Madiwani CCM wamkimbia mbunge wa CHADEMA

Madiwani CCM wamkimbia mbunge wa CHADEMA

TIQO

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Posts
13,786
Reaction score
2,104
MADIWANI na viongozi wa mitaa wanaotokana na Chama cha Mapinduzi (CCM), katika manispaa ya Iringa katika tukio la kushangaza, wamemkimbia Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, wakati wa operesheni usafi iliyoanza jana ndani ya manispaa hiyo.

Wakati watu mbalimbali wakijitokeza kushirikiana na mbunge huyo kufanya usafi katika kata ya Kitanzini, hakuna diwani wala kiongozi wa chama hicho aliyejitokeza kushiriki zoezi hilo, licha ya kuagizwa na kupewa taarifa kimaandishi.

Mbali na kumgomea, madiwani na viongozi hao, wanatuhumiwa kuwakataza baadhi ya wakazi wa mitaa hiyo kushiriki katika kampeni hiyo, kwa madai kwamba ingempatia sifa kubwa mbunge huyo anayetoka chama cha upinzani cha CHADEMA.

"Viongozi wetu wa mitaa walipita na kutuonya tusiende kwa sababu kampeni hiyo imeitishwa na mbunge wa upinzani, badala yake tusubiri ile itakayotangazwa na CCM," alisema mkazi mmoja wa kata ya Kitanzini aliyeomba jina lake lisitajwe gazetini.

Madiwani hao hususan wa kata za Kitanzini na Mshindo, pamoja na kuendesha kampeni dhidi ya mbunge, kata zao ndizo zinazoongoza kwa kusheheni uchafu unaofikia takriban tani 100 katika mitaa ya Ubena, Madrasat na Mtunduruni.

Katika kampeni hiyo, ni madiwani wawili tu wa kata ya Mivinjeni, Frank Nyalusi na wa Viti Maalumu Suzan Mgonukulima, wote wa CHADEMA, walioshiriki kikamilifu katika tukio hilo.

Akizungumzia hali hiyo, Diwani wa Kata ya Mivinjeni Frank Nyalusi (CHADEMA) alionyesha masikitiko yake juu ya madiwani wenzake kutoshiriki zoezi la kuiweka manispaa katika hali ya usafi.

"Baada ya kufika hapa nimesikitishwa sana kwa kuwa diwani wa kata hii tunayofanya usafi haonekani, wakati kata yake ndiyo yenye mlundikano mkubwa wa uchafu.

"Kama yeye ni kiongozi wa eneo husika ameshindwa kuudhiti uchafu huu hadi mbunge kuingilia kati, hii ni aibu kwa Taifa.

"Hii inaonyesha wazi kuwa viongozi wa CCM uwezo wao ni mdogo. Mahindi sasa hivi gunia moja ni sh 105,000, wanafunzi wa darasa la kwanza wanatakiwa kuchanga sh 75,000, badala ya wao kujadili mambo haya, wanaangalia mambo ya chama chao tu," alisema Nyalusi.

Diwani wa viti maalumu Suzan Mgonukulima ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Manispaa alisema, kama nchi itakuwa na viongozi kama wale waliosusia kampeni hiyo na kujenga moyo wa ushirikiano, hali ya nchi itafikia pabaya.

Akizungumza katika kampeni hiyo, Mchungaji Msigwa alisema siasa sio uadui na watu wanatakiwa kuwa marafiki katika suala zima la maendeleo ya nchi.

Hata hivyo, Diwani wa Kata ya Kitanzini ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jescar Msambatavanu, alisema asingeweza kushiriki kwa sababu alikuwa katika msiba huko Njombe.

"Niko Njombe msibani tangu jana nimefiwa na bibi yangu, na sasa tunajiandaa kwenda kuzika," alisema Msambatavanu.

Naye Diwani wa Kata ya Mshindo Daudi Albert alipopigiwa simu mara tatu, ili aseme kilichomfanya ashindwe kushiriki, simu yake ilipokelewa na mwanamke aliyedai yupo Makambako.

source;
Madiwani CCM wamkimbia mbunge wa CHADEMA

[TD="bgcolor: #ffffff"]
na Happiness Elias, Iringa
[/TD]
[TD="align: center"][/TD]

 
Hii imeniacha hoi sasa maendeleo ya jimbo yataletwa na nani jamani wana ccm?
 
, Mchungaji Msigwa alisema siasa sio uadui na watu wanatakiwa kuwa marafiki katika suala zima la maendeleo ya nchi.



[TD="bgcolor: #ffffff"]
na Happiness Elias, Iringa


[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"][/TD]

Mpuuzi huyu mzee, kila kukicha anawaporomoshea matusi, kashfa, dharau na kujiona yeye ndiye anajua kila kitu sasa leo ndio amejua kuwa siasa sio uadui? Aanze kwanza kujifunza yeye na kundi la wavutabangi wenzake.
 
Kama kweli wamekwepa tusitegemee ushirikiano baina ya wananchi wakati viongozi hawaonyeshi mfano. Jamani sisi sote ni ndugu...
 
Mpuuzi huyu mzee, kila kukicha anawaporomoshea matusi, kashfa, dharau na kujiona yeye ndiye anajua kila kitu sasa leo ndio amejua kuwa siasa sio uadui? Aanze kwanza kujifunza yeye na kundi la wavutabangi wenzake.

Mkuu upuuzi unatoka wapi wakati mheshimiwa alikuwa anasisitiza usafi wa halmashauri
 
Mkuu upuuzi unatoka wapi wakati mheshimiwa alikuwa anasisitiza usafi wa halmashauri

Hawa ndio wale wale ambao Msigwa huwaambia wameweka elimu zao mifukoni na kufikiri kama watoto wa Darasa la pili!
 
Mpuuzi huyu mzee, kila kukicha anawaporomoshea matusi, kashfa, dharau na kujiona yeye ndiye anajua kila kitu sasa leo ndio amejua kuwa siasa sio uadui? Aanze kwanza kujifunza yeye na kundi la wavutabangi wenzake.

Akili zako zimefanana na hao waliomkimbia Msigwa kwenye kampeni ya usafi.. Vichwa vikubwa ubongo wa ndege..
 
Viongozi wa CCM wamekimbia kwa kuogopa kumpa sifa,lakini ukiangalia vizuri kutokana na kukimbia kwa Madiwani wa CCM inaonyesha udhaifu uliopo CCM katika maendeleo ya jamii.
 
Hiyo ndo ccm halis,wao wanaamini ili uwe mtanzania lazima utoke ccm,nje ya hapo we sio mtanzania. Maendeleo yanaletwa na watu wote bila ya kujali dini zao,vyama vyao wala makabila yao! Binafsi nampongeza mbunge huyo kwa kuwa mzalendo wa taifa lake na jimbo lake, uchafu au usafi hauna chama!
 
Siasa sio uadui nimeipenda hii.Ukiona mtu anaongea kwa namna hii ujue Maji yapo shingoni.Endelea kutukana mkuu kwani unamwogopa nani si ndio mashabiki wako au wamekulisha maneno nini
 
Na ningependa hiyo kampeni iendelee ikiwezekana kila mwezi iwe inafanyika mara moja, wenzetu Rwanda kila mwezio wanafanya usafi kuanzia rais wao hadi mtoto wa shule lakini sisi tunaendeleza propaganda halafu tunategemea maendeleo yatakuja
 
CCM hacheni kujivua ufahamu ili tufanye kazi na kuwaletea watu maendeleo!
 
Kwani tatizo lipo? wewe unashangaa madiwani kumkimbia mh. Msigwa mbona wao walimkimbia mh. Raisi bungeni na Raisi aliendelea na shughuli zake kama kawaida; Msigwa na wenzake na wasafishe watakapoweza wakichoka madiwani wetu watamalizia patakapo bakia; si nyie ndio mlitufundisha kususa sasa kinawaliza kitu gani?

Chama
Gongo la mboto DSM
cc Ritz; Mzee Mwanakijiji
 
Last edited by a moderator:
Mpuuzi huyu mzee, kila kukicha anawaporomoshea matusi, kashfa, dharau na kujiona yeye ndiye anajua kila kitu sasa leo ndio amejua kuwa siasa sio uadui? Aanze kwanza kujifunza yeye na kundi la wavutabangi wenzake.

Si bure u.me.lo.gwa
 
Upinzani unapata kazi sana kufanya shughuli za maendeleo chini ya chama Cha Mapinduzi,CCM wanatumia fedha ya mlipa kodi ila Upinzani mara nyingi hujikuta wametumia hela zao mifukoni kuleta maendeleo eneo husika,ndo maana inawabidi kubuni njia kama zakufanya usafi(ambazo hazina gharama kubwa) etc ili kutimiza tu wajibu wa kutumikia wananchi,
 
Kwani tatizo lipo? wewe unashangaa madiwani kumkimbia mh. Msigwa mbona wao walimkimbia mh. Raisi bungeni na Raisi aliendelea na shughuli zake kama kawaida; Msigwa na wenzake na wasafishe watakapoweza wakichoka madiwani wetu watamalizia patakapo bakia; si nyie ndio mlitufundisha kususa sasa kinawaliza kitu gani?

Chama
Gongo la mboto DSM
cc Ritz; Mzee Mwanakijiji
kwa hiyo mnasusa mpaka kufanya usafi? Ama kweli ccm ni janga kwa tanzania ya leo!
 
Last edited by a moderator:
kwa hiyo mnasusa mpaka kufanya usafi? Ama kweli ccm ni janga kwa tanzania ya leo!

Acha upimbi unataka kusema wakazi wa Iringa hawajui usafi mpaka wafundishwe na Msigwa? Yeye anachotafuta ni picha za magazeti tu hana lolote

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Back
Top Bottom