Madhila ya wanawake

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,728
Reaction score
870,464
Hili jambo ni kongwe mno na linaazia pale kwenye bustani ya Eden ibilisi kupitia nyoka alipomhadaa mwanamke na hatimaye kufanya kinyume na maagizo ya Mungu.Ni tangu pale ndio Madhila ya mwanamke yalianza, kwanza aliambiwa atazaa kwa uchungu hii ni laana ambayo haijawahi kutenguliwa popote. Kisha kwenye Maandiko ya Biblia takatifu kitabu cha methali kuna mstari usemao.

Mwana mpumbavu ni mzigo wa *****. Haishii hapo tu, bali hata katika mahusiano... Ni jambo lisilo la kawaida kukuta mwanamke mmoja kaolewa na wanaume wawili kwa wakati mmoja. Mpaka leo hii kuna jamii za imani fulani zenye misimamo mikali kuhusu wanawake, akikutwa na mimba nje ya ndoa hata kama kabakwa au wakikutwa wawili wanafanya ngono kesi yote humuangukia mwanamke na adhabu yake ni kupigwa mawe mpaka kufa, haya yapo na yanatokea. Tumeshuhudia hata katika maisha haya kuanzia majumbani mwetu, ndugu wa kike tunaishi nao, wafanyakazi wa ndani, mashuleni na hata vyuoni maofisini na hata kupata cheo nk.

Tumeshawahi kusikia degree za chupi, tumeona kwa uwazi kabisa mfumo kandamizi mashuleni, binti anapata mimba bila kutafakari anafukuzwa shule na kupewa majina yote mabaya, huku mtenda akisepa au akipeta mitaani, wengi wameombwa rushwa ya ngono ili wapate upendeleo fulani huko makazini nk. Wengi wamekuwa watumwa wa ngono ili waweze kuishi.

Kwenye mahusiano vipigo na manyanyaso mengine ni vitu vinavyoonekana ni vya kawaida kabisa lakini pamoja na hayo yoote bado wameendelea kutupenda kutujali na kutuhudumia bila vinyongo huku wakiwa ni wepesi wa kusamehe na kuonyesha upendo mkuu namchukulia mwanamke Kama alama ya uwepo wa dunia yenye matumaini furaha na tumaini.Bila wanawake sijui dunia ingekuwaje Mungu aliona mbali sana.
 
I hear that loud, Chief. Despite all their flaws, Women make the world go 'round, it's as simple as that. If all women were to be wiped off the earth, I'd not think twice about joining wherever the hell they go, no questions asked.

Shout-out to all women with genuine hearts.
 
Sijui hata nichangie nini zaidi ya hiki nilichochangia
 
kwenye hilo la mwanamke kupigwa mawe akizini mbona liko wazi sana mkuu?
ni kwamba hilo ni suala la kiushahidi tu. kwa mfano mwanamke ana mimba wakati hana mume jibu lake ni rahisi tu alizini. sasa unataka wakamtafute mtu ambaye ushahidi haupo kuwa ndiye aliyempa mimba?
pili ili mwanamke azini ni lazima atongozwe na akubali kwa maana hiyo bila ridhaa yake zinaa haipo hivyo likitokea suala la kuzini yeye ndiye mwamuzi wa mchezo kwa sababu kama kakataa zinaa haiwezi kutokea.
kwa mfano hata house girl ndani kwako akilala na mume wako kuna mawili ama alitongozwa akakubali au alimtega mume wako achape nzigoo. kwahiyo nani mhusika mkuu wa zinaa hiyo?
wengine mtasema vishawishi na nini lakini bado tatizo liko pale pale kwa sababu ili ushawishiwe lazima uwe unashawishika sasa kama haushawishiki hata hivyo vishawishi haviwezi kufua dafu kwa hiyo ukikubali kushawishika umekubali kuzini engineer wa zinaa hapo ni. nani?
kweli yapo mengine ambayo wanafanyiwa ni ya hovyo sana na mengi yamejificha kwenye kivuli cha dini.
 
Anastahiri kwa kweli... et kaka mshana jr chagua zawadi itakayokufaa

Saidia bila kuhitaji malipo, jitoe kwa ajili ya wengine jifunze kutoa kuliko kupokea kuwa mwema kwa kila mmoja jifunze kusamehe na kuyafanya makosa ya wengine kama funzo kwako.. Hiyo ndio zawadi bora ninayotaka rubii
 
Last edited by a moderator:
" Saidia bila kuhitaji malipo, jitoe kwa ajili ya wengine jifunze kutoa kuliko kupokea kuwa mwema kwa kila mmoja jifunze kusamehe na kuyafanya makosa ya wengine kama funzo kwako.. Hiyo ndio zawadi bora ninayotaka" Natamani binadamu wa leo aishi hivi"
 
Saidia bila kuhitaji malipo, jitoe kwa ajili ya wengine jifunze kutoa kuliko kupokea kuwa mwema kwa kila mmoja jifunze kusamehe na kuyafanya makosa ya wengine kama funzo kwako.. Hiyo ndio zawadi bora ninayotaka rubii

sawa kaka mshana jr Nakuahidi hayo
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…