Simplicity.
JF-Expert Member
- Dec 19, 2013
- 2,636
- 1,664
Nafuatilia kipindi Star TV - mwanasheria anahojiana na mtangazaji kuhush madhara ya ukeketaji, nashangaa kusikia kumbe sheria haikatazi mwanamke mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kukeketwa!
Mie nilizaliwa katika kijiji ambacho ukeketaji ulikuwepo kwa kiwango cha kutosha, na sidhani kama kuna mama mtu mzima hata mmoja alikwepo ambaye hakukeketwa wakati huo, lakini madhara wanayoyataja kwa mfano mwanamke kushindwa/kujifungua kwa operesheni kwa sababu viungo vya uzazi kushindwa kutanuka, sijawahi kushuhudia wala kusikia pale kijijini kwamba kuna mama kajifungua kwa operesheni mida hiyo nikiwa naishi huko! Na cha ajabu watu vijijini unakuta mama amezaa watoto 11, 12, 13 nyakati hizo!
Swala la ukeketaji lipo pia nchi za ulaya, asia hata Marekani, kuna siri gani kuhusu hili swala?
Swali langu ni je, haya madhara yanayosemwa ni ya kweli kwa kiasi hicho? Kama ni ya kweli inakuwaje wamama wa zamani hawakukumbana nayo? Halafu inakuwaje kuna wanawake wanapata matatizo wakati wa kujifungua hadi kufanyiwa operesheni hali hawajakeketwa hasa Dar?
Bado madai kwamba hawana hisia za kimapenzi! Mbona kuna wanawake naowajua wamekeketwa lakini chupi zao wameshika mkononi?