Madhara ya kuvuta sigara

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125

Mwili wa mvutaji sigara


Kila sekunde nane, mtu mmoja hufariki kutokana na utumizi wa tumbako. Imebainika kuwa saba kati ya wavutaji sigara kumi, huanza uraibu huu wakiwa wangali watoto. Wanaoendelea kuvuta sigara kwa muda mrefu hufupisha maisha yao kwa miaka 20 hadi 25. Sababu ni kuwa sigara ina kemikali zaidi ya 4,000 ambazo zina uwezo wa kudhhuru afya ya binadamu. Madhara yanayosababishwa na uvutaji sigara ni mengi na yamesambaa mwilini kote. Yafuatayo ni baadhi tu ya maradhi yatokanayo na utumiaji wa tumbako.

Yaliyomo



1.Kung'oka kwa nywele

Uvutaji sigara hudhoofisha kinga ya mwili na kisha kudhuru mizizi ya nywele . hii husababisha kung'oka kwa nywele mapema.

2.Magonjwa ya macho

Wavutaji sigara hupata magonjwa ya macho mara nyingi kuliko wasiovuta. Sehemu ya macho inayopitisha mwangaza inaweza kufichwa kama vile wingu linavyoficha jua(yaani kwa ikimombo) na kusababisha upofu. Ugonjwa huu husababishwa kwa njia mbili. Kwanza moshi wa sigara huwasha macho na pili kemikali zilizo ndani ya sigara hupita kwenye mishipa , damu na hatimaye kudhuru macho. Sigara pia husababisha kudhoofika kwa sehemu ya kati ya macho(retina) na hivyo kupunguza uwezo wa macho kuona vizuri na hata kutofautisha rangi(macular degeneration).

3.Kukunjana kwa ngozi

Kemikali zinazopatikana ndani ya sigara hupunguza uwezo wa ngozi kujirekebisha hivi basi ngozi huzeeka haraka na kupoteza uwezo wa kulainika. Mvutaji wa sigara huonekana mzeee zaidi kuliko umri wake haswa.

4.Magonjwa ya masikio

Uvutaji sigara huleta magonjwa mengi ya masikio . Sababu ni kwamba uvutaji wa sigara husababisha uchafu kuganda kwenye mishipa ya damu na hivyo kupunguza mwendo wa damu hadi kwenye sehemu za ndani za masikio. Moshi na kemikali za tumbako pia hujeruhi sehemu za ndani za masikio na majeraha hayo yanaweza kuambukiza hata ubongo(menengitis). Yote haya yanaweza kusababisha uziwi.

5.Saratani ya ngozi

Uvutaji sigara unasababisha saratani ya ngozi. Kemikali za sigara husababisha vidonda kwenye ngozi na ambavyo haviponi kwa urahisi. Baada ya muda hugeuka kuwa saratani.

6.Magonjwa ya meno

Sigara hutatiza mdomo na kuongeza uchafu unaoganda kwenye meno hivi kusababisha kuoza kwa meno, harufu mbaya mdomoni na uchafu wa meno. Sigara pia hutatiza kupona kwa vidonda hasa baada ya kung'olewa kwa jino. Saratani ya mdomo na ulimi inapatikana zaidi kwa wavutaji sigara na watumiaji wa tumbako za aina nyingine.

7.Magonjwa ya mapafu

Uvutaji wa siagara ndio sababu kubwa zaidi ya saratani ya mapafu. Pia husababisha kupasuka kwa vibofu vya hewa safi na kutoa harufu mbaya mwilini. Wavutaji pia hupata saratani ya koromeo na kuziba njia ya hewa na hivo basi inabidi kutobolewa kwa kishimo kwenye shingo hili kuwezesha mwadhiriwa kupumua.

8.Mifupa

Sigara inasababisha mifupa kuwa myepesi na kupunguza nguvu. Sababu ni kuwa kemikali zilizoko ndani ya sigara hupunguza uwezo wa mwili kujenga mifupa iliyo na nguvu. Mifupa kama hii huvunjika kwa urahisi na kuchukua muda mrefu sana(asilimia 80 zaidi ya mifupa ya kawaida)kupona.

9.Ugonjwa wa moyo

Sigara ndio sababu kubwa zaidi ya magonjwa ya moyo. Inasababisha moyo kupiga kwa kasi zaidi na hivyo kuongeza msukumo wa damu mwililni( high blood pressure). Mwishowe husababisha mshtuko wa moyo na hata kifo.Moja kati ya kila vifo tatu ulimwenguni hutokana na magonjwa ya moyo na huua zaidi ya watu milioni moja kwenye nchi za Afrika.

10.Vidonda vya tumboni

Sigara hupunguza uwezo wa mwili kujikinga dhidi ya viini vinavvyosababisha vidonda tumboni. Pia hupunguza uwezo wa tumbo kustahimili nguvu ya asidi baada ya kula. Vidonda vya mvutaji basi huwa ni vigumu kutibu, na mara nyingi hutokea tena baada ya kupona.

11.Vidole

Kutu ya sigara hukusanyika na kuganda kwenye kucha na vidole vya mvutaji. Kisha hubadilisha rangi ya vidole na kucha kuwa za manjano au maji ya kunde. Ngozi ya vidole pia hukauka na kuwa ngumu sababu ya joto na kemikali za sigara.

12.Wanawake

Sigara huongeza hatari ya kupata saratani ya fuko la uzazi(cancer of theuterus ). NI vigumu zaidi kwa mwanamke mvutaji sigara kutungwa mimba na ni rahisi sana kwake kumpoteza mtoto katika mimba.(miscarrige). Uvutaji wa sigara pia humfanya mwanamke kumzaa mtoto aliyekufa(stillbirth) au aliye na uzito usiotimia wa kawaida. Watoto hawa huwa na afya duni baadaye. Sababu ni kuwa kemikali za sigara hupunguza mwendo wa mtoto kukua akiwa angali mimbani. Sigara pia husababisha ugumba(menopause) kabla ya wakati wake. Sigara pia inaweza kumfanya mwanamke kuwa tasa.

13.Wanaume

Sigara inapunguza mpigo wa damu kwenye sehemu za uume. Sigara pia huharibu mbegu za wanaume na kwa hiyo watoto wanaowazalisha huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata magonjwa ya saratani. Sigara pia huwafanya wanaume kuwa tasa.

14.Magonjwa ya ngozi

Sigara huleta magonjwa mengi ya ngozi kama vile uvimbe, kuwashwawashwa na hudhoofisha hali ya ngozi.

15.Ugonjwa wa ‘Buerger'

Huu ni ugonjwa wa uvimbe kwenye mishipa ya damu ya miguuni na mikononi. Mishipa hii huzibika na kuzuia mwendo wa damu kwenye sehemu zilizoathirika. Isipotibiwa kwa haraka,mvutaji anaweza kukatwa miguu au mikono.

16.Saratani

Zaidi ya kemikali 40 zinazopatikana kwenye tumbako zimethibitishwa kusababisha saratani. Ukilinganisha na asiyevuta sigara :

16(a).Mapafu

Mvutaji ana uwezekano wa mara 22 zaidi wa kupata saratani ya mapafu

16(b).Pua

Mvutaji ana uwezekano wa mara 2 zaidi kupata saratani ya pua.

16(c).Ulimi

Mvutaji ana uwezekano wa mara 2 zaidi kupata saratani ya ulimi.

16(d).Tumbo

Mvutaji ana uwezekano wa kupata saratani ya tumbo mara 3 zaidi.

16(e).Figo

Mvutaji ana uwezekano wa kupata saratani ya figo mara 5 zaidi.

Saratani Zinginezo

Uchunguzi unaonyesha kuwa saratani ya mdomo ni hadi mara 27, koo(mara 12), koromeo(mara10).Uchunguzi pia umebaini kuwa kuna uhusiano fulani kati ya uvutaji sigara na saratani ya matiti.

Chanzo: Madhara ya kuvuta sigara - Wikipedia, kamusi elezo huru
 
Mkuu MziziMkavu utawaambiaje wananchi wa Tabora na mikoa mingine wanaotegemea Tumbaku, na serikali inayopata mapato makubwa kutokana na zao hili?
 
Mkuu MziziMkavu utawaambiaje wananchi wa Tabora na mikoa mingine wanaotegemea Tumbaku, na serikali inayopata mapato makubwa kutokana na zao hili?
Watani wangu Wa Tabora na mikoa mingine iIabidi waache kulima hilo zao la tumbaku kwa sababu lina madhara makubwa Kuvuta Sigara kuna madhara makubwa kwa binadamu ingawa jambo hilo serikali inatambuwa na kulifumbia macho kwa sababu kuna kipato kingi kinachotokana na uuzwaji wa sigara.
 
tatizo hata nikiprint na kumpelekea mzee asome hatoacha coz alishaacha na amerudia kwa kasi wastani wa kuvuta sigara 25 kwa siku...
 
tatizo hata nikiprint na kumpelekea mzee asome hatoacha coz alishaacha na amerudia kwa kasi wastani wa kuvuta sigara 25 kwa siku...
jaribu Ku Print kisha umuonyeshe hayo madhara ya kuvuta Sigara. Unajuwa hili tatizo la kuvuta sigara kuacha kwake mpaka uende kwa doctor kisha doctor ikiwezekana akutishe kuwa usipoacha kuvuta sigara utakufa kwa

ushauri huo huenda ukaogopa kuendelea kuvuta sigara. Marehemu
Baba yangu alivuta sigara kwa muda wa miaka 50 kisha alivyokwenda kwa doctor, Daktari akampa maagizo mazito aliacha mbona ilikuwa mwaka 1980 sasa na wewe jaribu kufanya huo mpango aDoctor wa kumtisha baba yako huenda iksaidia hayo mawazo yangu.
 
adesf1.jpg


image010.jpg


1298211491-28.jpg


badlung.jpg


smoking-health-effects.jpg


How%252BTo%252BStop%252BSmoking%252B%252BQuit%252BCigarettes%252B%252BBest%252BWay%252BStop%252BEffects%252B%252525281%25252529.jpg


NEED I SAY MORE?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom