Kwa mtu wa Tanzania kutofahamu Tattoo ni kitu gani, ni kitu cha Kawaida sana .Kwa maana Tattoo wengi tunaziona kwa Watu maarufu ambao wengi wana maisha ya ajabu ajabu kama ya ha Wakina Irene
Lakini mtoa mada na wadau wengine nataka kukwambia kuwa Tattoo ni kitu muhimu sana kwa jamii tena za kiafrika kwani Tattoo ilikuwepo hata kabla ya Ukoloni.
Na Tattoo wakati huo hazikupakwa kama sehemu ya Urembo hapana, na haikuwa kwa ajili ya Watu maarufu pia.
Wakat huo tattoo ilikuwa ni kwa jamii nzima na ilikuwa ni sehemu ya Utamaduni. Kupitia Tattoo watu waliweza kuwasiliana na kupeana Utambulisho kwa mfano Kabila la Wamakonde
Lakini pia ukija huko Amerika hasa kwa Hao Watu weusi Tattoo zilikuwa sehemu ya Harakati za Ukombozi. Kwani ilikuwa kazi ngumu kusimama hadharani na kudai uhuru mbele ya Watu weupe uko Amerika.
Hivyo kupitia Tattoo watu walijichora na kuwalilisha Ujumbe kadri wawezavyo bila watu wengine kujua.
Hivyo ni asilimia kubwa sana ukiwa USA ukikutana na Watu wamechor tattoo watakwambia sababu za kuchora, na sababu zao zinafungamana na historia halisi ya maisha aidha ya mtu mmoja au ya jamii nzima. Na ndio maana huko unakuta mtu kachora Tattoo ya Rosa Park.
Lakini huku kwetu kwa kuwa tunaiga kupitia Video na kuona tu Wanawake wanaovaa vichupi na wanaume ambao ni Wasanii. Hudhani kuwa Tattoo ni kitu cha Starehe na hivyo ni kinyume na Dini zetu wa hapa Afrika.
Hapo hapo kuna mtu ambaye pengine yeye ni Mwislamu bado haelewi Tattoo ni kitu gani wakati huo huo kuna Wanamke kavaa ijabu na bado kapaka Ina. Ambayo kimsingi ni michiro ile ile na rangi ni zile zile. Na ina dhamira sawa na waliochora Tattoo.
[emoji421]️Hoja zangu hizi zinasimama kwa watu wanaoamini kuwa Tattoo ni Dhambi na wale wanadhani Tattoo ni Uhuni pia. Kwani kuna Watu wana Tattoo za Yesu, nao tunawaweka kwenye kundi gani??
Dhambi ya tattoo ni ipi? Kile ulichochora au tabia zako baada ya kuchora?
Leo hii Lil Wayne wa Cash Money akija Tanzania na kutaka kutoa ufadhiri wa ujenzi wa kanisa, kuna watu watamkataza kisa ana Tattoo mwilini?
Ni kweli kuna madhara yake lakini jamii pia lazima ifahami Tattoo ni kitu gani na sio tu kuwa majibu ya Kidini dini bila kujua historia kamili.
View attachment 1322625