.[emoji16]

#Zakuambiwachanganyanazako.
 
Duu basi Mwisho umekaribia sana hadi Magwiji wa falaki wanakimbilia chenye nguvu, sisi wanafunzi ni kina nani sasa hata tuache [emoji16]. Kama ni kweli nimefurahi sana, maana jamaa kwa elimu ya dini aliyokuwa nayo sikutegemea kama angekuja kuacha Imani yake.
 
Zaidi ya miaka 25 alishatoka huko.Walishafika level ya chief satanism wakaamua kutoka lakini sio rahisi still wanawindwa.
Wao waliamini shetani ana nguvu kuliko Mungu. Katika harakati zao za giza shetani alishindw waokoa dhidi ya Mapigo ya Mungu wakamua kumuacha shetani na kumgeukia Mungu. Leo wanatoa siri za giza.
 
Huwaga tunayakemea tu. Kwa jina la Yesu, toka na yana tii. Tunayaambia, kaa chini, simama na ondoka kwa Jina la Yesu na yanatii.
 
Umetoa Elimu mujarabu kabisa. Hongera mtumishi. Mbona ipo wazi. "Yaheshua" kwa kiebrania ikimaanisha "Yehova is my salvation" ndio Yesu kwa kiswahili. Yeye ndiye mwana wa mmiliki na ndiye mtu mkubwa na mwenye nguvu kuliko watu wote waliowahi kuishi duniani.

Huyo mganga anawatisha vijana tu humu kwa kueleza hao viumbe dhaifu na vinavyosubiri kuhukumiwa tu.
 
Mzee naona unaingia na kutoka tu. Kuna sehemu unaenda vizuri lakini sehemu nyingine unachanganya haki na batili yaani unakataza dhambi kwa mgongo wa dhambi nyingine.

Umeongelea mambo ya midoli hapa; haya makitu kwenye uislamu ni haramu lakini naona wewe unashauri tu watu wasichome pini badala ya kuwaambia kabisa wasiwe na midoli kwenye nyumba zao maana ni haramu. Maana yake unashauri watu waweke midoli/vinyago ndani ila wasivichome pini tu! Sub-hanallah!

Ukaongelea swala la mbwa na paka; mbwa ni miongoni mwa zile najisi kubwa mbili (yaani mbwa na nguruwe ni levo moja ya najisi) lakini hapa naona unashauri watu wakijiwa na mbwa wasijali wala nini watulie tena wasome na Quran kabisa (halafu na neno ulilotumia sio zuri kwasababu mamlaka ya ulinzi kwa viumbe ni ya Allah peke yake )

Kuna mengi tu humo nimeona unakwenda tofauti (mfano dua ya wakati wa kujitazama kwa kioo hiyo uliyoweka hapo siyo yenyewe) ila kwa leo ngoja niishie hapo kwanza
 
Lakini pia niwaombe ndugu zangu tumtafute Mungu wa kweli maana yupo na anapatikana, lengo langu si kuwafundisha watu falakhi kama wanavyofanya wengine ila ni kuonesha ubaya wa haya mambo na udhaifu wake na ni kipi kilicho bora cha kushikamana nacho maana pande zote nazijua, najua udhaifu wa upande fulani na nguvu ya upande fulani. Ingawa najua masikio ya wengi hupenda zaidi kusikila mambo ya gizani kuliko ya nuru yenyikujenga na ndio maana kuna baadhi ya vitu nilikuwa sivisemi makusudi hasa baadhi ya dua maana wapo wakujaribu, wakajaribu yakawakuta ya kuwakuta na lengo sio yakukute ila lengo ni upate hamasa ya kuujua ukweli uondokane na elimu za giza zinazopofusha fahamu ambao wenye ujuzi nazo huzitumia ki maslahi zaidi na sio kwa sababu wanakupenda au kukuhurumia sana nasema hivi kwa sababu najua katika ulimwengu wa kiroho wa giza hakuna kitu kinaitwa upendo au huruma huwa kuna amri kali sana zaidi hata ya jeshini na wafuasi wake ni watii sana kwa uoga na wako makini ili kulinda maisha yao. Upendo huu tunaouona duniani ni sehemu tu ndogo ya upendo wa Mungu aliyekuumba yeye ndio anakuhurumia maana ndiye aliyekuumba na anajua thamani yako, maana uchungu wa mwana aujuaye mzazi, na ndio maana ana rehema ya kusamehe, lakini ule upande mwingine hakuna kitu kinaitwa msamaha au rehema, ila kuna adhabu za kuogofya ambazo hazijali ubinadamu wala hazipo kwa lengo la kukufunza bali kukuumiza au kukuua kabisa.

Mungu anawapenda ndio maana nimepewa nafasi hii ili kuwaeleza habari za upendo wake, kupitia maarifa niliyonayo, maana hakuna mfuga majini atakaye kusaidia sababu anakupenda maana najua kule gizani neno "upendo"huu msamiati hautumiki, Zaidi sana kuna ulaghai uongo na kujificha mazingira ombwe na wengi wanaingia bila ufahamu hata wakija kufahamu tayari wameshanaswa na kwa tahadhari tu ukinaswa kule kutoka ni neema usione naficha baadhi ya vitu maana najua ninaweza kukufundisha ukafanya kama kimzaha ukashikwa na hizo roho, kwa hiyo nakuwa nimekuangamiza baada ya kukusaidia ambalo ndio lengo langu kuu.
Nina mengi ya kusema lakini muda hautoshi, ila Itafute kweli itakuweka huru maana wengi hawasemi mambo kama yalivyo sasa sijui ni kwa maslahi au hawana shule yake. Mwisho kabisa Mungu anakupenda sana na anatamani umfahamu yeye na nguvu zake kuliko unavyotamani kujua mambo ya giza, maana haya yapo kama ushuhuda tu ila lengo ni kumjua yeye sana kuliko chochote maana kwake ndio kuna siri zote za maarifa yaliyodhahiri na yalifichika kwa wenye mwili .

Falaki, elimu ya nyota, elimu ya maumbo, kugeuka roho kutembea bila kuonekana ni vitu vidogo sana katika mamlaka za nuruni kwenye ulimwengu wa roho ndio maana usishangae kwa nini mchawi mpaka awange, atumie dawa hirizi, viungo vya mwili wa binadamu,atoe kafara wengine wanaenda mpaka kuzimu ili wapate nguvu za kufanya mambo yao lakini wanaomjua Mungu wa kweli nguvu zao ni katika vinywa vyao, hakuna tunguli hakuna hirizi hakuna mafuta, sijui maji ya upako,kutuma sijui jini nani wao wanatuma neno la kinywa lilitamkwa kwa imani thabiti na matokeo yake ni dhahiri katika spiritual realm.

Siku nikipata muda nafikiri nitaandaa uzi maalum kuhusu nguvu ya kinywa katika mamlaka za rohoni.
Asanteni [emoji120]

Source: Elimu changa

#Zakuambiwachanganyanazako.
 
Unayafuga????😂😂😂😂😂
 
Kweli Mungu ni mwema, na atamlinda sana maana amebeba siri nzito sana, na maarifa yao ya gizani, ndio maana wanamuwinda hata mimi ningekuwa ndio shetani[emoji23] lazima ningemuwinda mtu potential kama huyu asije akaniharibia kazi, maana mbinu zote anazijua,huenda hata wanasoma Elimu ya falaki chuo cha maarifa kwa sasa watakuwa na habari zake maana kwa Tanzania sijui kama kuna mtu anaweza kulingana nae kwenye falaki, we jiulize kama wanafunzi aliofundisha ni Magwiji je mwalimu atakuwaje[emoji16]? , Nimeona YouTube kumbe hata huyo sijui pastor nani uliemtaja anasema na yeye alikuwa student wake na jamaa anasema yeye alikuwa gwiji east and central Africa .Lakini utashangaa kuna watu humu watakuambia wanajua falaki, muulize kajifunzia wapi au ndio ile ya kurithi au falaki ya JF ya nyuzi za kina fulani [emoji16].

No makasiriko ni maoni yangu tu [emoji16]

Source: Elimu changa [emoji3]

#Zakuambiwachanganyanazako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…