Mabibi na mabwana awamu ya tano imepita na sasa kazi inaendelea katika awamu ya sita chini ya Rais Samia.
Kwamba tupo awamu ya sita itakuwa kutojitendea haki mno kutoyaangazia kabisa madhara ya awamu ya tano kwa awamu ya sita yote chanya na hasi.
Kwa uzi huu itoshe kuyaangazia madhara hasi ya awamu ya tano kwa awamu ya sita.
Haikuwa ajali kwa awamu ya tano kujikita katika kujitanabaisha kwa nguvu zote kuwa ilikuwa ni ya wanyonge. Yaani wapiga debe, machinga, mama lishe, bodaboda na wa namna hiyo. Makundi haya yatoshe kuwakilisha aina ya philosophy iliyokuwa ikizisukuma agenda za serikali ya awamu ya tano.
Aina ya mafikara ya watu hao ndiyo yaliyokuwa yakiichezesha ngoma yote ya kiutawala tokea juu hadi chini. Ndiyo maana hadi leo, hata bungeni kunasikika wazi wazi sauti zenye kuhimiza kutambuliwa ubora wa wahitimu wa darasa la saba dhidi ya maprofesa au wasomi kwa ujumla.
Imani potofu zilizoambatanishwa na Corona zikiwamo upigaji nyungu, maombi, michai chai, malimao nk ni mwendelezo wa mafikara au philosophy ya watu wa makundi hayo.
Kwenye awamu ile, upepo wa mafanikio serikalini ulilihitaji zaidi kundi hilo la wasioelimika. Watendaji wakiwamo Mawaziri na wote wenye njaa zao walilazimika kuukana ukweli na hata kuzikana taaluma zao ili kuweza kukubalika kundini.
Ya akina Gambo leo na wote wanaoitisha kutolaumiwa kama wao binafsi, bali hali nzima ya utawala iliyokuwapo wakati huo ni mwendelezo wa matokeo hayo hayo.
Tulipo leo chanjo ya UVIKO ipo njiani kuja. Bila shaka jambo hili ni la kheri kabisa. Lakini si ajabu kuwa hii nalo litakutana sasa na kundi lile lililokuwa limeaminishwa kuwa ugonjwa haupo, bali ni vita vya kiuchumi tu dhidi ya Tanzania. Tena kuwa chanjo ni biashara na zaidi sana ni sumu dhidi ya Waafrika na hasa Watanzania.
Siyo siri tuko pabaya sana bila ya kuyashughulikia madhara haya yaliyopandikizwa kutokea awamu ya tano wakati ilipokuwa katika kujitafutia uhalali wa kuwepo kwake.
Matatizo tuliyo nayo kuhusiana na kundi hili yanapaswa kufahamika ili kuweza kupatiwa ufumbuzi kamili. Hii ikiwa ni wa muda mfupi na hatimaye wa kudumu.
Kuuishi ukweli na haki hata kama kwa kufanya hivyo pana machungu yake ni mambo yasiyoepukika.
Awamu ya sita imerithi kundi kubwa la wajinga na "the brainwashed to be catered for." Lenye mtizamo hasi katika elimu, sayansi na teknolojia. Kunatakikana jitihada kubwa za dhati na za pamoja katika kuyaweka mambo sawa.
Ni vizuri kufahamu kuwa tuna kundi kubwa la watu wasiojua nini wanataka au nini hawataki. Hii ikiwa ni kwa sababu tu ya kukosa elimu kulikokolezwa vilivyo na kupotoshwa kulikofanyika kwa makusudi.
Ya DC na DED Morogoro ni mwendelezo wa yatokanayo na mitizamo ya kundi hili ambayo hayajapatiwa suluhisho.
Kwa pamoja tunaweza kuyaweka mambo sawa hatimaye. Hata hivyo si haba kutambua kuwa pana mlima mkali kweli kweli wa kupanda.
Penye nia pana njia.
Ninawasilisha.