Suala la medical misinformation na disinformation limekuwa likisababisha binadamu kujitibu au kupata tiba zisizo sahihi.
Watu wengi wanaosumbuliwa na ugonjwa wa ngozi maarufu kama mba wamekuwa wakishauriwa kutumia mafuta ya breki kujitibu. Wasiwasi wangu ni kuwa, kweli mwili wa binadamu unaweza kuhimili kuchakata viambata vilivyo kwenye mafuta hayo bila kuacha madhara makubwa kwa binadamu?
Kuna sehemu nimesoma kuwa matumizi ya mafuta ya break kwenye mwili wa binadamu hupelekea matatizo ya ini na figo.
JamiiCheck naomba mnisaidie hili, naamini majibu yenu yatasaidia wengi sana maana matumizi ya mafuta ya breki kutibu mba ni makubwa sana.