Hili suala nadhani linaleta mjadala wakati ambapo hakuna ulazima wa mjadala huu...ni kweli wamachinga walikuwepo siku zote, lakini ni kweli pia wapo mitaani kinyume na sheria (au by laws) za jiji...utakumbuka kulikuwa na fukuza fukuza ya hapa na pale, lakini wakifukuzwa walikuwa wanarudi kwa kuwa kulikuwa hakuna dhamira ya kweli kwa viongozi wengi wa awamu ya nyuma...Hata bandarini mambo yalikuwa hivyo hivyo, makontena zaidi ya 2000 hayalipiwi ushuru, meli pia hazilipiwi ushuru, na kadhalika...kwa hiyo mambo mengi yalikuwa yamelala...Kwenye awamu iliyopita kulikuwa pia na bomoabomoa lakini utashi wa kisiasa ulikuwa mdogo...mimi binafsi siamini kuwa hiyo hamisha ya wamachinga ni suala kwamba eti kwa kuwa jiji lina madiwani wengi wa vyama vya upinzani...Kumbuka awamu ya JPM ni ya uzinagatiaji wa sheria, na ndiyo maana kuna 'majipu' yanatumbuliwa...cha kusisitiza hapa ni kuwa maeneo yatengwe ili wafanyabiashara ndogo ndogo wapate eneo la kufanya biashara zao...Haiwezekani mji ukawa kila barabara ni soko, no way...pale msimbazi wamachinga wanapanga bidhaa barabarani...nasikia upo wakati teksi dereva alimgonga kwa bahati mbaya muuza bidhaa ndogo ndogo pale msimbazi na akauawa na wamachinga wenye hasira...mtu huwezi kutoka nyumbani kwako na kwenda kutandaza bidhaa barabarani, ukiambiwa uondoke, unadai upewe eneo la kufanya biashara...mambo hayaendi hivyo, lazima kuwe na mipango na taratibu...mimi masuala haya huwa sihusishi na siasa...wawe ni CCM au CHADEMA au CUF au chama chochote sheria lazima zizingagatiwe...