Madudu mengine ya IGP Mwema

Madudu mengine ya IGP Mwema

Kassim Awadh

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
884
Reaction score
187
Katika mwendelezo wa ukabila, uswahiba Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Said Ally Mwema amemkumbatia na kuendelea kumwacha katika utumishi Kamishna Msaidizi wa Polisi - ACP Grace Ngassa ambaye kimsingi alistaafu kazi tangu Julai 2012.

Acp Grace Ngassa kwa sasa analiwakilishi Jeshi la Polisi Tanzania katika ulinzi wa amani jimbo la Darfur nchini Sudan, uwakilishi ambao kigezo cha kwanza ni lazima uwe askari polisi uliye katika utumishi. ACP Ngassa ambaye kashalipwa mafao yake ya kustaafu baada ya Katibu mkuu kutoa kibali chake cha kustaafu anatajwa kubebwa na IGP kwa sababu ya kabila lake kuwa moja na Mwema.

Mwema pia kwa misingi ya uswahiba amekuwa akimbeba kamishna msaidizi mwandamizi SACP Zelothe Stephen ambaye yuko katika mkataba kwa mara ya tatu na sasa amempa madaraka ya u-RPC Mtwara.
 
watu wa Majungu, hata cheo cha boss wako unashindwa kukitaja inavyotakiwa
 
mwema mwenyewe muda wake wa kustaafu umepita nadhan ulitakiwa uanzie kumwambia rais hata mwema nae aende nyumban IGP mpya ateuliwe......... tunasali tu asiwe kamuhanda maana tutapata tabu!!
 
Kama kweli Mungu anasikia dua letu hapa Tanzania basi tusingetawaliwa na CCM mpaka leo hii. CCM as chama kimepoteza malengo kwani waliopo madarakani hivi sasa wapo tu kwa ajili ya kulindana na kuharibu nchi.
 
Hivi ni kwanini watumishi wa ngazi za juu wa nchi hii hawataki kustaafu kwa mujibu wa sheria ? Wanaogopa nini ? Walimkosea nani , mbona hawajiamini ?
 
IGP Thobias Andengenye akiingia tu ofisini atawaondoa wote waliobebwa na huyo mpare
 
Katika mwendelezo wa ukabila, uswahiba Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Said Ally Mwema amemkumbatia na kuendelea kumwacha katika utumishi Kamishna Msaidizi wa Polisi - ACP Grace Ngassa ambaye kimsingi alistaafu kazi tangu Julai 2012.

Acp Grace Ngassa kwa sasa analiwakilishi Jeshi la Polisi Tanzania katika ulinzi wa amani jimbo la Darfur nchini Sudan, uwakilishi ambao kigezo cha kwanza ni lazima uwe askari polisi uliye katika utumishi. ACP Ngassa ambaye kashalipwa mafao yake ya kustaafu baada ya Katibu mkuu kutoa kibali chake cha kustaafu anatajwa kubebwa na IGP kwa sababu ya kabila lake kuwa moja na Mwema.

Mwema pia kwa misingi ya uswahiba amekuwa akimbeba kamishna msaidizi mwandamizi SACP Zelothe Stephen ambaye yuko katika mkataba kwa mara ya tatu na sasa amempa madaraka ya u-RPC Mtwara.

Asante kwa kutoa lako la moyoni. Kumpa mkataba wa kazi Zelothe kwangu naona kafanya sawa na inamwongezea credit IGP; kubali usikubali Zelothe ni jembe. Namkumbuka sana akiwa Mwanza watu wa Mwanza walipata usingizi kuliko vipindi vya ma RPC wengine. Zelothe alikuwa anakwenda patrol mwenyewe usiku, nisijue utendaji wake kwa sasa huko Mtwara bado kwangu namwona bado anaweza kutoa mchango wake kwa taifa lake kwa fani yake ya uaskari. Huyo mwanamke mwingine wa Dafur no comment.
 
mwema mwenyewe muda wake wa kustaafu umepita nadhan ulitakiwa uanzie kumwambia rais hata mwema nae aende nyumban IGP mpya ateuliwe......... tunasali tu asiwe kamuhanda maana tutapata tabu!!

kwani ule upanga wa dhahabu wa SADC ameshaurudisha?
 
Asante kwa kutoa lako la moyoni. Kumpa mkataba wa kazi Zelothe kwangu naona kafanya sawa na inamwongezea credit IGP; kubali usikubali Zelothe ni jembe. Namkumbuka sana akiwa Mwanza watu wa Mwanza walipata usingizi kuliko vipindi vya ma RPC wengine. Zelothe alikuwa anakwenda patrol mwenyewe usiku, nisijue utendaji wake kwa sasa huko Mtwara bado kwangu namwona bado anaweza kutoa mchango wake kwa taifa lake kwa fani yake ya uaskari. Huyo mwanamke mwingine wa Dafur no comment.

ni kweli mkuu! Hata alipokuwa hapa R.T.O Mbeya, alikuwa anashinda road na pikipiki muda mwingi kuliko kwenye wheel chair za ofisini!
 
Anayeongeza mkataba wa makamishna si IJP, ni Ikulu. Askari wa chini ndo huruhusiwa na katibu wa wizara, ambaye anapokea mapendekezo toka kwa IJP. Kwa taarifa nilizonazo, naye alitakiwa àstaafu july, J.K aligoma anataka wastaafu pamoja ingawa yeye alitaka àpumzike matusi n shutuma. Nasikia by dec anasepa
 
Asante kwa kutoa lako la moyoni. Kumpa mkataba wa kazi Zelothe kwangu naona kafanya sawa na inamwongezea credit IGP; kubali usikubali Zelothe ni jembe. Namkumbuka sana akiwa Mwanza watu wa Mwanza walipata usingizi kuliko vipindi vya ma RPC wengine. Zelothe alikuwa anakwenda patrol mwenyewe usiku, nisijue utendaji wake kwa sasa huko Mtwara bado kwangu namwona bado anaweza kutoa mchango wake kwa taifa lake kwa fani yake ya uaskari. Huyo mwanamke mwingine wa Dafur no comment.

Ndugu yangu Bishoke nimekuelewa sana lkn kumbuka tunatakiwa na jamii ya utumishi ya kuachiana majukumu. haiwezikani eti mtu amefanya kazi nzuri kiasi kwamba hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi kama huo. hayo ni mambo ya kijinaga na hayana nafasi ktk karne ya sasa. Tuna watumishi wengi ktk jeshi la polisi ambao wakipata nafasi kama hizi watafanya wonders. Kumbuka kabisi kuna watumishi wengi wabovu bado wameajiriwa wakti tuna vijana wazuri ambao wanaweza kufanya hizi kazi. Huyo IGP nafikiri anajua anachokifanya na nafikiri itafika wakti nafsi yake itamsuta. Ni hayo tu bwana Bishoke!!!!
 
mwema mwenyewe muda wake wa kustaafu umepita nadhan ulitakiwa uanzie kumwambia rais hata mwema nae aende nyumban IGP mpya ateuliwe......... tunasali tu asiwe kamuhanda maana tutapata tabu!!

Kamuhanda ni hatari sana na hivi mtoto wa mkulima alishasema tupigwe akiteuliwa huyo bwana tutakufa maana atatupiga kweli huyo,hafai.
 
Upanga Upanga Upanga wa dhahabu thamani milioni mia sita,

Wakuu wa mikoa wanateuliwa wakiwa mabrigedia wa jeshi, wakistaafu wanarudi kuvaa kombati sembuse huyo "poRIzi"?
 
Back
Top Bottom