Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,422
- 5,676
"Ukiwa kwenye taamuli unaona kilichokuwa kinaendelea akilini mwako wakati wote" Allan Lokos.
Zipi hasa ni baadhi ya FAIDA za kufanya taamuli vyema na mara kwa mara;
1. Taamuli(meditation) inasaidia kutengeneza furaha ya ndani- hii ni furaha halisi ya nafsini inayokufanya upate ridhiko na utimilifu wa kukata kiu la uhitaji na hivyo kujikuta ukiwa na amani na furaha isiyo na kifani. mf kuondokana na tamaa za kimwili na kidunia pia na hisia hasi.
2. Kujifunza kufurahia wakati uliopo- kuishi maisha yako kwa kufurahia kila sekunde inayohesabu ukijua tunaishi leo na si kesho.
3.Kuongeza umakini- kupitia practises za kuconcentrate na kufocus katika jambo moja muhusika ufikia kiwango cha kuziamulia na kuziongoza fikra zake kipi ni muhimu adili nacho kwa wakati huo hii umwongezea umakini na ufanisi katika mambo yake nakumfanya muhusika kuwa na mafanikio zaidi katika jambo halilonuia kufanya.
4. Mwenye kujali zaidi, mwepesi wa kusamehe, kuelewa hisia za wengine, usiyechukizwa kirahisi na vitu vidogo vidogo na hivyo kuwa msaada kwa wengine wanaohitaji faraja, amani au support.
5. Kuwa bora katika mengi utendayo pasipo hata wewe kulibaini hilo hasa ikilinganishwa na miongoni mwa marafiki na familia pasipo kujua hata kwanini inakuwa hivyo.
6. Mengi ufanyayo kwa kutia nia na juhudi ufanikiwa kwa asilimia zote bila ya makosa makosa.
7.Utaacha kasumba ya kuzungumzia vilivyofanywa na badala yake vitafanyika kadiri ya kuongea/mwono wako.
8. Yule "Mimi Ndiye" uanza kujidhihirisha kuwa "Mimi Ndiye" katika kila nyanja ya maisha yako.
Basi kama ilivyoada tunapozungumzia taamuli(meditation) mara zote tunaishia kwenye mazuri tu ila upande wa MADHARA au MATOKEO HASI huwa atuzungumzii, hivyo hili likanifanya nivutiwe kuchunguza na kuokota-okota vichache hili tuweze kushea yapi ni madhara ya kufanya meditation.
Nitayazungumzia madhara haya katika makundi makuu mawili yaani beginners na wazoefu.
Tukianza na kundi la kwanza la wasio wazoefu/wanafunzi ambao kwa asilimia kubwa kundi hili uwa halina viongozi/master uanzia katika mitandao mfano JF au kusoma habar hizi kwenye vitabu na kuyatekeleza kivyao haya ndo madhila yake:-
1. Kujaza kelele nyingi za fikra katika ubongo (katika siku za mwanzo wa meditation) kiasi cha kujikuta muda wote unawaza na kuwazua pasipo kukoma mpaka muda wa kulala.
2. Kichwa kuuma,kuchemka na kukosa usingizi inafikia wakati unahisi kizunguzungu au hali ya ubongo kuchoka na unahitaji kurefresh.
3. Uzembe na uvivu unaanza kukuingia taratibu kama hautokuwa makini muda mwingi utakuwa unautumia kwenye mambo hayo nakujisahau kuwa wapaswa kufanya kazi muda mwingi.
4. Kwa wasiofanya mazoezi tegemea kunenepa zaidi kutokana na ukosefu wa usingizi,mawazo na kuketi mno, kupata choo kigumu, kupata kiungulia kikali na kilimi/kansa kutokana na matatizo ya mabadiliko ya homoni nakuzidi kwa tindikali asidi tumboni kutokana na mambo ya kulala au kukaa muda mwingi sehemu moja huku mwili ukiwa haujongei.
5. Kuandamwa na fikra nyingi mbaya au ndoto za kutisha au attacks ukiwa macho au umelala ambazo ni illusions nasiyo halisia ambazo usipokuwa makini zinaweza kupelekea kupata matatizo ya shambulio la moyo, upumuaji, BP au kifo cha ghafla.
6. Kuanza kujitenga na vitu, watu na vyakula na kubadilika tabia mf. kutembea peke yako au kujifungia ndani ambapo kwako ni jambo jema ila kwa jamii na mazingira yanayokuzunguka tiyari ni tatizo litakalokugharimu kiuchumi na kimahusiano.
7. Kubaguliwa, kuchukuliwa oya oya tofauti na wengine na kuchelewa kimaisha mf. pale jamii kubwa itakapokuwa ikikutafsiri vibaya kama mshirikina au mtu back kutokana na matendo yako yasiyo normal hata ule ushirikiano wa kupata madili ya kimaisha usuasua watu wakishakuchukulia poa au mzee wa busara.
Haya ni baadhi tu ya madhila kwa wasio wazoefu, je kwa wabobevu yapi ni madhara ya meditation kwao;
1.Unatokomea zaidi nakuzama katika kina kirefu zaidi cha kutaka kufuzu na kuwa immortal. Hapa ndipo mgogoro wa nafsi unapoanzia. Mind (akili) haitaki kufa/kutoweka mazima wakati meditation ya kina nia kuu nikufanya akili inyamaze na kutokomea mazima hili uruhusu ufahamu wa ndani zaidi pekee utawale. Akili lazima ipambane kubakia.
2. Mwisho wa siku kama upo kwenye mstari mnyoofu wa taamuli unaishia kupoteza imani yako ya kiroho na dini pale unapofikia UKWELI. Kwa maana Ukweli hauna dini bali ni omnipresent.
3. Inategemeana na kwanini umeamua kufanya meditation lakini jua kwa kila jambo/tendo utakalo lifanya lina gharama yake na lazima utailipa kwa namna yeyote ile.
4. Kulala mara kwa mara pasipo kujalisha ulipo ilimradi umeridhia kufanya hivyo au kumeditate katika mazingira yeyote yale iwe ndani ya basi ukiwa safarini, darasani au kwenye kikao inaweza kukuponza, kukufanya uonekane wa ajabu au kukupotezea ufanisi.
5.Kutokujali watu wanakufikiria nini siyo mara zote ni sahihi licha ya hivyo unaweza kuwa mvivu na asiye tegemewa kwa lolote zaidi ya kuishi katika ulimwengu wa fikra na imagination zisizokuwa na uhalisia.
Mwisho nikupoteza kipindi kirefu cha maisha yako ukiwa ufanyi lolote la maana zaidi ya kukalia kumeditate.
6. Mahusiano ya kimapenzi, ndoa,familia, marafiki na jamii kiujumla uyumba kimtindo-
hii utokea pale unapokuwa unajitosheleza mwenyewe kihisia na nafsi inakosa kutamani, mfano kama ilivyo saikolojia ya kawaida ya kiumbe uonapo jinsia tofauti lazima uvutiwe kimapenzi.
Lakini wewe utajikuta mzito na asiye na hisia au mpango na mambo hayo hata kama demu/meni akifanya juhudi zote kukufukuzia au kukuonesha ishara yakukutaka kimahusiano itakuwa ni kazi bure hivyo utaishia kuwa mbinafsi wa hisia za kimapenzi na mahusiano na wengine kiasi cha kubaki na followers wachache mno au wewe peke yako.
7. Ukiwa katika hatua za enlightenment utajikuta mara kwa mara ni mtu wa kufanya meditation mno ambapo kwa muda mrefu ukiendelea na hali hiyo tegemea kukumbana na reflux oesophagitis na hapo ndipo utaanza kukumbana na vikwazo vya kutokunywa chai, kahawa, vitu yabisi au vyenye asidi au tindikali nakadhalika.
8. Ukiwa katika hizo hatua za juu ikiwemo mambo ya astray projection tegemea mara kwa mara kukumbwa na attacks usingizi.
9.Kupoteza uwezo wa kuota na hivyo hapo tegemea lazima usingizi pia uwe ni wa taabu kwa kuwa ndoto ni chanzo cha usingizi mzuri.
10.Kujihisi raha/starehe au ridhiko la nafsi linalozidi kiasi pia uboa nakufikia sehemu ya kuwa karaha, kwani maisha mazuri ni yale yenye balance kati ya utamu na uchungu au raha na maumivu kiasi.
Sasa meditation inapofikia kiwango hiki muhusika uanza kutamani lahiti na yeye ange-experience japo kidogo uchungu au kushea hali ya simanzi na wapendwa wake au kuwa kawaida kihisia au mguso kama wengine walivyo ila ndo hivyo haiwezekani kila kitu kwake ni sawa tu na utenda kwa hekima na usahihi muda wote.
11. Katika ulimwengu usiyoshikika au kuonekana unakuwa ni mtu aliyepiga hatua kubwa kweli kweli ila katika ulimwengu unaoonekana au wa kimwili unakuwa umeachwa mbali sana.
12. Ukibahatika kujiondoa katika utumwa huu ambao ni ulevi mbaya kama ule wa madawa ya kulevya au punyeto yaani ngumu kuacha,
Waliopitia wanadai kuna nafasi bado ya kujirekebisha na kuwa normal, isipokuwa kama utashindwa kujitoa itageuka kuwa merry go around maisha yako yote.
13. Wakati mwingine watu ugeuka kuwa egoistic (wabinafsi) na wenye majivuno pale wanapojihisi ni superior na wenye ufahamu mkubwa kuliko wengine.
14. Wengine hujikuta wakianza kuishi maisha ya fantasies na illusions nakadhalika.
Naomba nikomee hapa maana orodha ni ndefu ila chakushika hapa kisikuponyoke ni kuwa;
Katika hii dunia tuishio ukweli juu ya ridhiko upatalo katika matokeo CHANYA kupitia matendo yako katika chochote kile kina gharama yake ya kulipiwa.
Na matokeo HASI ndo malipo yake.