Madiwani Ilala wampinga Mkurugenzi juu ya machinga

Madiwani Ilala wampinga Mkurugenzi juu ya machinga

Sidhani kama tunatofautiana ktk hili.

Mimi nimejiuliza tu, kwamba, ilikuwaje hawa watu waanze kupanga biashara ktk maeneo yasiyoruhusiwa kwa shughuli hizo na wakati huohuo mamlaka zinazohusika (serikali) ikiangalia tu hata imefika mahali hawa watu wamejipa uhalali na haki yao ya maeneo hayo?

Jamani serikali ni serikali tu hakuna cha serikali ya wakati ule sijui ilikuwa vile na eti ya sasa iko hivi.

Hapana. Tusiwatafutie excuse ktk hili kwa sababu hakuna nabadiliko yoyote ya sheria. Sheria na taratibu zilizokuwepo wakati ule ndizo hizi ambazo zipo hadi sasa, hazijabadilika!!

Halafu nimesema, pamoja na kwamba makosa yalifanyika kwa pande zote tangu wakati ule kwa maana ya hawa wamachinga kuvamia maeneo yasiyoruhusiwa kufanyia shughuli zao na kwa upande mwingine mamlaka zinazohusika kutozuia kuvunjwa kwa sheria mapema hata sasa tatizo limekuwa kubwa na sugu;

Basi ni kwa nini Baraza la madiwani na Mkurugenzi huyu anayesemwa kuwa ni wa manispaa ya Ilala watofautiane ktk kurekebisha tatizo hili? Hili ndilo tatizo jingine linalotaka kuzalishwa ....... yaani tatizo juu ya tatizo!!

Kwa mwendo huu wa kutunishiana misuli, hawafiki popote na watavurugana tu lazima. Na popote palipo na vurugu, hakuna maendeleo....!!

Narudia tena kusema, kwamba, hawa wote walishakubaliana namna bora ya kutatua tatizo hili, lakini kuna kidudu mtu anataka kuwakoroga kwa sbb anazozijua yeye.

Na bila kupepesa macho, kuna uwezekano mkubwa kidudu mtu huyu akawa si mwingine zaidi ya serikali kuu ya mkoa wa DSM inayoongozwa na CCM kupitia RC Makonda!!

Na kama wataendelea hivi, basi ni wazi watavurugana sana tu to the point ya kusababisha violence hata maumivu kwa baadhi ya watu na kuwachanganya zaidi hao wanaowaongoza - wamachinga!!

Thanks, nadhani uko sahihi....good night, comrade
 
Back
Top Bottom