Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,884
Jana nilikuwa Kata ya Bugarama, Jimbo la Msalala Wilaya ya Kahama. Kata hii inapakana na Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu. Nimeshuhudia Kijiji cha Bugarama kinavyokufa kiuchumi kufuatia kufungwa kwa mgodi baada ya suala la Makanikia. Hii ni sehemu ya Hotuba yangu niliyotoa jana 2/8/2018
Wananchi wa Bugarama, Watanzania
Januari 2017 nilikuwa kata ya Isagehe pale Kahama kuzungumza na Wananchi. Nilizungumzia madini ya dhahabu yanayopatikana hapa kwenu na namna nchi yetu haifaidiki. Nilimsema Rais Magufuli kwanini hachukui hatua kuboresha Sekta ya Madini. Rais alichukua hatua Lakini hatua ambazo hazina maarifa ya kutosha na hivyo kuwa na madhara makubwa. Nchi yetu haijafaidika na utajiri wa madini kwani tumepata kiduchu sana. Tangu mwaka 1997 tulipoanza uchimbaji mkubwa migodi kadhaa imeshafungwa. Resolute Nzega na Tulawaka huko Biharamulo wameshafunga migodi.
Tokea tumeanza kuchimba dhahabu kwa makampuni makubwa ( uchimbaji mkubwa ) mwaka 1997-2018 tumeshauza nje dhahabu yenye thamani ya $22.5bn ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi trilioni 49. Bajeti ya Tanzania ya mwaka huu 2018/19 ni shilingi 32 trilioni. Hivyo utaona kiasi gani tangu mwaka 1997 uchimbaji mkubwa wa Madini ulipoanza nchi yetu imeuza nje. Lakini mauzo hayo nje yanafaidisha nchi?
Kwa Mauzo hayo na matrilioni hayo, Tanzania imepata $980 milioni tu Kama mapato ya kodi na ushuru mbali mbali. Sisi katika nchi licha ya kuuzwa kwa dhahabu zote tumepata trilioni mbili tu kwa miaka yote, chini ya asilimia 4 ya mapato yote ambayo makampuni ya dhahabu yameuza katika migodi yote.
Leo hii nimepita katika barabara ya Kakola kuja Kahama. Hii ni barabara inayounganisha migodi mitatu mikubwa lakini haina hata Lami. Haikuwa na lami kabla ya Uhuru mpaka leo hii ni aibu na uonevu kwa wananchi na ACT Wazalendo tukiwa na madaraka katika nchi hii tutaiita barabara ile ' Barabara ya unyonyaji ' ( Exploitation Road ) kwa kuwa Mali zao zinapitishwa pale lakini wenyewe hawanufaiki. Barabara inayounganisha migodi mikubwa ya dhahabu nchini Geita, Bulyanhulu na Buzwagi haina lami ni aibu kubwa Sana.
Rais alisikia haya. Akachukua hatua. Lakini hatua zake hakutumia busara Katika kuzitekeleza. Hatua zake zimeleta madhara makubwa kwenu. Nimeona mji wenu unavyokufa. Mgodi umefungwa na Wafanyakazi kuondoka hapa Bugarama. Mzunguko wa fedha umeshuka kwa sababu watumiaji wameondoka. Nimeona maduka yamefungwa. Nimeona nyumba za wageni zimefungwa. Biashara zimefungwa.
Wafanyakazi wa Bulyanhulu 6000 walioondolewa kazini walikuwa wanalipwa mishahara kama shilingi 57 bilioni kwa mwaka. Sehemu ya Fedha hii ilikuwa inaingia hapa kijijini kwenye matumizi. Walikuwa walikuwa wanakula hapa. Wanakunywa hapa nk.
Halmashauri yenu ya Msalala nayo imepoteza mapato na hivyo kupoteza uwezo wa kuwahudumia. Kabla ya suala la makanikia Msalala walikuwa wanapata Mapato ya shilingi 4.6 bilioni kwa mwaka. Leo Msalala wanapata 1.8 bilioni tu. Watawezaje kuboresha afya? Elimu? Barabara za mtaa?
Tulimshauri Rais kuwa awe makini na suala la makanikia. Angesubiri tungepata fedha nyingi kama 1.8 trilioni kutoka mauzo ya mgodi na wamiliki wapya tungewapa masharti mapya. Serikali haikusikia ikatuahidi Noah kila Mtanzania. Tukaishia kuambiwa ni Balimi 7 kila Mtanzania ( $300m za kishika uchumba) ambazo nazo hatujapata mpaka leo.
Leo CCM wanaona aibu kuongelea suala la Makanikia hapa Bugarama kwa sababu wanajua wameharibu. Wanajua hayakuwa maamuzi mazuri.
Lazima tufanye mabadiliko ya kweli kwa kuikataa CCM na kujenga upya Uchumi wa nchi yetu na kurudisha Demokrasia yetu.