Madhara ya chumvi nyingi ni yapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madhara ya chumvi nyingi ni yapi?

Discussion in 'JF Doctor' started by Thinker2, Jan 4, 2012.

 1. T

  Thinker2 Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana Jf naomba ushauri,mi tatizo langu ni kutumia chumvi nyingi kuliko kawaida yaani msosi ukifika mezani naongeza kabla ya kuonja...!?.Bila shaka ingekuwepo tuzo ya watumiaji chumvi ningechukua Afrika mashariki na kati,Record niliyoiweka nilikuwa naweka chumvi kwenye chapati za kusuma mezani!?
  Naomba nijue madhara na jinsi ya kuacha...
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,151
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Chumvi mbichi ya kuongeza mezani madhara yake ni pressure na stroke 100%
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kula chumvi nyingi kunaweza kupelekea matatizo ya FIGO, MOYO na UBONGO.

  Anza kupunguza taratibu, unaweza ukaanzisha utaratibu wa kutoweka chumvi mezani wakati unakula, au kisiwekwe chumvi kabisa jikoni ili ukiweka (mezani) usiwe unaongeza bali unaweka kiasi kile kile ambacho hua unaongeza, huku ukipunguza taratibu.
   
 4. T

  Thinker2 Member

  #4
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante@Lizzy
  Mbona cna pressure wala stroke na kwenye ukoo wetu tupo kama watano hv...@King kong
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu, umenichekesha sana huu uzi wako, lakini pia mimi nimekuwa natumia chumvi sana, naweza hata kula hivihivi

  ushauri uliotolewa wa kupunguza chumvi ni mzuri, je? alternatively unaweza ukatumia ukatumia vyaku gani ili kuweza kufanya upunguze matumizi ya chumvi nyingi
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Haiji mara moja, huko ndani kutaharibika taratibu mpaka siku mwili utakaposhindwa kustahimili kwahiyo usidhani kwasababu tu hujapata mpaka sasa hivi basi you are off the hook. Chukua tahadhari kabla ya hatari.
   
 7. G

  Geka Senior Member

  #7
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lizzy kakueleza vema, kusema unatumia tangu kitambo isiwe sababu ya kudhani chumvi nyingi haina madhara, tumia kiasi, madhara yanayotokana na matumizi makubwa ya chumvi (hasa hiyo unayoongeza mezani!kha, na ile LAT anayotafuna) na ni bora sasa uanze kupunguza.

  Ulishajaribu kula mchicha usotiwa chumvi? saladi aka kachumbari isiyotiwa chumvi?
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kama unaweza ukapata Soy sauce hapo ulipo basi nunua. Yenyewe ina chumvi kidogo waweza kuwa unaweka badala ya chumvi. Ila muhimu zaidi ni wewe kuanza kujizoesha kula chumvi kidogo taratibu, kila wiki/siku punguza "a pinch" (kiasi unachoweza kushika na vidole vyako viwili) , utaenda ukizoea.
   
 9. The last don

  The last don JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  Ili kujua kama ni tatizo au laa tuambie je unaweza kuweka chumvi kwenye chai au juisi soda etc?..nadhani kuweka chumvi kwenye ngano si ajabu sana na wala haijaonesha kwamba umevunja rekodi ya wala chumvi kiongozi.kama uwezi weka chumvi kwenye soda,chai,juisi,etc na bado u feel some taste on sweets then usiogope bado chumvi unayotumia ni ya kiwango cha kawaida labda issue usipende kuiongeza on table,madhara ni kama yaliyoainishwa na wachangiaji waliopita.

   
 10. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #10
  Jan 5, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  chumvi


  Stori kuhusu chumvi:
  Tunapata chumvi nyingi kwenye vyakula vyetu siku hizi. Chumvi nyingi itasababisha shinikizo la damu, uvimbe, matatizo kwenye kibofu cha mkojo, matatizo ya moyo na orodha inaendelea.

  Tunaambiwa chakula chenye chumvi kidogo au kisicho na chumvi kabisa ndicho bora kwa afya zetu.


  Ukweli kuhusu chumvi:
  Mpaka zama za pili za mawe (middle stone ages), hakuna chumvi iliyokuwa mbaya. Waharifu waliuliwa gerezani kwa kupewa chakula bila chumvi, iliwasababishia kifo cha taratibu.  Miaka 2000 iliyopita, chumvi ilitumika kama hela. Dhahabu na Chumvi vyote vilikuwa na thamani sawa. Neno 'salary' (mshahara) linatokana na neno 'salt' (chumvi).

  Hapa kwetu Tanzania, watu hutumia msemo, 'Nimekula chumvi nyingi' kumaanisha kuishi miaka mingi.

  Katika siku hizo za kale, chumvi ilitumika pia kuhifadhia vyakula. Siku hizi tunatumia rifrijereta, kwa hiyo chumvi chache inahitajiwa isipokuwa kwa matumizi machache ya kusokotea nyama.

  Wanyama wote wenye damu moto, lazima wawe na chumvi ili kuishi. Ubongo wa binadamu pamoja na uti wa mgongo, vimo katika mfuko wa maji chumvi uitwao 'cerebrospinal fluid (csf)'. Umajimaji huu huzunguka sehemu zote za ubongo na uti wa mgongo.

  Sote tulitumia miezi tisa kuishi katika mifuko ya uzazi ya mama zetu inayoelea kwenye maji chumvi (amniotic fluid).

  Machozi yetu ni chumvi na tunatokwa na jasho ambalo pia ni chumvi. Mifupa yetu ina uwazi katikati yake (uboho) ambamo seli za damu hutengenezwa. Uboho huu umefunikwa na tabaka nyingi za chumvi kalisiamu kama vile kamba inavyoshikizwa pamoja. Kowa chumvi (salt crystals) zinashikizwa pamoja na kalisiamu, na kowa hizi ndizo zinazoifanya mifupa yetu kuwa imara, na siyo kalisiamu pekee.

  Mifupa inamiliki asilimia 27 ya chumvi yote mwilini. Wakati mwili unahitaji chumvi zaidi, huikopa toka mifupani, jambo hili likitokea, kalisiamu huondolewa pamoja na chumvi na kuifanya mifupa kuwa miembamba, laini na midhaifu.


  Chumvi imeundwa kwa Sodiamu na Klorini, kwa pamoja inaitwa; 'Sodiamu kloridi' (Na Ci).


  Sodiamu ni metali laini yenye chaji chanya (+), wakati Klorini ni gesi yenye chaji hasi (-) ambayo hubadilika kuwa katika hali ya umajimaji inapoongezewa shinikizo.

  Klorini ni gesi au umajimaji, lakini kwa namna fulani wakati dunia imeumbwa, klorini ilibadilika kuwa ngumu pamoja na sodiamu na madini mengine. Unaweza kuisaga chumvi na kuwa katika unga, klorini bado itabaki na sodiamu.


  Klorini katika hali ya ugumuugumu, huitwa Kloridi.

  Chumvi tutumiayo siku hizi inatoka katika bahari, maziwa, mito au katika migodi ya chumvi. Zaidi ya sodiamu na klorini, chumvi yote kwenye sayari yetu huja pamoja na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake!.


  Kwa hiyo tunaweza kuona ni jinsi gani madini hayo yalivyo na umhimu kwetu, la sivyo yasingeshikamanishwa na chumvi. Kwa sababu ya thamani yake kibiashara, madini hayo huondolewa ili kutengeneza faida kubwa.
  Mwili wa binadamu una uwezo wa kuienguwa klorini kutoka katika sodiamu kadiri inavyohitajika. Damu yetu huihitaji klorini kama zifanyavyo ogani zingine ndani ya miili yetu.


  Tumbo huitumia klorini kutengeneza haidrokloriki asidi inayohitajika ili kuuwezesha mfumo wa umeng'enyaji chakula kufanya kazi vizuri.

  Miili yetu pia huitumia sodiamu kloridi kama chumvi kuufanya ubongo, uti wa mgongo, machozi, mifupa, tezi za jasho, ogani na damu kufunikwa na chumvi.


  Mwili unanufaika pia kutoka katika madini mengine yaliyomo katika chumvi ili kuuweka katika hali ya ualikalini na afya.

  Ni kama na vile kwa kunywa maji kuzidi kunaweza kumuua mtu (hyponatremia), vivyo hivyo kwa kutumia chumvi kuzidi, kunaweza sababisha; uvimbe, kuharisha na kifo.

  Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini madini na hupitishwa katika joto la nyuzi joto 1093. Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha kemikali kama vile 'aluminium silicate' huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki katika hali ya unga. Aluminium silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo wetu wa fahamu. Inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

  Sodiamu iliyozidi inaweza kutokea kutokana na kula vyakula vingi vyenye viongezi (additives) vya sodiamu. Sodiamu siyo chumvi, chumvi ni sodiamu-kloridi. Sodiamu bikaboneti,sodiamu benzoeti na monosodiamu glutameti (msg) ni baadhi ya viongezi hivyo.

  Sodiamu, potasiamu na kloridi ni elektrolaiti (madini maalumu) ambayo huyeyuka katika maji na kubeba chaji za kiumeme na kuzipeleka sehemu zozote za mwili kuliko na maji. Madini haya yenye chaji za kiumeme yana uwezo wa kuingia na kutoka ndani ya seli kwa uhuru wote, huku yakipeleka lishe ndani na kubeba nje taka na maji yaliyozidi ili kuiacha seli katika hali yake ya usawa (balanced cell).

  Wakati huo huo, kadiri elektrolaiti hizi zikitembea ndani na nje ya seli na kufanya mabadiliko yake, usawa maalumu wa Potasiamu ndani ya seli lazima utunzwe kwa kiasi maalumu cha sodiamu na kloridi ili kuishikilia potasiamu ndani katikati ya seli.

  Elektrolaiti zinapatikana kwenye majimaji yote mwilini na hubeba mapigo (impulses) kwenye neva zetu. Kitendo hiki huusaidia moyo na kiwambo cha moyo (diaphragm) kusinyaa na kulegea.

  Elektrolaiti hubeba Glukozi (damu yenye sukari) na kuipeleka ndani ya seli baada ya Insulini kufungua milango kwa ajili ya sukari kuchukuliwa.

  Elektrolaiti pia huwasha pampu za kuzarishia nguvu ziitwazo kwa kitaalamu 'Cation pumps' ambazo huzarisha umeme ambao huifadhiwa kwenye beteri zijulikanazo kwa kitaalamu kama 'mg Adenosine Triphosphate (mgATP)' na 'mg Guanosine Triphosphate (mgGTP)' za mwili.

  Ikiwa mtu atapungukiwa kwa kiasi kingi cha Elektrolaiti hizi kutokana na kuharisha au kwa sababu ya dawa za kukojosha (diuretics), anaweza kuwa mgonjwa sana na itamlazimu kwenda hospitali kupewa elektrolaiti hizi katika mfumo wa dripu (intraveneous fluid, IV), kama vile; maji chumvi (saline solution), maji sukari (dextrose fluid) na madini.

  Siku hizi vinywaji vyetu vingi baridi vinaongezwa kafeina ambayo ni kikojoshi kinachoyalazimisha maji kutoka ndani ya mwili na kutusababishia upungufu wa maji mwilini (dehydration).


  Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, hakuna kinywaji ambacho ni mubadala wa maji.

  Wanasayansi na madaktari bado hawaelewi ni kwa jinsi gani chumvi huyeyuka ndani ya maji au ni kwa vipi iwezavyo kuendelea kuwa na hali ya uchumvi na uchumvi. Wanasayansi na wanakemia wana baadhi za nadharia, lakini bado hawajaweza kuzithibitisha. Bado imebaki kuwa ni fumbo (mystery).

  BAADHI YA KAZI ZINGINE MHIMU ZA CHUMVI MWILINI:  • Chumvi huyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli. Inarekebisha uwiano sawa wa kiasi cha maji yaliyopo nje ya seli. kuna bahari mbili za maji ndani ya mwili, bahari moja imejishikiza NDANI ya seli, na bahari nyingine ya pili imejishikiza NJE ya seli. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa ujazo wa maji uliopo baina ya bahari hizi mbili, na usawa huu unawezeshwa pekee na chumvi, chumvi ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi.
  • Chumvi husaidia kuondoa dalili za mfadhaiko (stress).
  • Figo hazitaweza kufanya kazi zake vizuri bila chumvi.
  • Kukata tamaa na matatizo ya kisaikolojia, vitaondolewa kwa kuchukuwa chumvi zaidi, kula mlo kamili na kufanya mazoezi ya kutembea.
  • Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida yanaweza kurudishwa katika hali yake ya kawaida kwa kuchukuwa kipande cha chumvi na kukiweka mwishoni mwa ulimi na kukifanya kiyeyuke.
  • Mifupa inapata uimara wake toka katika chumvi, na siyo katika kalisiamu pekee.
  • Je wewe ni mwanaume na unashindwa kuhimili kusimama? unahitaji chumvi zaidi na kunywa maji halisi zaidi.
  • Kuichukuwa chumvi na kunywa maji kabla ya mazoezi, kutakusaidia kupumua vizuri na kutokwa na jasho chache.
  • Matatizo ya kibofu cha mkojo na upotevu wa mkojo wa makusudi, vingeweza kurekebishwa kwa kuongeza chumvi zaidi kwenye mlo wako.
  • Dalili za maumivu ya jongo (Gout) zinaweza kuzuiwa kwa kutumia chumvi.
  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia kuvimba kwa mishipa na vena kwenye miguu.
  • Kwa sababu tunapata potasiamu karibu katika kila chakula tunachokula, chumvi inatakiwa kuongezwa katika milo yetu, hii itairuhusu miili yetu kuhimili usawa sahihi wa maji kati ya bahari ya ndani na ile ya nje ya seli.
  • Chumvi ni mhimu ili kuondoa asidi iliyozidi kwenye seli, hasa seli za ubongo.
  • Chumvi ni mhimu kwa ajili ya kusawazisha kiasi cha sukari kwenye damu, hivyo kuzuia ugonjwa wa kisukari.
  • Chumvi ni mhimu katika uzarishaji wa nguvu umeme itokanayo na maji katika seli zote za mwili.
  • Chumvi ni mhimu katika mawasiliano ya neva na ufanikishwaji wa taarifa wakati wote seli za ubongo zinapofanya kazi tangu kuzaliwa hadi kufa.
  • Chumvi ni mhimu katika umeng'enywaji wa chakula na madini kwenye utumbo mdogo (intestinal tract).
  • Chumvi ni mdhibiti madhubuti dhidi ya histamini.
  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia mikakamao ya mishipa (cramps).
  • Chumvi ni mhimu katika kusafisha makohozi na kubana kwa kifua.
  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia uzarishaji wa kuzidi wa mate katika kiwango kwamba yanatoka nje ya mdomo wakati umelala, kitendo hiki cha kutoa mate (udenda) wakati umelala ni dalili ya upungufu wa chumvi mwilini.
  • Chumvi ina umhimu mubwa katika uimarishaji wa mifupa. Ugonjwa wa mifupa (osteoporosis) kwa sehemu kubwa, ni matokeo ya upungufu wa chumvi na maji mwilini.
  • Chumvi ni mhimu katika usafishaji wa makohozi mapafuni na maji yaliyogandamana hasa kwa watu wenye pumu, ikiwa inakulazimu kusafisha koo kila wakati, ni dalili kuwa umepungukiwa chumvi.
  CHUMVI KIASI GANI:
  Dr.Batmanghelidj anashauri; ¾ (robotatu) gramu za chumvi kwa kila nusu lita ya maji (16 ounces), au nusu kijiko cha chakula kwa kila nusu galoni ya maji, au kijiko kimoja cha chakula kwa kila galoni moja la maji tunayokunywa. Hiki ni kiasi kizuri kwa kuanzia na siyo kanuni, tafadhari tumia aina ya kijiko kilichotajwa hapo juu kwa vipimo sahihi.


  Ukiona viwiko, vidole au kope za macho zinavimba, usitumie chumvi kwa siku 2, kunywa maji halisi pekee na kisha siku ya tatu, endelea kuchukuwa chumvi tena.  NAMNA ZA KULA CHUMVI:  • Njia ya kwanza ni kuiweka chumvi katika sehemu ya mbele ya ulimi, hakikisha unaihisi radha yake, na kisha kunywa maji juu yake yakiisafisha kuelekea chini.
  • Unaweza pia kuongeza chumvi ya ziada kwenye chakula chako.Tatizo la njia hii ni kuwa, chakula kinahisika kuwa na chumvi zaidi ya radha zingine.
  • Unaweza pia kunywa nusu ya maji unayotaka kunywa, kisha utamung'unya taratibu chumvi mdomoni kama ulavyo pipi, na kisha umalizie nusu ya maji iliyobaki.

  kuichanganya chumvi pamoja na maji ya kunywa si wazo zuri sana.

  je chumvi husababisha BP?, bonyeza: http://maajabuyamaji2.artisteer.net/shinikizo-la-damubp/
   
 11. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  jiandae na magonjwa ya kizungu kama lile gonjwa la importance, uume unao, lakini ndio huo uko likizo
   
 12. T

  Thinker2 Member

  #12
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hayo maneno tu hata wanasiasa wanayo@Nazjaz
   
 13. N

  NIMEKIMBIA CCM Senior Member

  #13
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka pole kwanza kwa tatizo lako,ushafahamu madhara ya ku2mia chumvi kwa mh Lizzy,sasa hakikisha unafuata na utaratibu aliokuambia u2me,
   
 14. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Sweet poison!
   
 15. MissyNana

  MissyNana Member

  #15
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaribu kutumia kutumia maji ya ndimu au limau, pilipili manga pamoja na kitunguu swaumu hivi vinaongeza ladha ya chakula kuliko kutumia chumvi.
   
 16. L

  LAT JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  @ Lizzy & MissyNana

  thank you for your valuable advice

  nitajitahidi kuzingatia ushauri mlionipa
   
 17. N

  Nguku mapera New Member

  #17
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uwe na utekelezaji kwa ulo elekezwa!
   
 18. N

  Nguku mapera New Member

  #18
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na vp pilipili?
   
Loading...