Madhara ya maamuzi ya Makanikia kwa Uchumi wa Wananchi Wilaya ya Msalala

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,883
Jana nilikuwa Kata ya Bugarama, Jimbo la Msalala Wilaya ya Kahama. Kata hii inapakana na Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu. Nimeshuhudia Kijiji cha Bugarama kinavyokufa kiuchumi kufuatia kufungwa kwa mgodi baada ya suala la Makanikia. Hii ni sehemu ya Hotuba yangu niliyotoa jana 2/8/2018

Wananchi wa Bugarama, Watanzania

Januari 2017 nilikuwa kata ya Isagehe pale Kahama kuzungumza na Wananchi. Nilizungumzia madini ya dhahabu yanayopatikana hapa kwenu na namna nchi yetu haifaidiki. Nilimsema Rais Magufuli kwanini hachukui hatua kuboresha Sekta ya Madini. Rais alichukua hatua Lakini hatua ambazo hazina maarifa ya kutosha na hivyo kuwa na madhara makubwa. Nchi yetu haijafaidika na utajiri wa madini kwani tumepata kiduchu sana. Tangu mwaka 1997 tulipoanza uchimbaji mkubwa migodi kadhaa imeshafungwa. Resolute Nzega na Tulawaka huko Biharamulo wameshafunga migodi.

Tokea tumeanza kuchimba dhahabu kwa makampuni makubwa ( uchimbaji mkubwa ) mwaka 1997-2018 tumeshauza nje dhahabu yenye thamani ya $22.5bn ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi trilioni 49. Bajeti ya Tanzania ya mwaka huu 2018/19 ni shilingi 32 trilioni. Hivyo utaona kiasi gani tangu mwaka 1997 uchimbaji mkubwa wa Madini ulipoanza nchi yetu imeuza nje. Lakini mauzo hayo nje yanafaidisha nchi?

Kwa Mauzo hayo na matrilioni hayo, Tanzania imepata $980 milioni tu Kama mapato ya kodi na ushuru mbali mbali. Sisi katika nchi licha ya kuuzwa kwa dhahabu zote tumepata trilioni mbili tu kwa miaka yote, chini ya asilimia 4 ya mapato yote ambayo makampuni ya dhahabu yameuza katika migodi yote.

Leo hii nimepita katika barabara ya Kakola kuja Kahama. Hii ni barabara inayounganisha migodi mitatu mikubwa lakini haina hata Lami. Haikuwa na lami kabla ya Uhuru mpaka leo hii ni aibu na uonevu kwa wananchi na ACT Wazalendo tukiwa na madaraka katika nchi hii tutaiita barabara ile ' Barabara ya unyonyaji ' ( Exploitation Road ) kwa kuwa Mali zao zinapitishwa pale lakini wenyewe hawanufaiki. Barabara inayounganisha migodi mikubwa ya dhahabu nchini Geita, Bulyanhulu na Buzwagi haina lami ni aibu kubwa Sana.

Rais alisikia haya. Akachukua hatua. Lakini hatua zake hakutumia busara Katika kuzitekeleza. Hatua zake zimeleta madhara makubwa kwenu. Nimeona mji wenu unavyokufa. Mgodi umefungwa na Wafanyakazi kuondoka hapa Bugarama. Mzunguko wa fedha umeshuka kwa sababu watumiaji wameondoka. Nimeona maduka yamefungwa. Nimeona nyumba za wageni zimefungwa. Biashara zimefungwa.

Wafanyakazi wa Bulyanhulu 6000 walioondolewa kazini walikuwa wanalipwa mishahara kama shilingi 57 bilioni kwa mwaka. Sehemu ya Fedha hii ilikuwa inaingia hapa kijijini kwenye matumizi. Walikuwa walikuwa wanakula hapa. Wanakunywa hapa nk.

Halmashauri yenu ya Msalala nayo imepoteza mapato na hivyo kupoteza uwezo wa kuwahudumia. Kabla ya suala la makanikia Msalala walikuwa wanapata Mapato ya shilingi 4.6 bilioni kwa mwaka. Leo Msalala wanapata 1.8 bilioni tu. Watawezaje kuboresha afya? Elimu? Barabara za mtaa?

Tulimshauri Rais kuwa awe makini na suala la makanikia. Angesubiri tungepata fedha nyingi kama 1.8 trilioni kutoka mauzo ya mgodi na wamiliki wapya tungewapa masharti mapya. Serikali haikusikia ikatuahidi Noah kila Mtanzania. Tukaishia kuambiwa ni Balimi 7 kila Mtanzania ( $300m za kishika uchumba) ambazo nazo hatujapata mpaka leo.
Leo CCM wanaona aibu kuongelea suala la Makanikia hapa Bugarama kwa sababu wanajua wameharibu. Wanajua hayakuwa maamuzi mazuri.

Lazima tufanye mabadiliko ya kweli kwa kuikataa CCM na kujenga upya Uchumi wa nchi yetu na kurudisha Demokrasia yetu.
 
Daaaah hizo habari za makanikia hatutaki kuzisikia kabisa , vijiwe tumeweka pamba maskioni
 
Yatupasa tuvumiliane tu kwa kweli. maana mpaka mwamba ukubali kulainika lazima upatikane moto wa volcano
 
Habari ya makinikia kwa jamii ya leo,ni SASA NA SISTA WA ROMA, KUONA DHAKARI YA MWANAUME, HARAMU TUPU
 
kiongozi ,jiwe anawajua watz wanavyopenda mijadala miepesi hasa matukio isiyo ya msingi,anatujua vizuri tulivyo wasahaulifu wa mambo ya msingi yanayohusu hatima yetu wenyewe na taifa letu.ndio maana haishiwi kubua vioja ,uteuzi na utenguzi imradi tu kamera zisiikose sura yake na awe mjadala kila kona kwa msaada wa vyombo vya habari.anapenda sifa binafsi bila kujali gharama halisi kwa taifa.ndio maana kadhibiti media .kwa sasa mhariri mkuu wa media zote anaishi magogoni,ni sifa tu.wasaidizi wake wanamjua anavyopenda kiki,wanajua kileo chake kikuu ni sifa nao wanaenda na mdundo huo huo,ni kusifia tuu ata upu uzi.
ukitaka cheo cha kuteuliwa wewe mwaga sifa na wachafue wapinzani wake.malilikia alishasema TL kuwa pale ni changa la macho,mapro watz ni wasanii mno.
 
Jana nilikuwa Kata ya Bugarama, Jimbo la Msalala Wilaya ya Kahama. Kata hii inapakana na Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu. Nimeshuhudia Kijiji cha Bugarama kinavyokufa kiuchumi kufuatia kufungwa kwa mgodi baada ya suala la Makanikia. Hii ni sehemu ya Hotuba yangu niliyotoa jana 2/8/2018

Wananchi wa Bugarama, Watanzania

Januari 2017 nilikuwa kata ya Isagehe pale Kahama kuzungumza na Wananchi. Nilizungumzia madini ya dhahabu yanayopatikana hapa kwenu na namna nchi yetu haifaidiki. Nilimsema Rais Magufuli kwanini hachukui hatua kuboresha Sekta ya Madini. Rais alichukua hatua Lakini hatua ambazo hazina maarifa ya kutosha na hivyo kuwa na madhara makubwa. Nchi yetu haijafaidika na utajiri wa madini kwani tumepata kiduchu sana. Tangu mwaka 1997 tulipoanza uchimbaji mkubwa migodi kadhaa imeshafungwa. Resolute Nzega na Tulawaka huko Biharamulo wameshafunga migodi.

Tokea tumeanza kuchimba dhahabu kwa makampuni makubwa ( uchimbaji mkubwa ) mwaka 1997-2018 tumeshauza nje dhahabu yenye thamani ya $22.5bn ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi trilioni 49. Bajeti ya Tanzania ya mwaka huu 2018/19 ni shilingi 32 trilioni. Hivyo utaona kiasi gani tangu mwaka 1997 uchimbaji mkubwa wa Madini ulipoanza nchi yetu imeuza nje. Lakini mauzo hayo nje yanafaidisha nchi?

Kwa Mauzo hayo na matrilioni hayo, Tanzania imepata $980 milioni tu Kama mapato ya kodi na ushuru mbali mbali. Sisi katika nchi licha ya kuuzwa kwa dhahabu zote tumepata trilioni mbili tu kwa miaka yote, chini ya asilimia 4 ya mapato yote ambayo makampuni ya dhahabu yameuza katika migodi yote.

Leo hii nimepita katika barabara ya Kakola kuja Kahama. Hii ni barabara inayounganisha migodi mitatu mikubwa lakini haina hata Lami. Haikuwa na lami kabla ya Uhuru mpaka leo hii ni aibu na uonevu kwa wananchi na ACT Wazalendo tukiwa na madaraka katika nchi hii tutaiita barabara ile ' Barabara ya unyonyaji ' ( Exploitation Road ) kwa kuwa Mali zao zinapitishwa pale lakini wenyewe hawanufaiki. Barabara inayounganisha migodi mikubwa ya dhahabu nchini Geita, Bulyanhulu na Buzwagi haina lami ni aibu kubwa Sana.

Rais alisikia haya. Akachukua hatua. Lakini hatua zake hakutumia busara Katika kuzitekeleza. Hatua zake zimeleta madhara makubwa kwenu. Nimeona mji wenu unavyokufa. Mgodi umefungwa na Wafanyakazi kuondoka hapa Bugarama. Mzunguko wa fedha umeshuka kwa sababu watumiaji wameondoka. Nimeona maduka yamefungwa. Nimeona nyumba za wageni zimefungwa. Biashara zimefungwa.

Wafanyakazi wa Bulyanhulu 6000 walioondolewa kazini walikuwa wanalipwa mishahara kama shilingi 57 bilioni kwa mwaka. Sehemu ya Fedha hii ilikuwa inaingia hapa kijijini kwenye matumizi. Walikuwa walikuwa wanakula hapa. Wanakunywa hapa nk.

Halmashauri yenu ya Msalala nayo imepoteza mapato na hivyo kupoteza uwezo wa kuwahudumia. Kabla ya suala la makanikia Msalala walikuwa wanapata Mapato ya shilingi 4.6 bilioni kwa mwaka. Leo Msalala wanapata 1.8 bilioni tu. Watawezaje kuboresha afya? Elimu? Barabara za mtaa?

Tulimshauri Rais kuwa awe makini na suala la makanikia. Angesubiri tungepata fedha nyingi kama 1.8 trilioni kutoka mauzo ya mgodi na wamiliki wapya tungewapa masharti mapya. Serikali haikusikia ikatuahidi Noah kila Mtanzania. Tukaishia kuambiwa ni Balimi 7 kila Mtanzania ( $300m za kishika uchumba) ambazo nazo hatujapata mpaka leo.
Leo CCM wanaona aibu kuongelea suala la Makanikia hapa Bugarama kwa sababu wanajua wameharibu. Wanajua hayakuwa maamuzi mazuri.

Lazima tufanye mabadiliko ya kweli kwa kuikataa CCM na kujenga upya Uchumi wa nchi yetu na kurudisha Demokrasia yetu.
Migodi hiyo itakapofunguliwa (ama kwa kupata wawekezaji wengine au kwa hawa kukubali masharti) tutapata hizo hela. Tusubiri. Mbona tulisubiri muda mrefu (katika kipindi cha hayati Julius Nyerere) kwa nini sasa tushindwe? Inawezekana tukaja kupata saidi ya hicho kiasi unachosema! Tusubiri!
 
Yaani bado tu anafanya siasa kwenye jimbo la mwingine?

Halafu hakuna point ya maana isipokuwa uchochezi tu. Kwani huo Mgodi wa Bulyanhuru utaendelea milele? Si ungalifungwa kama ulivyofungwa ule wa Nzega baada ya kumaliza kusomba hiyo dhahabu na wananchi wakiachiwa mashimo na umasikini wao? Sasa si afadhali mgodi wa Bulyanhuru umefungwa kabla waporaji hawajamaliza hiyo dhahabu. Umefungwa ukiwa bado una dhahabu. Tukipata mchimbaji atakayekubaliana na masharti yetu ya win-win kwa mjibu wa sheria mpya ya madini, mgodi utafunguliwa na hizo barabara zitawekwa lami. Tukimkosa tutachimba wenyewe hata baada ya miaka 100. Kwani dhahabu huwa inaoza? Mbona enzi za Nyerere na Mwinyi hazikuchimbwa?

Zitto uache hiyo tabia ya kuhamasisha wananchi waichukie serikali yao halali. Kuhamasisha chuki dhidi ya serikali halali wakati wa kipindi ambacho si cha kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu, ni kitendo cha uchochezi/uhaini kwa mjibu wa katiba ya nchi na sheria zake. Kitendo hicho unachofanya kinaruhusiwa tu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu kwa kanuni na utaratibu maalum unaosimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Unapaswa kuyaelewa na kuyazingatia haya badala ya kuendelea kubwabwaja ovyo ovyo kila mahala na kila mara.

Kuwa mbunge hakumaanishi unaruhusiwa kuropoka cho chote unachotaka mahala po pote na wakati wo wote. Hata ndani ya bunge kuna kanuni za kudhibiti uropokaji wa aina hiyo licha ya kwamba kuna bungeni mbunge ana kinga. Nje ya bunge hakuna kinga ya kibunge. Nje ya bunge hakuna tofauti ya mbunge na raia wengine kuhusu uropokaji huo. Nje ya bunge utakamatwa na hatimaye kufikishwa mahakamani na baadaye kufungwa jela. Fanya siasa za kistaarabu. Hayo maneno ya reserve kwa kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu kitakachoanza mwezi August 2020. Wakati huu iache serikali ifanye kazi zake ilizokusudia kuzifanya. Hii ndiyo dhana ya demokrasia, the rule of the majority and not the minority.
 
Apo kwenye barabara nafikiri kuna umuhimu wa kuangalia upya barabara ya kakora kutokea geita tu kahama ..maana hii barabara inaunganisha vijiji vingi napia itakuza movement za watu katika biashara
 
Yaani bado tu anafanya siasa kwenye jimbo la mwingine?

Halafu hakuna point ya maana isipokuwa uchochezi tu. Kwani huo Mgodi wa Bulyanhuru utaendelea milele? Si ungalifungwa kama ulivyofungwa ule wa Nzega baada ya kumaliza kusomba hiyo dhahabu na wananchi wakiachiwa mashimo na umasikini wao? Sasa si afadhali mgodi wa Bulyanhuru umefungwa kabla waporaji hawajamaliza hiyo dhahabu. Umefungwa ukiwa bado una dhahabu. Tukipata mchimbaji atakayekubaliana na masharti yetu ya win-win kwa mjibu wa sheria mpya ya madini, mgodi utafunguliwa na hizo barabara zitawekwa lami. Tukimkosa tutachimba wenyewe hata baada ya miaka 100. Kwani dhahabu huwa inaoza? Mbona enzi za Nyerere na Mwinyi hazikuchimbwa?

Zitto uache hiyo tabia ya kuhamasisha wananchi waichukie serikali yao halali. Kuhamasisha chuki dhidi ya serikali halali wakati wa kipindi ambacho si cha kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu, ni kitendo cha uchochezi/uhaini kwa mjibu wa katiba ya nchi na sheria zake. Kitendo hicho unachofanya kinaruhusiwa tu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu kwa kanuni na utaratibu maalum unaosimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Unapaswa kuyaelewa na kuyazingatia haya badala ya kuendelea kubwabwaja ovyo ovyo kila mahala na kila mara.

Kuwa mbunge hakumaanishi unaruhusiwa kuropoka cho chote unachotaka mahala po pote na wakati wo wote. Hata ndani ya bunge kuna kanuni za kudhibiti uropokaji wa aina hiyo licha ya kwamba kuna bungeni mbunge ana kinga. Nje ya bunge hakuna kinga ya kibunge. Nje ya bunge hakuna tofauti ya mbunge na raia wengine kuhusu uropokaji huo. Nje ya bunge utakamatwa na hatimaye kufikishwa mahakamani na baadaye kufungwa jela. Fanya siasa za kistaarabu. Hayo maneno ya reserve kwa kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu kitakachoanza mwezi August 2020. Wakati huu iache serikali ifanye kazi zake ilizokusudia kuzifanya. Hii ndiyo dhana ya demokrasia, the rule of the majority and not the minority.
Povu la clean soft ili
 
The expoitation road.! Mkuu ZZK hizo Balimi 7 umenitamanisha sana..

Kwanini nyinyi wabunge msimshauri JIWE awe tu mfalme.
 
Zito Kabwe ameshajua Kigoma hawamrudishi hivyo anatafuta Jimbo la kugombea, lkn kwa Kahama umenoa labda jaribu Machame Mbowe akikusaidia!
 
Jana nilikuwa Kata ya Bugarama, Jimbo la Msalala Wilaya ya Kahama. Kata hii inapakana na Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu. Nimeshuhudia Kijiji cha Bugarama kinavyokufa kiuchumi kufuatia kufungwa kwa mgodi baada ya suala la Makanikia. Hii ni sehemu ya Hotuba yangu niliyotoa jana 2/8/2018

Wananchi wa Bugarama, Watanzania

Januari 2017 nilikuwa kata ya Isagehe pale Kahama kuzungumza na Wananchi. Nilizungumzia madini ya dhahabu yanayopatikana hapa kwenu na namna nchi yetu haifaidiki. Nilimsema Rais Magufuli kwanini hachukui hatua kuboresha Sekta ya Madini. Rais alichukua hatua Lakini hatua ambazo hazina maarifa ya kutosha na hivyo kuwa na madhara makubwa. Nchi yetu haijafaidika na utajiri wa madini kwani tumepata kiduchu sana. Tangu mwaka 1997 tulipoanza uchimbaji mkubwa migodi kadhaa imeshafungwa. Resolute Nzega na Tulawaka huko Biharamulo wameshafunga migodi.

Tokea tumeanza kuchimba dhahabu kwa makampuni makubwa ( uchimbaji mkubwa ) mwaka 1997-2018 tumeshauza nje dhahabu yenye thamani ya $22.5bn ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi trilioni 49. Bajeti ya Tanzania ya mwaka huu 2018/19 ni shilingi 32 trilioni. Hivyo utaona kiasi gani tangu mwaka 1997 uchimbaji mkubwa wa Madini ulipoanza nchi yetu imeuza nje. Lakini mauzo hayo nje yanafaidisha nchi?

Kwa Mauzo hayo na matrilioni hayo, Tanzania imepata $980 milioni tu Kama mapato ya kodi na ushuru mbali mbali. Sisi katika nchi licha ya kuuzwa kwa dhahabu zote tumepata trilioni mbili tu kwa miaka yote, chini ya asilimia 4 ya mapato yote ambayo makampuni ya dhahabu yameuza katika migodi yote.

Leo hii nimepita katika barabara ya Kakola kuja Kahama. Hii ni barabara inayounganisha migodi mitatu mikubwa lakini haina hata Lami. Haikuwa na lami kabla ya Uhuru mpaka leo hii ni aibu na uonevu kwa wananchi na ACT Wazalendo tukiwa na madaraka katika nchi hii tutaiita barabara ile ' Barabara ya unyonyaji ' ( Exploitation Road ) kwa kuwa Mali zao zinapitishwa pale lakini wenyewe hawanufaiki. Barabara inayounganisha migodi mikubwa ya dhahabu nchini Geita, Bulyanhulu na Buzwagi haina lami ni aibu kubwa Sana.

Rais alisikia haya. Akachukua hatua. Lakini hatua zake hakutumia busara Katika kuzitekeleza. Hatua zake zimeleta madhara makubwa kwenu. Nimeona mji wenu unavyokufa. Mgodi umefungwa na Wafanyakazi kuondoka hapa Bugarama. Mzunguko wa fedha umeshuka kwa sababu watumiaji wameondoka. Nimeona maduka yamefungwa. Nimeona nyumba za wageni zimefungwa. Biashara zimefungwa.

Wafanyakazi wa Bulyanhulu 6000 walioondolewa kazini walikuwa wanalipwa mishahara kama shilingi 57 bilioni kwa mwaka. Sehemu ya Fedha hii ilikuwa inaingia hapa kijijini kwenye matumizi. Walikuwa walikuwa wanakula hapa. Wanakunywa hapa nk.

Halmashauri yenu ya Msalala nayo imepoteza mapato na hivyo kupoteza uwezo wa kuwahudumia. Kabla ya suala la makanikia Msalala walikuwa wanapata Mapato ya shilingi 4.6 bilioni kwa mwaka. Leo Msalala wanapata 1.8 bilioni tu. Watawezaje kuboresha afya? Elimu? Barabara za mtaa?

Tulimshauri Rais kuwa awe makini na suala la makanikia. Angesubiri tungepata fedha nyingi kama 1.8 trilioni kutoka mauzo ya mgodi na wamiliki wapya tungewapa masharti mapya. Serikali haikusikia ikatuahidi Noah kila Mtanzania. Tukaishia kuambiwa ni Balimi 7 kila Mtanzania ( $300m za kishika uchumba) ambazo nazo hatujapata mpaka leo.
Leo CCM wanaona aibu kuongelea suala la Makanikia hapa Bugarama kwa sababu wanajua wameharibu. Wanajua hayakuwa maamuzi mazuri.

Lazima tufanye mabadiliko ya kweli kwa kuikataa CCM na kujenga upya Uchumi wa nchi yetu na kurudisha Demokrasia yetu.
Na kama hiyo hitoshi na bado Mgodi umetoa MEMO ya kupunguza tena Wafanyakazi wachache waliopo kuanzia trh1 mpk9
 
Na bado tutaumia zaidi! Matokeo ya maamuzi ya kukurupuka ili mtu apate misifa, misifa ya kijinga. Halafu utasikia mtu kutwa kukicha, Mungu hivi, Mungu vile! "Ndugu zangu watanzania tukimtanguliza Mungu...." "watanzania tukimtegemeza Mungu..." "Haya ni maamuzi ya Mungu " ...."Pesa ipo" bla bla tu wakati watu wanaumia kwa sababu ya maamuzi ya ajabu kabisa
 
Back
Top Bottom