Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
MADIWANI wa Manispaa ya Ilala wamesikitishwa na maamuzi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ndugu Isaya M. Mngurumi kwa kufanya maamuzi kinyume na maazimio ya baraza la Madiwani la Ilala juu ya wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kwa jina LA maachinga kuondolewa katika ya jiji.
Bwana Mngurumi alitoa tangazo hilo Mei 06, 2016 siku ya ijumaa Mbele ya waandishi wa Habari ofisini kwake alisema mwisho wa wafanyabiashara ndogondogo hao kuondoka kwa hiyari ni 08/05/2016 na kuanzia tarehe 09/05/2016 hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wale wote watakaokaidi.
Akizungumza katika kikao hicho na waandishi wa habari Mkurugenzi alisema kuwa Halmashauri ya Ilala imeainisha maeneo kwa ajili ya shughuli za wafanyabiashara ndogo ndogo ambapo aliyataja maeneo hayo kuwa ni soko la Kigogo Freshi, Soko la Tabata Muslimu, eneo lililopo mkabala na Gereza la Ukonga na soko la Kivule. Machinga hao waliotambuliwa na kuorodheshwa ni kutoka maeneo ya kariakoo, Karume, Buguruni, Ukonga Mombasa, Jangwani, Kibasila, Banana na Gongolamboto ambapo kwa mujibu wa Mkurugenzi idadi yao ni 2961. Hata hivyo Mwenyekiti wa umoja wa machinga wapinga na idadi hiyo na kusema wako 3700.
Maeneo yaliyoainishwa ni kama ifuatavyo soko la tabata Muslimus machinga 1166, soko la kidogo freshi 1500, soko LA kivule 1000 na Ukonga ni 1500 idadi ambayo inasemekana ni kubwa kuliko uwezo wa maeneo yenyewe.
Madiwani wa Manispaa ya Ilala walishutusha na taarifa hizo baada ya kuziona kwenye vyombo vya Habari na kutaka kujua uhalali wa maamuzi hayo ambapo walilazima kuwasiliana na Mstahiki Meya mhe. Charles Kuyeko ambapo naye hakushirikishwa na hakuwa akijua chochote.
Aidha, Madiwani walifikia maamuzi ya kuitisha kikao cha dharura leo tarehe 08/05/2016 chini ya Mstahiki Meya mhe.Kuyeko ambapo madiwanibhao wamepinga agizo la Mkurugenzi kuwaondoa machinga bila ya kutekeleza maazimio ya Baraza la Madiwani la Manispaa ya Ilala. Kikao cha baraza LA Madiwani walikubaliana kuwa mpango wa kuwaondoa machinga utafanywa Mara baada ya kuboresha miundombinu ya masoko watakayo pelekwa machinga. Miundombinu ya vyoo, Maji na usafiri yenye uhakika ni lazima ijengwe kwanza katika maeneo husika ndipo wapelekwe.
Akizungumza katika kikao hicho Diwani wa Tabata mhe. Patrick Assenga alisema ni ukiukwaji wa hali za binadamu kupeleka wafanyabiashara kwenye eneo ambalo halina choo,wala Maji. Lakini pia eneo hilo linauwezo wa kuchukua angalau watu 400 mpaka 600 inashangaza kuona Mkurugenzi kuelekeza watu takribani 1166 katika soko la Muslimu. Mhe. Assenga alienda mbali na kusema kwa maamuzi haya ya Mkurugenzi sisi kama Madiwani tumeanza kuona mashaka na huyu mkurugenzi, aanze kujitafakari.
Naye Mwenyekiti wa umoja wa machinga katika Manispaa ya Ilala ndugu Steve alisema wameshutushwa na maamuzi ya mkurugenzi ya kuwaondoa wao mjini bila kuwashirikisha wakati awali walikubaliana kushirikiana kwa kila jambo katika kufanya mipango ya kuwahamisha.
Katika kikao hicho Diwani kwa Kata ya Kimanga mhe.John Mjema alisema jambo lolote la Manispaa ya Ilala ni lazima baraza la madiwani waazimie kwanza ndiyo mambo yafanyike. Mjema alisema suala la machinga siyo la kiutendaji na Madiwani hawajaagiza hivyo. Maamuzi aliyoyafanya siyo ya Manispaa yetu bali ni maamuzi yake binafsi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala mhe. Kuyeko amesema Msimamizi mkuu wa shughuli zote za Manispaa ya Ilala ni Meya. Inashangaza kuona jambo muhimu kama hilo (machinga) Mkurugenzi analikurupukia kinyume na maamuzi na maelekezo ya baraza LA Madiwani. Mbaya zaidi Mkurugenzi ametoa agizo kupitia vyombo vya Habari bila Mimi (Meya) kujua. Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala aliungana na Madiwani kuwa maamuzi na tangazo la Mkurugenzi ni tangazo lake binafsi na haliwezi kuwa LA Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Sote tunatambua kuwa suala la machinga linachangamoto nyingi na kwa kutambua hivyo, suala hilo Manispaa ya Ilala inashughuliki kwa kushirikiana na viongozi wamachinga ili kuepusha vulumai na fujo wakati wa kuwaondoa machinga.
Mhe. Kuyeko alisema machinga ni watanzania na sisi ndiyo viongozi wao, hivyo basi ili kutatua tatizo hili lazima kwanza tukae nao tujue mahitaji yao na baadae tuboreshe miundombinu ya masoko yote Ilala.
Mhe. Kuyeko amewataka walioagizwa kutekeleza zoezi la kuwaondoa machinga kwa nguvu listishwe mpaka hapo utaratibu utakapofutwa. Sitaki watu wa ilala wageuzwe punda, machinga hawanakosa wala hata yoyote bali utaratibu wa kuwaandalia maeneo yenye tija ni sisi Manispaa, sasa kwa nini tuwaondoe kwa nguvu wakati tunakowapeleka hakuna tija kibiashara?
Kwa mujibu wa maazimio ya kikao cha leo, agizo la Mkurugenzi wa Ilala ndugu Isaya Mngurumi ni batili na haliwezi kutekelezwa. Diwani wa Ukonga mhe. Juma Mwipopo na Diwani wa Kata ya Pugu Mhe. Boniventure wamesema hawana imani na Mkurugenzi hapo tena na ifike wakati sasa aulizwe ni kwa nini anafanya nje ya maagizo ya baraza LA Madiwani.
Imetolewa Leo 08/05/2016
Na Alex Massaba
Katibu wa Meya Manispaa ya Ilala