Maduka yote ya dawa nje ya hospitali za Serikali marufuku

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
Maduka yote ya dawa nje ya hospitali za Serikali kuondolewa.

Ni mkakati wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wa kukomesha wizi wa dawa unaofanywa na watumishi wasio waaminifu.

Katibu mkuu Dk. Donald Mmbando amesema tayari wameandaa rasmi rasimu ambayo imeshakamilika wanasubiri Waziri wa Afya atakayeteuliwa aweze kuipitisha.

Adai Serikali pia inatarajia kutoa bei elekezi ya matibabu katika hospitali zote za binafasi ili mwananchi aweze kumudu gharama za matibabu.

Aiagiza MSD kuhakikisha inaweka dawa za kutosha kwenye hospitali wakati wote "naomba iwe mwisho kusikia mgonjwa anaenda kununua dawa nje, eti kisa hospital haina dawa, natamka sitaki kusikia tena'.

Chanzo: Magic Fm

UPDATE:

Mwaka 2022, Serikali imesisitiza kuwa ni marufuku kuwa na duka la dawa ndani ya mita 500 toka hospitalini. Soma Waziri Ummy Mwalimu: Maduka ya dawa nje ya hospitali yaliyo ndani ya mita 500 kuondolewa
 
Haya mambo yalotakiwa kufanyika toka tupate uhuru leo ndio wanamka..nani asiyejua dawa zinazouzwa pharmacy zinatoka ndani ya hospital..
 
...walikuwa wapi siku zote hizo? Muhimbili imezungukwa na pharmacy kibao, imagine kuna private pharmacy ndani ya hospitali kule block ya wazazi..hivi walikuwa wapi siku zote hizo?
 
Utazuiaje biashara halali kwa kuwa iko karibu na hospitali?
Hapo si ndio kwenye wateja!
Utapangaje bei za hospitali private? Huyo ameshapanic anakurupuka.

Wajipange wenyewe wazuie wizi wa madawa kama upo na sio kuingilia biashara halali.
 
Nina imani baadhi ya sehem maduka yapo kwenye maeneo ya watu na si ya serikali na watu wale wameingia mkataba wa muda mrefu. Lakini pia serikali inatakiwa ipambane na watendaji wake si wafanyabiashara. Hii ni anti business na haikubaliki. Muda si mrefu wataondoa petro station karibu na office za serikali, baadae maduka ya stationary. Wahangaike na watendaji wao.
 
wangemkamata mwenye duka akiuza dawa za serikali. ni kichekesho kufikiri kuwa kwa hali ilivyo sasa hospitali ya serikali ya weza kuwa na dawa zote muda wote, ni kichekesho. kwanza hao msd walisha lipwa deni lao?

kuhusu bei elekezi nalo ni jambo la ajabu kidogo. kuna vigezo vya kufikia bei ya kitu. mfano maabara iliyo mtaa wa samora dsm, haiwezi kutoza bei ya kipimo sawa na maabara iliyo yombo dovia dsm.

mh Magufuli angalia watendaji serikalini wasije kutumiwa kukuhujumu. hekima itumike kufikia maamuzi.
 
Utazuiaje biashara halali kwa kuwa iko karibu na hospitali?
Hapo si ndio kwenye wateja!
Utapangaje bei za hospitali private? Huyo ameshapanic anakurupuka.

Wajipange wenyewe wazuie wizi wa madawa kama upo na sio kuingilia biashara halali.

Ni kweli ni biashara halali, ila utoaji wa leseni utabadilishwa. sio kila sehemu unaweza kufanya biashara yoyote.
Kila leseni ina masharti yake, wenda shariti la kutofanya biashara ya madawa katika eneo la mita kazaa karibu na hospitali litaongezwa.
#hapakazitu
 
Astakafilullah umaskini huoooo unagonga hodi kwa sisi wenye maduka[/QUOTE

Binafsi huo mkakati wa kuondoa maduka nje ya hospitali haina mashiko. Suala ni dawa kupatikana ktk hospitali za umma. Mbona huwa tunafuata maduka kwa umbali wowote ule kwa kuwa hospitali za umma hazina dawa.

Nadhani approach nzuri ya kuyaondoa maduka hayo ni kuhakikisha hospitali zinahuduma zote wakati wote. Maduka hayo yataondoka yenyewe baada ya kuwa biashara hailipi. Biashara nje ya hospitali ni biashara halali zilizosajiliwa. Lingekuwa ni tatizo ikiwa dawa za MSD ndizo zinazopatikana kwenye hayo maduka hapo ningeona kuna uhusiano wa kukosekana dawa hospitalini.

Kama nchi tulipanua wigo wa huduma za afya kutolewa na sekta binafsi, kama ilivyo kwenye elimu. Mfano, huwezi kusema shule binafsi zifutwe kwa kuwa shule za serikali zinafelisha wanafunzi. Serikali inatakiwa ku-hit the target na sio kucheza na psychology za umma. Vipi kama maduka hayo yataondolewa halafu dawa zikaendelea kukosekana hospitalini???????? Ni mawazo yangu huru
 
Nina imani baadhi ya sehem maduka yapo kwenye maeneo ya watu na si ya serikali na watu wale wameingia mkataba wa muda mrefu. Lakini pia serikali inatakiwa ipambane na watendaji wake si wafanyabiashara. Hii ni anti business na haikubaliki. Muda si mrefu wataondoa petro station karibu na office za serikali, baadae maduka ya stationary. Wahangaike na watendaji wao.

zipo phamarcy ndani ya eneo la hospital hizo lazima ziondoke, bado zile stationary maeneo ya chuo nazo ziondolewe, mwalimu anakuja na kitini darasani bado anawambia mkatoe copy badala ya chuo kugawa vitabu kwa wanachuo.
 
Astakafilullah umaskini huoooo unagonga hodi kwa sisi wenye maduka[/QUOTE

Binafsi huo mkakati wa kuondoa maduka nje ya hospitali haina mashiko. Suala ni dawa kupatikana ktk hospitali za umma. Mbona huwa tunafuata maduka kwa umbali wowote ule kwa kuwa hospitali za umma hazina dawa.

Nadhani approach nzuri ya kuyaondoa maduka hayo ni kuhakikisha hospitali zinahuduma zote wakati wote. Maduka hayo yataondoka yenyewe baada ya kuwa biashara hailipi. Biashara nje ya hospitali ni biashara halali zilizosajiliwa. Lingekuwa ni tatizo ikiwa dawa za MSD ndizo zinazopatikana kwenye hayo maduka hapo ningeona kuna uhusiano wa kukosekana dawa hospitalini.

Kama nchi tulipanua wigo wa huduma za afya kutolewa na sekta binafsi, kama ilivyo kwenye elimu. Mfano, huwezi kusema shule binafsi zifutwe kwa kuwa shule za serikali zinafelisha wanafunzi. Serikali inatakiwa ku-hit the target na sio kucheza na psychology za umma. Vipi kama maduka hayo yataondolewa halafu dawa zikaendelea kukosekana hospitalini???????? Ni mawazo yangu huru

Ipo haja pia kuweka mfumo wa computer kama wa aghakan au aar kilakitu kiwe online kuanzia mapokezi hadi kutoa dawa na mtandao huo uunganishwe hadi msd.
 
Utazuiaje biashara halali kwa kuwa iko karibu na hospitali?
Hapo si ndio kwenye wateja!
Utapangaje bei za hospitali private? Huyo ameshapanic anakurupuka.

Wajipange wenyewe wazuie wizi wa madawa kama upo na sio kuingilia biashara halali.
Mitz min?fiki kweli aisee. Hivi nyie watu mnataka nini lakini. Tabia ya kupinga kila jambo ni upuuzi uluotukuka. Wakati mwingine mtu akikaa kimya huhesabiwa mwenye busara.
 
Wao waboreshe huduma za afya na dawa zipatikane kwenye hosp za serikali hakuna sababu ya kuwatoa wenye maduka walioko karibu na hosp zao maana kuwepo tu kwa dawa ni njia rahisi ya kuwaondoa naona wameanza tabia kurupushi.
 
Utazuiaje biashara halali kwa kuwa iko karibu na hospitali?
Hapo si ndio kwenye wateja!
Utapangaje bei za hospitali private? Huyo ameshapanic anakurupuka.

Wajipange wenyewe wazuie wizi wa madawa kama upo na sio kuingilia biashara halali.

Na wanapozipiga marufuku, hospitali zenyewe zina dawa??? Si ndio kuuana huku??
 
Mbona majeneza yanauzwa karibu na hospitali.....na wamiliki wa maduka ya majeneza ni wafanyakazi wa hospitali, vp kuhusu hilo
 
Utazuiaje biashara halali kwa kuwa iko karibu na hospitali?
Hapo si ndio kwenye wateja!
Utapangaje bei za hospitali private? Huyo ameshapanic anakurupuka.

Wajipange wenyewe wazuie wizi wa madawa kama upo na sio kuingilia biashara halali.

Mkuu...
Ni jukumu la serikali kuhakikisha inadhibiti mfuniko wa bei ya kilakitu kwa manufaa ya watumiaji au wananchi wenye kipato cha kati/chini.
Pia katika hali ya kawaida haiwezekani kwa kila mwenye hospitali au muuza dawa za binadamu ajipangie bie atakavyo.
Pia kuhusu mipaka au maeneo ya kufanyia biashara, pia ni jukumu la serikali kupanga, kutoa vibali/ ruhusa, au kufuta/kuhamisha biashara yeyote ambayo itathibitika kwamba inaleta madhara, uonevu, unyonyaji nk kwa wananchi wake
 
Back
Top Bottom