Madoido ya 'Kobe wetu'

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Kwetu tunaye Kobe. Nimemchunguza nikagundua sifa zake. Amejaliwa gamba, tena gumu kweli kweli. Gamba hili humpa hifadhi lakini zaidi sana humpa uhakika wa usalama anapokuwa amejificha ndani yake. Hata anapotembea kobe huwa salama kwasababu hulivaa gamba lake daima. Anaweza kusema chochote, kufanya chochote na asihofie kudhirika.

Hata hivyo salama ya kobe yaweza kuwa ya muda tu kwasababu ukweli ni kwamba pamoja na gamba lake bado kobe hulazimika kukitoa kichwa na shingo yake nje aweze kutembea. Afanyapo hivyo hawezi kuwa salama. Kobe huyu basi analazimika ama kuwa rafiki wa wengine awe salama atembeapo au kuwa adui wa wengine lakini awe tayari kulipa gharama ya kujificha ndani ya gamba lake siku zote za maisha yake.
 
Utazingirwa na polisi kwa uchochezi.

Utaulizwa huyo kobe ni nani anayetakiwa "kulipa gharama ya kujificha ndani ya gamba lake siku zote za maisha yake?"
 
Back
Top Bottom