Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,808
- 6,500
Hili swali nimekuwa nikijiuliza lakini nashindwa kupata jibu/majibu sahihi hasa nikichukulia kuwa walioandika waraka ni Nape Nnauye na January Makamba.
Hii inatokana na kwamba wameandika waraka mrefu halafu wakapata woga hata kutaja jina la mtu anayemtuma au kumkingia kifua anayejiita 'mwanaharakati' Cyprian Musiba. Hii inaonyesha kuwa wanamuogopa huyo mtu au taasisi wanayedai yuko nyuma ya Musiba.
Ukiangalia utagundua kuwa waraka wa Kinana na Makamba umempa umashuhuri'mwanaharakati' Cyprian Musiba kwa sababu hata watu ambao walikuwa wanampuuza kwa sasa inabidi wasikilize anachokisema hata kama ni ‘’pumba’’. Mimi bado ninaamini mengi anayoyasema huwa ni ‘’pumba’’. Machache ndio husema kweli kwa sababu hata saa mbovu kuna muda husema kweli!
Musiba ambaye tulikuwa tunaambiwa TUMPUUZE kwa sasa anaandikiwa waraka na Makatibu wa CCM Wastaafu huku akipewa nguvu ambazo kimantiki hakuwa nazo! Kimantiki, Waraka unatuambia tusimpuuze Musiba!
Musiba wa kabla ya waraka sio huyu Musiba wa sasa ambapo wa sasa akiitisha mkutano na waandishi wa habari, meza inajaa vyombo vya kunasia sauti. Mfano ni juzi alipoitisha mkutano wa waandishi wa habari.
Waraka umesababisha tujue sababu halisi za waraka kupitia audio ya sauti za Nape na Kinana zilizodukuliwa walipokuwa wanasema Rais Magufuli amewasahau baada ya kupata Urais pamoja na kwamba walimsaidia kufika hapo alipofika.
Waraka umesababisha Makamba Jr kufukuzwa Uwaziri na kuna uwezekano hata ubunge akaukosa.
Waraka umesababisha Mzee Mwinyi kusema walichokifanya Makatibu wastaafu ni kitendo cha UTOTO.
Waraka umesababisha Makamba Jr kufuta haraka ujumbe wake wa kumshukuru Rais Magufuli ukionyesha picha akicheka na Mzee Mwinyi baada ya kufukuzwa Uwaziri.
Waraka umesababisha Makamba Jr kupotea kwenye mitandao ya kijamii hasa twitter ambako alikuwa hapitishi siku moja bila kuweka twit au kujibu twit.
Mpaka sasa ninashindwa kuelewa Malengo ya waraka yalikuwa ni nini kwa sababu kwa maoni yangu waandishi na watoa waraka umewapa matokeo hasi!